Thursday, November 24, 2011

Home flower arrangment - Tiger Lilies

Roses

Carnations

Janna nilifanya tour namanga mbuyuni na nilifanya mahojiano na wapambaji na waandaji wa maua, katika duka mojawapo, nilitaka kujua kama inawezekana kununua maua fresh na kuweka majumbani kwetu, badala ya haya ya plastics tuliyoyazoea.
Nilijibiwa kua inawezekana kabisaaa, sasa nilichagua maua hayo niliyoyashika yanaitwa tiger lilies. nilichagua rangi 2, nyeupe na zambarau.

Tukaandaa verse yetu, na kuweka maji kama inavyoonekana

Akachukua maua, na kuyafungua

Sasa hapa ni kwamba, ni lazima kukata shina la ua kwa kiupande, kila ua, hii husaidia kufyonza maji. na unatumia mkasi

Akaanza kuweka ua moja moja

na mengineyooo, na unapoweka uweke kwa mtindo wa kupishana, yaani design ya X. haihitaji uwe mtalaam

Na ua letu liko tayari, unaweza kuwe, kwenye dinning table, kwenye kona, etc. na sio lazima ukatumia verse ndefu, inategemea na sehemu unayotaka kuweka........ ua hili linakaa siku 4-5 ndio unalibadilisha(linakufa)

NB: watu wanasema hayo maji ni lazima uweke chumvi, magadi, etc ili likae sana, hapana usiweke chochote.

No comments:

Post a Comment