Thursday, March 25, 2010
Inasikitisha sana sana, na nimeshindwa kuvumilia........
Jamani kwanza natanguliza shukrani zangu za dhati, na nawaomba msamahaa wadau wangu wote, kwa kuwa this week nimelega lega ku upload blog hii yangu.
Mimi ni muajiriwa kwenye N G O moja hivi jina kapuni as a secretary/admin. Sasa kuna nafasi za kazi zimetangazwa na watu wame apply, kwa njia ya email na P. O. Box.
Njia ya email wangine hawa ja attach hizo documents, wengine wametuma tu CV etc. kama mtu huwezi kutumia email sio lazima tumia postal address na kwa Dar kwa Dar inawahi kufika.
Nimekuwa nikifungua hizo barua zao, lol nyingi ni vichekesho kwa kweli, na utakuta mtu ana degree, masters etc.
Najua sio kazi yangu na pia sio lengo la hii blogsite kwa yote hayo ila nimeguswa sana sana, kwani Barua ni utambulisho tuu na haitakiwi kuwa na mambo meengi mpaka employer akachoka kusoma. CV ndio ya kukuelezea wewe na ndio unajiuza kwa huyo new employer.
Kulikuwa na blogsite mpya ya kueleza jinsi ya kuandika barua za kuomba kazi, cv etc. ila naona siku hizi haja update muda mrefu sijui ni vipi.
Nawaomba wadau wangu tuingie katika hii mada tusaidiane kwenye mada hii mtuonyeshe jinsi ya kuandika barua za kuomba kazi na cv.
Tusaidiane kwa hili jamani, mimi nitakuwa ni mtu wa mwisho kuonyesha jinsi barua na CV zinavyotakiwa kuandikwa just Format.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hii ni kazi yako kwani jamii itajifunza kutokana na makosa, hivyo kueleza ukweli kwetu ni nzuri zaidi ili tujue kama hatujui. Mimi pia ni Secretary, huwa napenda kusoma sana mambo mbalimbali katika hii blog yako. Naahidi kuandika mfano wa Application letter moja kesho (Leo niko busy kidogo). wasomaji mkiona haifai, please do not hesitate to make some corrections.
ReplyDeleteNashukuru sana sana kwa comment yako, maana ninaweza kuona niko sawa kumbe ninakosea ndio maana nikaomba ushauri wako.
ReplyDeleteUkipata huo muda kesho pls do send the letter to me, then nii publish. Najua kwa kufanya hivi tutakuwa tumewasaidia wengi.
Jamani, yani uwa unanikamata lakini leo umenikumbatia kabisa.
ReplyDeleteHii ni habari nzuri sana. Ni wengi sana kati yetu tunafanya makosa sana katika pande hii, na wengi wetu utakuta kazi tunaweza, lakini vitu hivi vinatuangusha.
Tafadhali tupeni hiyo mifano wengi tupate kuelimika.
Hapa ofisini kuna wakati inabidi umsaidie mtu kuandika barua kabla hajaenda kwa boss, ni maroroso tu.
disminder.
Hi sylvia,
ReplyDeleteNimekutumia maoni yangu kuhusu Application Letters kwa email yako ya yahoo.