Thursday, July 11, 2013

TATIZO LA PANYA .........SWALI KUTOKA KWA MDAU WETU.....


Mambo Homez Deco. 

Ninaishi nyumba ya kupanga nasumbuliwa sana na panya. hata wakiisha ni kwa kipindi maana wapangaji wenzangu hawatilii umakini na wanatoboa sakafu na kuingia ndani hata ukiziba mashimo wanatoboa tena. Nisaidie nifanyaje.

From,
Angel.


Tumepokea email hii kutoka kwa mdau wetu, kama isomekavyo kua anasumbuliwa na tatizo la panya nyumbani, na ningependa kumjibu kama ifuatavyo......

Kwanza kabisa panya wanapenda mazingira ambayo ni machafu, na kama ndio mnakaa wengi, basi ukiwa unaweka wewe dawa wenzio hawaweki, unakua haujatibu tatizo la panya kabisa.......

Kinachotakiwa ni kua, wote mkubaliane kuweka dawa, na pia mfanye usafi wa mazingira kwa ujumla.....na mshirikiane katika hili, na usafi uwe ni wa ndani mpaka nje, na ndio muweke dawa, na muendelee na utaratibu huo mpaka panya wakiisha, na uwe ni utaratibu wenu wote wa kuweka dawa mara kwa mara na usafi uzingatiwe......


Tunakaribisha maoni katika hili kumsaidia dada Angel.......


2 comments:

  1. Awekw dawa inaitwa indosine ni Tsh 500 tu, kwenye chakula wanachopenda kula panya awategee watakufa.

    ReplyDelete
  2. Indosine ni dawa ya binadamu kwaajili ya ugonjwa wa gauti, ila ni simu kwa panya.

    ReplyDelete