Monday, January 16, 2012

Our work, hii ilikua alhamisi na ijumaa last week.... Curtain poles....Kazi hii ilifanyika siku mbili, maana umeme ulikatika, na kazi hii iko awamu mbili, nyumba ndio mpya wamehamia, so wameanza na hizo curtain poles, halafu tutakuja maliza na mapazia etc....... ukipanga kila kitu kinawezekana, ....... tutawaletea awamu ya pili, vyumbani rangi ya ukuta ni green, na sitting room, dinning, corridor ni butter scotch....

Baada ya kazi, ninajiandaa kuondoka, yaani nywele ni tim tim, so ndio ninajiweka fresh hapa........

Niko tayari sasa kwa kuondoka, katika kazi zangu hua ni lazima niwepo, kuhakikisha kila kitu kimekwenda sawa na kwa wakati............ Tunasubiri pazia sasa........... nakushukuru mteja wangu........ Tulikua mbagala-Kijichi.


NB: Hua ninapiga picha katika kila kazi zangu, na kuwaletea hapa na zingine ninaweka kwenye album/portfolio file. sasa kuna wateja wengine wamekua wakikataa nisipige picha kazi zangu, ila ninachotaka kuwaomba na kuwaambia ni kwamba, hua sitaji ni nyumba ya nani wala kutoa details, kwa ajili ya usalama, na kama ningekua sipigi picha, nadhani nisingekua ninapata kazi, na nisingekua na picha hizo za waliokubali nifanye kazi. napenda kuwashukuru wale wote wanaokubali nipige picha, na ninaendelea kuwaelimisha wale wote ninaofanya nao kazi, kua kupiga picha kazi zangu mnakua mnanisaidia.

7 comments:

 1. HI MAMA J, HIVI CURTAIN POLES UNAZITENGENZA AU, JE PRICES ZIKOJE? AU INABIDI MTEJA AWE NAZO WE NI KUFITISHA TU. URGENT PLEASE MANA NAZIHITAJI

  ReplyDelete
 2. dada wewe umrembo na unaonyesha chapa kazi, ila mi naomba niende off topic. Profile pic yako ni nzuri na inaonyesha jinsi gani ulivorudia shape yako ya uschana, but i guess it is too revealing kua kwenye front page, ni hilo tu mpenzi, yani ni mapaja zaidi kuliko homedecoz

  ReplyDelete
 3. kazi nzuri hongera.
  je bei zikoje za poles na kuweka kwa dirisha kwa sisi walala hoi
  asante

  ReplyDelete
 4. Kazi nzuri mama J.
  NB:
  Nina swali naomba msaada wako eti Eyelet curtain zinapendeza kuweka living room? na je kama nikizihitaji hapo kwako unazo? Thanks

  ReplyDelete
 5. Hi anonymous wa 1, Curtain poles ninatengeneza mimi mwenyewe, na tunakuja ku fitisha sisi wenyewe, bei kwa dirisha moja full set ni tshs. 70,000/- na inachukua siku saba kua tayati kwa nyumba nzima.

  ReplyDelete
 6. Habari anonymous wa 2, nashukuru sana kwa compliment, ila nimeweka picha hiyo kwa kua niauza products, za shear butter, na ninajitahidi watu watumie products hizi maana kwanza ni orignal, hazichubui, na ni nzuri, sio mpaka mtu atumie mkorogo ndio aonekane mzuri..... I hope umenielewa.(nitabadilisha baada ya muda)

  ReplyDelete
 7. Hi anonymous wa 4, hailet design inapendeza sana katika kila chumba, haijalishi ni chumba gani, na pia inatakiwa iwe na marinda mengi yaani yakutosha ndio inapendeza. hapa kwetu homez deco zinapatikana, sasa basi natakiwa nijue ukubwa wa dirisha lako, (Urefu na Upana) ndio nikuambie zinaingia ngapi, na kitambaa ni mita ngapi.

  Naomba tuwasiliane kwa maelezo zaidi..

  ReplyDelete