Wednesday, September 9, 2009

Vyumba vya watoto wetu

Tumekuwa tukisahau vyumba vya watoto wetu, Hii ni sehemu muhimu pia. Kupamba chumba cha mtoto sio kazi sana.

Kwanza jaribu kumdadisi mtoto wako anapendelea nini? (magari, madoli, kuchora etc.) 

Pili jua rangi gani anapenda, ila hii ni kwa wale watoto walionza kuelewa rangi, tumekuwa tukijua ya kuwa watoto wa kiume,ni rangi ya blue na wa kike ni rangi ya pink. Ila sio lazima waweza kupaka rangi mbalimbali na kukapendeza pia.

Mimi napenda sana uumpe nafasi mtoto akipambe chumba chake hata kama ni wa miaka 2 na kuendelea. Hili linawezekana. Mpe karati achore, weka picha kwenye fremu, itundike ukutani

hiyo michoro yake ukutani ama weka ubao mdogo chumbani kwake na hii itasaia kwa wale watoto wanaopenda kuchora ukutani hapa ni kwa wale wanaopenda kuchora. 

2 comments:

  1. nimekuelewa sana dada yangu ila mimi nina watoto wawili mmoja wa kiume na mwingine wakike na kila mmoja anakipaji chake kwa kweli nimjitahidi kuwapa kila kitu lakini mh huyu wa kike anapenda sana midoli nikamnunulia midoli kila aina wakiume anapenda sana kuchora na ndivyo watoto wengi wananpenda lakini mma yangu hicho chumba hata ukupamba asubuhi ukienda dukani na ukirudi utadhani hakijasafishwa kina miaka miwili hebu nipe utaratibu nini nifanye kwa hawa wanangu mana nawapenda sana

    ReplyDelete
  2. asante sana kwa comment na swali lako zuri, ila hujaniambia watoto wako wamepishana miaka mingapi. Sasa Chumbani kwa hao watoto nakushauri tumia rangi za wash 'n' ware. rangi hizi zikichafuka unaweza kufuta kwa dasta lenye maji na sabuni na zinadumu.
    Baada ya kupaka rangi, usijaze sana vitu vingi chumbani kwa watoto hawa, kumbuka wanahitaji kucheza, hivyo jitahidi kuacha nafasi kadri uezavyo, tafuta mahala pa kuhifadhia vitu vyao vya kuchezea eg, vitenga vyenye urembo ama tengeneza droo kwenye hivyo vitanda vyao etc. Huyo wa kiume yeye mwekee ubao ukutani kwa ajili ya kazi zake, sio mbaya ukampa karatasi akishachora akupatie uzifrem chumbani kwao (akizoea hivyo atakuwa akichora anakupatia na wewe ndie unachagua uzifanyie kazi gani na kutakuwa hakuna kutupa tupa makaratasi hovyo). na pia jaribu kuwa nao karibu na kuwaelewesha wapi pa kuhifadhi vitu vyao vya michezo. naamini mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, watoto ni wa kueleweshwa na kuelekezwa wakizoea wanafanya.kwani watoto wa kizungu wanawezaje na wa kwetu washindwe? kwa maelezo zaidi tuwasiliane (sylvia - homez deco).

    ReplyDelete