Wednesday, November 30, 2011

Hii tabia nilikua naisikia tuu..... Hili ni eneo la Tazara. mida ya saa 11:15am 30/11/2011
Duh, hatati tupu, hii tabia nilikua naisikia tuuu, yaani sasa leo ni live bila chenga, kama unawavyowaona hapo, kwanza gari la mafuta ya petrol, lilipokua linapunguza mwendo kwa ajili ya foleni nikaona vijana wanakimbilia, sasa mie nikajua labda kuna mtu kagongwa, si nikaanza kutoa macho, heee kumbe wanafuata gali la mafuta, jamani niliogopa, maana wanavyofungua kama kwamba walifunga wao, hawa vijana wako na mifuko ya rambo hapo unawavyowaona, sasa kule dereva na msaidizi wake nikawa najiuliza kwa nini hawashuki? heeehhee kumbe mafuta yamekwisha, sasa wao ndio wanachukua ya mwisho mwisho.

Jamani inasikitisha, na inahuzunisha. ni tabia mbovu na chafu sasa gari ikilipuka hapo, ni watu wangapi watakufaaaa..........

Na je wanaenda kuuza wapi hayo mafuta machafu... na hao wanaonunua wana akili kwelii...........

Naomba mamlaka husika mlifanyie kazi hili suala...........

NB: ila mgeniona ninavyopiga hizo picha, maana ninasikia hua wanafujo, na wanaweza hata kuvunja vioo vya gari na kadhalika.......

Ukiwa na tukio lolote lite usisite kunitumia, nami nitalipost, maana kwa kufanya hivi najua wahusika watapata tuu habari na itasaidia sana kuyachukulia hatua....

No comments:

Post a Comment