Friday, November 30, 2012

Stoo za jikoni.....

Leo naomba tuangalie upande wa stoo zetu za jikoni, mpangilio ukoje? usafi je? shelf nazo zina hali gani.....ama kama hauna shelf ufanyaje?

Tumekua tukijisahau kwa upande wa stoo za jikoni, na mpangilio sio mzuri.....kumbuka stoo hii mara nyingi mahali hapa ni pakuwekea akiba ya chakula.....sasa kunatakiwa kuwe kusafi muda wote, maana ukipaacha ndio panakua ni chanzo cha panya, mende etc...kuweko mahala hapa....

Nimeweka baadhi ya picha ya jinsi unatakavyoweza kuweka mpangilio mzuri wa stoo yako...iwe kubwa ama ndogo... zote zinatakiwa kua katika hali nzuri na kuwafi muda wote....






 Kama tunavyoona mpangilio, unatakiwa kuweka vyakula kwenye makopo yanayoonyesha ndani, kama ni ya glass ama plastic na kama hauna basi weka lebo ili utakapo kua unataka kutumia basi iwe ni rahisi kujua nini uchukue na urudishe kiurahisi
 Inategemea na stoo yako imekaaje...kama ni ndogo basi tengeneza shelf kulingana na ukubwa wa stoo. kama hii inayoonekana hapa ni ndogo...




 Kwa mpangilio wa vitu, vitu vizito siku zote vinatakiwa vikae chini, nikimanisha ndoo za mafuta, madumu etc.... na usichanganye chakula na vitu visivyo ni chakula.....









Baadhi ya design za stoo.....najua mpaka hapa utakua umepata wazo la vipi utengeneze stoo yako ama ui karabati etc...

Nawatakia weekend njema......

Wednesday, November 28, 2012

More wallpapers...available @ Homez Deco.....


Wallpapers ziko za kila rangi, karibuni mno....na nina furaha kwamba sasa mnaweza kuzipata ofisini kwetu, na kubandikiwa ukutani bila ku chajiwa zaidi.....

Niliulizwa na mdau kua hizi wallapaper nazipata wapi?
Jibu ni kua ninaletewa kutoka South Africa na USA.......

Wallpaper za jikoni na bafuni sina....ila zikifika nitawajulisha humu humu

More Pillows & Pillow cases....available @ Homez Deco...




Mito na foronya ni nyingi kukidhi mahitaji yenu....karibuni nyote....

Tuesday, November 27, 2012

Mbolea za garden......na Mrs. Jossyanne George from USA

Hizo pictures ni baadhi ya maeneo ambayo tumefanya kazi za gardening kama mnavyoona, mbolea ni muhimu sana, udongo unaostahili  maji, yawe ya kumwagilia yawe ya mvua ni muhimu, hapo tulikuwa tunaweka mbolea kwenye miti maua, sehemu mbalimbali za gardens, si kwamba ukiishapanda miti basi umemaliza  kuna kuongeza mbolea majani,  plunings kuna vitu vingi sana vinavyoitajika ktk kuboresha gardens,zikaonekana nzuri na za kuvutia,   

Huku new york tunatumia mbolea aina ya mulch,  na hizi mulch kuna za ina tofauti kuna red mulch kuna black mulch kama mnavyoona hapo kwenye picha.

kwetu sisi black mulch ni nzuri, ina ubora zaidi na mimea yawe maua iwe miti bushes vinastawi sana, jambo lingine wapendwa ni vifaa ktk hii kazi ya landscaping vifaa vya kufanyia kazi ni muhimu sana  vinarahisisha kazi, unaokoa muda, na nguvu, maana mfano mzuri ni Dar watu wa gardens wanachukuwa mrefu kumaliza kazi,, kwa kuwa wengi wao hawana vifaa ya proper gardening tools, ila ninawapongeza sana wanafanya kazi kupendezesha jiji,

 majumbani sehemu za bihashara, nawaomba watanzania wenzangu tuyapende mazingira yetu tunayoishi, pandeni miti, maua unakuta mtu amejenga nyumba nzuri tu ila mazingira ya nje ya nyumba ni yakusikitisha,  iweje ugaramikie jumba la garama ushindwe garden nzuri ?  

baadhi ya watu wanasubiri mvua zinyeshe wafungulie septic tanks mtaani,malundo ya takataka mbele za nyumba zenu uchafu kila kona , hii ni hatari sana vyanzo vya maambukizi yamagonjwa, chloea, kipindupindu, huu wote ni uchafu uchafu, jitaidini wapendwa kuwa wasafi kuyasafisha mazingira mnayoishi,usafi ni muhimu sana ktk afya zetu, majumbani, kwenye mikusanyiko ya watu, , kwenye migahawa, shm za kazi  

haya yote ynaanzia ngazi ya familia, mpaka  taifa   jitaidi wapendwa, nasisitiza usafi kiujumla, wa mazingira, mnayoishi ziwe nyumba za kupanga au yakwako binafsi usafi ni wajibu  na  muhimu sana    yalinde yatunze mazingira yaliyokuzunguka daima,  

mungu awabariki na kuwalinda  




Ukimya wa Jossyanne George ..........


Wapendwa wa blog ya garden & landscapings natumaini hamjambo, na familia zenu, nilikuwa kimya sana
 ni kwa sababu nilifiwa na baba yangu mzazi, mzee josiah mwesiga.  nilikuwa tanzania  kwa muda mrefu, nachukua furusa hii kuwashukuru wote, waliotufariji ndugu, marafiki,  na jamaa na jeshi la polisi viongozi wa serikali. na  viongozi wa dini. nawashukuru sana,

 kwa niaba ya familia mzeeJJ M WESIGA .


  

Swali kutoka kwa mdau....



Hi,naitwa angela ninapenda blog yako coz huwa ninapata ideas nyingi nzuri kwa kuboresha nyumba yangu.ninaomba unisaidie namna ya kujiunga gnld au kama unaweza niunganisha na mtu ambaye atanisaidia kujiunga nao.ningependa kuwa nanunua bidhaa kwa ajili ya nyumbani kwangu hasa sabuni ya kufulia.nitashukuru sana kwa msaada wako.
stay blessed.

Jibu, 
Naomba tuwasiliane kwa namba hii 0713 - 920565 nikupe maelekezo, maana hukuweka contact yako niweze kukuelewesha.
Na kwa kujiunga unakua unanunua kwa bei nafuu....Karibu

Monday, November 26, 2012

Wallpapers...Available @ Homez Deco...



Wallpapers ni karatasi za urembo ambazo hubandikwa ukutani. Waweza bandika ukuta mmoja ule wa tv kwa sebuleni na chumbani ule ukuta ambao hauna madirisha.....

Wallpapers, inatakakiwa kubandikwa kwa uanvalifu mkubwa, maana inabidi ukuta uwe ni mzuri na msafi yaani usiwe na mchanga mchanga,

Homez Deco tunakuja kukubandikia sisi wenyewe, ukinunua....

Kwa hesabu za haraka haraka wallpapers zinaweza kuingia kwenye ukuta mmoja kuanzia mbili mpaka tatu, inategemea na ukubwa wa ukuta wako.....Hivyo utakapochagua tunapima ama utapima urefu na upana ili kujua tunapata square meter ngapi, ndio tupate idadi zinaingia ngapi....

Kumbuka muda ni mchache kuelekea sikukuu,
Karibuni .......

Site ya Kigamboni.....Homez Deco tuliweka Kabati la nguo la Mninga....

 Hili ndilo kabati languo la mninga muonekano wake wa nje.....mteja alihitaji kabati litakaloweza kuhifadhi nguo za watoto wa kike wa wili na kama atatokea mgeni basi nae anaweza akaweka nguo zake hapo....na wote waweze kuweka viatu....
 Kabati muonekano wa ndani.....Kama unavyoona Kushoto na kulia kuna fanana, nikiwa na maana ya kwamba, kuna sehemu ya ku hang nguo, kuna sehemu ya ku kuweka nguo zilizokunjwa, na kuna droo mbili kila upande, na katikati ndio sehemu ambapo mgeni akija basi ana uwezo wa kuweka nguo hapo bila kusumbua wengine.....na chini ndio sehemu ya kuweka viatu....
 Kama kawaida, nikiwa nimepozi mbele ya kazi yangu baada ya kuikagua na kuridhika nayo....

NB:
Mbao nzuri kwa makabati ni mninga, mkongo, kwa wale wanaojiweza...na kuna mbao zingine ambazo ni mpodo, etc.....Mbao ni gharama hasa kwa kipindi hiki ambacho miti haikatwi katwi ovyo.....

Mninga ama Mkongo, ni imara na hupendeza sana.....

Waweza pia kutengeneza kabati la nguo la MDF, ni haya makabati ya ready made.....ambayo tunayaona madukani....ila sio imara kwakweli, na hayataki shida, kama kuhama hama, etc...

Karibuni sana kwa mahitaji ya makabati ya nguo, ya jikoni, etc.....

Homez Deco tutakuja kupima nyumbani kwako ama sehemu utakayotaka tukuwekee...maana hatupokei vipimo vya mteja.....na kukupa bei kulingana na design, na mbao uliyoichagua.....

Friday, November 23, 2012

Dulux Paints........




Hizi ndio rangi za Dulux, ukiangalia kwanza kabisa ndoo zilizotumika kuhifadhia rangi hizi, ni nzuri na zinavutia.....na kwa upande wa matumizi, rangi hizi hubana matumizi sana kwa utumiaji wake, yaani sehemu ya kutumia ndoo 3 wewe utatumia ndoo 2......kwa mfano hicho kindoo kidogo ni lit. 5 kinatosha kabisa kupaka chumba kimoja...... sasa fikiria ndoo ya lit. 20.....

Rangi hizi mzionazo hapo juu, zinatosha kwenye nyumba ya vyumba 3 vya kulala, jiko, dinning, sebule, na nje ukuta wa nyumba nzima......

Kwa upande wa bei, ni mpaka nijue ni rangi gani utahitaji kwani kadri inavyozidi kubadilika ama zile rangi tofauti tofauti kama pink, green, blue etc...bei ni tofauti....

Tayari tumeshaanza kupokea orders za rangi za Dulux na wadau/wateja wetu wanazifurahia na kuzipenda kwani mkombozi wa kubana matumizi amewasili Tanzania......na rangi hizi hudumu ukutani kwa muda wa miaka 8-10.......bila kupauka ama kubadilika rangi yake......

Karibuni mtoe order.....wasiliana nasi kwa simu namba 0713 - 920565 ama email: sylvianamoyo@yahoo.com

Sofa Repair.....

Kuna mdau alinitumia swali, kua kama anataka kubadilisha sofa kitambaa inawezekana?

Jibu ni kua, kwanza niione hiyo sofa, na pia inategemea na uchakavu wake. maana kuna zingine zimechakaa mpaka zile mbao za ndai zimevunji. sasa kwa sofa ya aina hiyo hua nina shauri ununue ingine...maana ukarabati wake utakua ni mkubwa, tena karibu sawa na kua sofa mpya....

Naomba ndugu wadau, muwe mnanitumia picha ya sofa zenu ili niweze kuziona kabla ya kutoa jibu....nitumie email sylvianamoyo@yahoo.com

Karibuni sana........

Metal Furniture....

 Furniture zikiwa tayari kwenda kwa mteja.....
 Poziiii.........................
Nikiwa nimepozi kwenye kazi yangu......Kwa kweli hua ninaona raha sana pale ambapo nimefanya kazi na imetoka safi na nzuri....Nimeweka rangi hizi tunaziita neutral colors, mteja wangu anapenda rangi hizi......

Hapa ni wakati kabla hazijaondoka kwenda nyumbani kwa mteja....ziko ofisini kwa nje.......seti ya hii sofa ni ya watu watatu 2 na yawatu wawili 1.......


Naomba ijulikane kua hiki ndicho kipindi cha kujiandaa kutengeneza kwako, ama kujiandaaa kumalizia nyumba yako na kuhamia, ama kupamba nyumba yako......Karibu sana Homez Deco tutakusaidia kwa hili......

Pillows & Pillow cases available at Homez Deco.....(all these products designed and made by homez deco)












 Mito na foronya za watoto zinapatikana pia.....







Animal print foronya pia zinapatikana....hii ndio size ya mito ya sofa ya mapambo

Mito ndio hiii, kila size utapata......ya kulalia, ya makochi, etc......


Mzigo wa X-mass ndio huo unaaanza .......tuna mito na foronya za kila aina......hizo ni baadhi tuuu....

Bei ya mito kwa size hii ni bila foronya zake:

1. 55 by 38 = tshs. 18,000/-mito ya kwenye sofa/makochi, kitandani


2. 45 by 45 = tshs. 15,000/-mito ya kwenye sofa/makochi, kitandani


3. 40 by 40 = tshs. 15,000/-mito ya kwenye sofa/makochi, kitandani

4. 45 by 30 = tshs. 12,000/- mito ya kwenye sofa/makochi, kitandani

5. 88 by 88 = tshs. 45,000/- mito ya chini sakafuni



Bei ya foronya za mito kwa size

 55 by 38 = tshs. 13,000/-

2. 45 by 45 = tshs. 12,000/-

3. 40 by 40 = tshs. 12,000/-

4. 45 by 30 = tshs. 10,000/-

5. 88 by 88 = tshs. 15,000/-


Kwa sababu muda ni mdogo mno mpaka sikukuu......Homez Deco tunayo furaha kukuarifu kua,  tutafanya delivery....na utalipia 10,000/- kokote uliko......utapata mzigo wako ukiwa salama......kwa upande wa malipo tunapokea tigo pesa, m-pesa kwa namba ifuatayo 0713 - 920565.....muda ni mchache mno ....karibuni sana.....