Tuesday, March 16, 2010

Vifaa vya usafi

Hivi ni baadhi ya vifaa vya usafi, mimi sielewi utamkuta mtu anafanya usafi bila vifaa muhimu, huo sio usafi, na ndio mwanzo wa uvivu wa kugusa sehemu zote za usafi.

Kuwa na vifaa vifuatavyo na hivi ni general vifaa:
  1. Ndoo ya usafi na dekio na hii iwe ni kwa matumizi ya usafi tuuu, ama kuna wengine huwa wanatumia mop pia ni nzuri tuu inategemea na uwezo wako.
  2. Fagio
  3. Kizoleo
  4. Dasta ziwe mbili ya kufutia vumbi, iwe mbichi na ingine kavu kwa ajili ya kukausha na ziwe ni cotton.
  5. Brash, ama hoover kwa wale wenye carpets.
  6. Spray bottle na sabuni yake.
  7. Fagio la kutoa buibui. etc
Ukiwa na hivi vyote nakuhakikishia utakusa kila kona ya nyumba yako kwenye usafi. Na hakikisha vitu ambavyo huvitumii tupa ama gawa. ACHA KUJAZA MATIVU USIYOTUMIA NI MOJA YA UCHAFU HUOOOOOO!!!!

No comments:

Post a Comment