Tuesday, November 22, 2011

Curtain Poles - Nyumba ya kupangishwa


Wengi wetu tumejaaliwa kua na nyumba hapa mjini na tumeamua kuzifanyia biashara, ya kuzipangisha, ila sasa, wengine tuna kua wavivu kuzifanyia ukarabati, na hata ukifanywa basi ni wa juu juu, utakuta nyumba inachakaa kabla ya wakati,

sasa basi, nina wazo kwa hawa wenye nyumba, unajua kutoboa toboa ukuta kunachangia kuharibika kwa nyumba na hatimae kuleta ufa, hebu fikiria kila mpangaji anaeingia aweke curtain poles zake, hiyo nyumba itadumu kweliiii.

Hivyo basi mwenye nyumba una mamlaka yote ya uchaguzi wa nini kifanyike, amua kuweka curtain poles za design unayoipenda, hii itasaidia kufanya nyumba yako idumu. (ukiweka ac kabisa pia ni vizuri zaidi, yaani vile vitu vya ukutani we viweke kabisaaaa, ingawa picha za ukutani wao wapangaji wataweka, ila utaawaambia kabisa nini wafanye ukuta usiharibike)

asilimia kubwa kwenye issue za delivery hua ninakuwapo ili kuhakikisha kila kitu kiko sawa, na mteja anaridhika.

No comments:

Post a Comment