Monday, July 1, 2013

Mr. & Mrs. Joe.....wamefika Tanzania......

 Leo nimepata suprise, mrs. Jossyanne amekuja tayari, kumbe tokea ijumaa, sasa wakawa wanataka kunifanyia suprise, mdogo wake akanipigia simu akaniambia, ananiletea mteja mchana.. Haya nikajiandaaa, na kuja ofisini kuja kusubiria mteja.......Hee mara anaingia na Jossyanne....yaani nilifurahi mnooooooo. mpaka nikashindwa kuongea kwa muda tumebaki tumekumbatiana........na mumewe nae tukasalimiana, yaani hua ananicheka, kua nina mwili mdogo, basi hua ananibeba, ananiambia jamani uko hivi hivi kila siku......hahhaahahhahaha.....

Wako ofisini kwetu, na wakitizama rangi za Dulux color chart yetu......na tukaongea mawili matatu........

Mimi na Jossyanne tumejuana kupitia blog... mwaka ule ule nioanzisha blog mwezi 8 mwaka 2009.   Alinipigia simu na kusifia ninachokifanya, na tukawa tunawasiliana mara kwa mara.....na mwisho wasiku, tumekua ni ndugu, sio marafiki sasa.......

Tunashauriana, maisha, biashara etc......blog imeniletea marafiki, na wengine wamekua ni ndugu sasa......

Yeye ndie mama wa ubatizo wa Jaydan wangu......

NB:
Mrs, Jossyanne ataanza kupatikana kikazi kuanzia tarehe 20/7/2013   karibuni mtoe appointment, na muweze kusaidiwa katika swala la gardening & landscaping in a proffessional way.........

1 comment:

  1. Msalimie Jossyanne, my school mate

    ReplyDelete