Tuesday, March 16, 2010

General cleaning...

Hivi umeshawahi kwenda nyumbani kwa mtu na ukapishana na panya, mende buibui ukutani ndio usiseme etc,
Ila ukimuona anayeishi hapo barabarani, alivyopendeza.
Huwezi amini, jamani inatia aibu sana sana,

Tuwasaidieje hawa watu wa design hii?

mimi kwa mawazo yangu, je, nianze kupiga picha nyumba hizo na kuzitoa kwenye blog labda ataona aibu na kujirekebisha? ama tufanyaje?

Maana mie binafsi sioni sababu ya mtu unajipendezesha wakati unapolala kunanuka, yaani wengine utadhani wanafuga panya, ama mende, mimi binafsi ninavyoogopa panya, ninaweza hata kuahama nyumba.

Kuna siku panya aliingia nyumbani kwangu, jamani ilikuwa ni saaa nne usiku ndio nimerudi home nikakuta kala vitu baadhi, sikuweza kukaa humo ndani, nilimuita my hubby all the way kutoka kinondoni kuja kumtoa. Thanks lord alitoka.

Sasa u can emagine wanaoishi na panya wakati dawa za wadudu zipo, lol aibu......

Tuwasaidiaje hawa? na sio kwamba hawa uwezo, naijiulizaga maswali sipati majibu, ama ni hulka ya uchafu, lakini mbona anapendezea barabarani si nako angekuwa ni mchafu????

No comments:

Post a Comment