Friday, March 26, 2010

Pasaka imekaribia tumejiandaaje? Nyumba zetu tumeziandaaje? na je tunaweza kukaribisha wageni bila aibu ama kuficha baadhi ya vitu.

Kama kawaida, mtakubaliana na mimi kuna baadhi yetu tunafanya general cleaning mpaka ikifika kipindi cha sikukuuu, haya sikukuu hiyo imekaribia umejipangaje?

Najua mavazi mmeshaandaaa, vyakula vya kupika tayari mshajua mtapikanini, na mtakwenda kutembea wapi, hiyo yote ratiba iko tayari, lakini je nyumbani kwako kukoje, usafi je?

Kuna vitu vya kuangalia vya kurekebisha, baadhi ni
 1. Rangi ya ukuta
 2. Makochi yanahitahi kubadilishwa kitambaa
 3. Mito ya makochi yanahitaji kubadilishwa kitambaa
 4. Carpet linahitaji kuoshwa
 5. Toa bui bui kwenye kuta
 6. Fanya general cleaning
 7. Jikoni kusisahaulike
 8. Chooni chooni chooni huko ndio kabisaaaaa
 9. Vyumbani usafi
 10. Nje ya nyumba jamani
 11. Mapazia kama sio kubadilisha basi yafuliwe
 12. Mwisho kabisa uani, yaani huku mara nyingi wengi wetu ndio tunajisahau, kuchafu kuchafu kuchafu
Kwa usaidizi usisite kunijulisha karibu sana.

No comments:

Post a Comment