Monday, July 1, 2013

Wallpaper kwenye ukuta unaokaa TV, sitting room...........

 Matumizi ya wallpaper kwenye nyumba zetu. Wallpaper ni karatasi za urembo, ambazo ni maalum kwa kuwekwa ukutani, na zinabandikwa na gundi, ziko za aina nyingi, kuna za aina nyingi, za bafuni, jikoni, hizi ni tofauti, na kuna za sitting room na chumbani hizi zinatumika kote kote.


Hizi picha ni mifano ya wallpaper inavyoonekana ikiwa imeshawekwa, na wallpaper ziko za rangi tofauti tofauti, na utahitajika kununua wallpaper iendane na fanicha zako ama rangi zisipishane sana, la sivyo kutachusha, na kuchukiza. Mwanga pia ni wakuzingatia, ili wallpaper iweze kuvutia na kuongezeka na kua na mvuto.
 Kitu kingine ni kua wenzetu wakiweka flat screen tv ukutani, huoni nyaya zikining'inia, na hii nitakuja kulizungumzia hivi karibuni, kwani utakuta nyumba zingine, nyaya nyingi zaidi, zina ning'inia na hakupendezi....
 Wallpaper hubadilisha muonekano kwa haraka na ni nafuu. maana unabandika na haziharibu ukuta. bandika kwenye ukuta wa tv, na kwenye kuta zingine, rangi inaendelea kubaki, ama


karibuni kwa mahitaji ya wallpapers......bado sale inaendelea @ roll 50,000/- na ina urefu wa mita 10 na upana 53 cm.

No comments:

Post a Comment