Wednesday, July 31, 2013

Moses busket Inauzwa.......


Imetumika miezi 2 tuuuuu bei ni 300,000/-

Wasiliana na 0657-417070 Sylvia. (ni wajina wangu)....

Ukarabati wa vyumba vyetu katika kipindi hiki cha kuelekea kusherehekea sikukuu.............

Tumeshazungumzia, sebule, dinning, korido, vyooni na sasa tunaelekea vyumbani na kisha tutakuja jikoni, na nje ya nyumba zetu.......

Katika eneo hili la chumbani, hapa ni mahali pa kupumzika, ama kulala unapohitaji, kama ni usiku ama mchana.......Mwili unahitaji kupumzika, na kama unahitaji kupumzika, basi hakuna budi chumba kiwe kisafi, kizuri, na kiwe na nafasi....

Hivi mi jamani hua ninashangaa kwakweli, kuona vyumba vimejaa vitu. na kama mnavyojua vyumba vyetu vya kulala hua ni standard size....kama ndio 12 by 12 ama 10 by 10....kama ni nyumba ya kupanga ama ni nyumba yako.......sasa kwanini mtu usiweke vitu ambavyo utavitumia, na kuliko kurundika vitu?

Kwa mfano, unakuta mtu kaweka kitanda 6 by 6, makabati , dressing table, shoe rack, stand ya pochi, na tv, kochi, hanger ya nguo etc......basi ni kurundika vitu tuuu

Cha msingi jamani kwanza angalia ukubwa wa chumba chako, na ikiwezekana ukipime kama hujui size yake....na baada ya hapo, weka vitu kulingana na ukubwa wa chumba......sasa utakuta chumba ni kidogo lakini mtu anaweka kitanda kikubwa ama kabati kubwa.....yote haya ni ya nini?

Na huko kwenye makabati kuna nguo nyingi mtu na zingine hazivaliki......yaani kabati mpaka linalemewa....sasa ukija kwenye viatu ni vingi mno, na vingine huvai labda kwa kuharibika, ama umevichoka....ila bado unavyo tuuuuu....

Naomba kushauri kua vitu ambavyo hutumii jamani GAWA......

Kwa kufanya hivi itakusaidia kupata nafasi na hewa izunguke katika chumba chako, kua na vitu vingi sio kupendezesha nyumba........

Kwani ukiweka vitu kulingana na chumba chako, tena kwa mpangilio kutakua na tatizo?

Kwa upande wa rangi za vyumbani, tafadhali rangi zipakwe zilizopoa, maana rangi nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa mno katika kukufanya u relax.....

katika vyumba vyetu tukumbuke pia usafi wa kina, ukianzia usafi wa cyling board, madisha, mashuka...etc.....

Dressing table zetu jamani hua tunazisahau.......mafuta yakidondokea hua yanaacha alama, vitana navyo....etc

Rangi hizo baadhi ni.................
 Kama rangi ina kiza, basi ipakwe kwenye upande mmoja wa ukuta na  kuta zingine ziwe na rangi ambazo ziko angaavu...

Thursday, July 18, 2013

Public Toilets and Bathrooms....

Umeshawahi kukutana na toilet ambapo ukipita kwenye korido, unasikia harufu mbaya inatoka na kusambaa korido nzima, ama kama tena na hiyo toilet iko karibu na sitting room ama dining room basi ndio harufu yote inasambaa................

Kumekua na tabia kwa asilimia kubwa, watu kudharau ama kuona kinyaa kufanya usafi kwenye vyoo....vya nyumba zao...ama kumuachia tuu msichana wa kazi afanye usafi ajuavyo bila kumfuatilia usafi umefanyika vizuri tena kwa dawa zinazotakiwa kutumika, maana utakuta ukuta una ukungu ama kutu , masinki nayo basi vurugu tuuuuuu.......

Tuesday, July 16, 2013

KORIDO ZA NYUMBA ZETU....


Naomba leo tuangalie upande wa korido, baada ya kua tumeshaona sitting room, dinning room........

Katika eneo hili, kwa upande wa kuanzia usafi na rangi ni muhimu sana kuzingatia
Korido nyingi hua hakuna dirisha ama madirisha...hivyo kunakua na kiza cha aina flan hivi.......kulingana na ulivyojenga.

Hapa kuna nyumba aina mbili: kuna ambazo ni fupi na kuna ambazo ni ndefu (urefu kutoka juu mpaka chini).......ingawa wengi wetu tunajitahidi kujenga nyumba ndefu kulingana na maendeleo na mabadiliko ya kila kukicha.

Mtakubaliana nami kua kwenye korido zetu hua zinachafuka mno, maana utakuta mtu akipita mwingine kashika na mikono yake michafu, ama mwengine anashika tuuu basi ilimradi tabu tupu, na hivyo kufanya korido kuchafuka, na kama ndio haukua umepaka hizi rangi za wash 'n' ware ama silk maana rangi za aina hizi hua unaweza kusafisha na maji na uchafu ukapungua ama kuisha kulingana na uchafu wenyewe.

Kama unaona ukuta wako hauridhishi, basi waweza kupaka rangi, kwa kuuandaa ukuta wako. Mwite mtaalam, akupe hesabu ya rangi inaingia kiasi gani na gharama zake na aina ya rangi.......hivyo atauandaa ukuta kwa kupiga msasa, na kuziba mashimo kama yako, nashauri mtumie skimming plaster smoothover za dulux, halafu apake rangi iliyokusudiwa kama ni za Dulux etc.......

Rangi za korido ni light colors, ama rangi zenye mwangaza......Kumbuka katika eneo hili hakuna madirisha hivyo mwanga kupenya ni asilimia ndogo mno, ni nyumba chache zenye madirisha katika eneo hili.

Sasa unapopaka rangi zenye kiza, korido inakua ni ndogo, na giza na haitakua na mvuto wowote, hata kama kuna taa ambazo utaziwasha wakati wa usiku.......

Baadhi ya rangi za kupaka korido ni hizi, ingawa inategemea pia na sitting room na dinning room umepaka rangi gani......

Dawa Ya Mende....

hongera sana kwa kazi nzuri unayofanya. nina shida moja nahitaji msaada wako nyumbani kwangu kuna mende sana kila sehemu , kama unaweza kujua dawa nisaidie hili nilitatue hili tatizo.  nijibu kupitia blog yako.

asante sana
mimi-Anna 


Homez Deco tumepata email hii kutoka kwa mdau wangu na anaomba usahuri kama inavyosomeka.....Na napenda kumjibu hivi.....

Unachotakiwa kufanya ni kutafuta sababu ya mende kuwa katika nyumba yako, na sababu ni kati ya hizi, :
1. hauweki vitu kwa mpangilio
2. nguo ni nyingi na ziko katika malundo
3. hautumii products nzuri za usafi
4. uchafu uliokithiri
5. mabaki ya chakula hayatupwi sehemu husika na kwa usafi
6. usafi pia haufanyiki ipasavyo etc...
Hizi ni baadhi ya points ambazo ningependa uzifanyie kazi.....kuanzia nje mpaka ndani....na inahitajika uache kazi ufanye kazi, nikiwa nina maana kua ujitolee siku moja ufanye usafi wa nyumba nzima.......ikiwezekana utoe vitu nje vipigwe na jua kwa muda hata wa siku mbili ama tatu, na ndani ufanye fammigation pamoja na nje.....
Kabla ya kuingiza vitu ndani, hakikisha unachagua vitu unavyovihitaji, usivyo hitaji kama viko katika hali nzuri gawa, kama havifai basi tupa sehemu husika.......

This time ingiza ndani vitu utakavyotumia na upunguze mlundikano wa vitu.....na usafi uwe ni wa mara kwa mara, na kwasababu umefanya fammigation, ile ni sumu fanya usafi vizuri........

NB:
Hakikisha unahusisha na majirani katika fammigation maana ukifanya wewe mende watakimbilia kwa wenzio. dawa ikiisha nguvu mende wanarudi.......

Homez Deco tunakaribisha ushauri zaidi.....


Friday, July 12, 2013

UPAMBAJI WA ENEO LA KULA CHAKULA ( DINING AREA)

Leo tuingie upande wa dining area, katika chumba hiki wengi wetu katika nyumba hua kinaangaliana na sitting room, na kwa wachache hua wamekitenga yaani kinakua na ukuta hukioni.....

Tuanze na kwa hawa ambao dining inaonekana......katika ukipamba chumba hiki, angalia kwanza unahitaji kiweje yaani kiwe na mandhali gani, na kisha angalia ni nini na nini ni cha kuondoa. kama kimechakaa ama kimekwisha, ondoa ili uweze kupata nafasi nzuri kwa kuweza kudesign.

Kwa wale wenye dining room inayojitegemea unaweza paka rangi tofauti maana humu kunajitegemea......

Ingia mitandaoni, ama nunua magazines za home deco...angalia mipangilio iliyoko huko na mpaka rangi.....halafu ukisha jua ni nini unataka, viandike, na uanze kutafuta, sasa hapa waweza kuja kwa mtaalamu wa mambo ya decorations (Homez Deco) ama ukafanya mwenyewe.

Fanya window shopping kwanza, na uangalie pia na ukubwa wa dining area yako.....wengi wetu tuna eneo dogo lakini bila kujua ama wengine hawajali, wanaweka meza kubwa ya watu 6 wakati eneo ni lakuweka meza ya watu 4.....hili jamani tuwe makini katika hili....(Kufanya window shopping inakusaidia kufanya manunuzi ndani ya budget uliyopangilia)

Thursday, July 11, 2013

MITO YA SOFA ........


 karibuni, mito bado iko.................

TATIZO LA PANYA .........SWALI KUTOKA KWA MDAU WETU.....


Mambo Homez Deco. 

Ninaishi nyumba ya kupanga nasumbuliwa sana na panya. hata wakiisha ni kwa kipindi maana wapangaji wenzangu hawatilii umakini na wanatoboa sakafu na kuingia ndani hata ukiziba mashimo wanatoboa tena. Nisaidie nifanyaje.

From,
Angel.



MAPAMBO YA SEBULENI (SITTING ROOM) KATIKA MAANDALIZI YA SIKUKUU.....


Homez Deco imeona ni vema kuanza kuangalia chumba kimoja kimoja katika upande wa mapambo kwa kadri ya uwezo wa mtu mwenyewe.....

Kuna kama makundi matatu hivi kwa upande wa kupamba nyumba zao....
Kundi la kwanza ni jamii ya Waarabu:
Mtakubaliana nami kundi hili la kwanza wao hupenda sana nyumba zao, kwa mapambo na hua ni mara kwa mara huzipamba.......

Kundi la pili ni wale wote wanaopamba nyumba ikikaribia sikukuu:
Kundi hili la pili lenyewe ni mpaka sikukuu ikaribie ndio nyumba zipambwe, na ikisha sikukuu basi inasubiriwa ingine.....

Kundi la mwisho ni wale wanaopamba kwa msimu......
Hili la mwisho wao ni kwa msimu, yaweza kua ni kila baada ya miezi 3 ama miezi 6 ndio wanapamba nyumba zao......


Wednesday, July 10, 2013

MSIMU WA KUPAMBA NYUMBA ZETU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUUU


Habari nduge wadau wangu wote kwa ujumla.......

Napenda kuwaletea mada ya kupamba nyumba zetu katika kipindi cha sikukuu......Yaweza kua ni kupaka rangi nyumba yako, kubadilisha fanicha kwa ujumla, ama kubadilisha mapambo yako ya ndani, ama pia kufanya set up ya mpangilio wako wa fanicha za ndani.....

Katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani, ndio muda muafaka wa kufanya maandalizi kwa ajili ya sikukuu ya Idd....usisubirie dakika za majeruhi ndio uanze kuhangaika kupamba nyumba yako....

Ukianza mapema hata na wewe pia inakusaidia kwa njia moja ama ingine kwa upande wa mapambo unakua haikupi tabu.

Sasa basi unachotakiwa kufanya ni kuangalia nyumba yako imekosa kitu gani, ama inahitaji kitu gani ili iwe nzuri naya kuvutia, ili hata wageni watakapo kuja basi usipate aibu, ama hata wewe mwenyewe, pia upate kusherehekea vizuri na familia yako....

Yaweza kua ni rangi ya nyumba......anza kutafuta mtaalam sasa ili uweze kujua gharama, na ujipange mapema hiii.......ama mapazia pia.......etc...

Karibuni sana Homez Deco kwa mahitaji ya kupambiwa nyumba yako na ushauri pia......


SITE YA MBEZI BEACH.....



 Rangi yoyote utakayo kwa ajili ya kitanda chako ama furnitures zako, utaipata hapa Homez Deco....Kitanda hiki ni cha mtoto wa kike ana miaka 5, na alitaka pink.....

SITE YA KUNDUCHI....


Design yoyote ile utakayo tunaweza kukutengenezea.......tulipeleka vitanda hivi:


SITE YA BUNJU.........

Homez Deco, tulipeleka vitanda site ya bunju.......


 Homez Deco tulitengeneza vitanda na neti zake.....na huu ndio muonekano baada ya kazi kuisha.....

Monday, July 8, 2013

KUPAMBA KITANDA KWA KUTUMIA MITO.......

 Mandhali ya chumba chako cha kulala ni wewe ndie unae amua kiweje, na kipendeze vipi......Hapa leo tutazungumzia jinsi ya kupamba kwa kutumia mito.....Katika upambaji wa aina hii kwanza kabisa hakuna kanuni ya uweke mito mingapi katika kitanda chako.....ni idadi unayoitaka wewe...kulingana na ukubwa wa kitanda chako.....Mashuka pia yanachangia kwa kiasi kikubwa mno kupendezesha chumba chako......

Thursday, July 4, 2013

JINSI YA KUWEKA FLAT SCREEN UKUTANI BILA NYAYA KUONEKANA......


Nakumbuka kuna siku niliwaambia kua nitawaletea makala ya jinsi ya kuweka flat screen ukutani bila nyaya kuonekana.....
Hili limekua ni tatizo kubwa miongoni mwetu, maana utakuta nyumba nzuri, sitting room nzuri ila kwenye ukuta wa tv nyaya kibao kiasi kwamba sasa inaharibu muonekano na kua kama uchafu.....

Wengi wetu, kwenye upande wa tv hua tunachukulia tuu ni rahisi kuiweka juu ya meza ama ukutani kwa kua ni flat tv basi haina neno, na tunasahau kabisa swala la nyaya zake kuonekana......Katika picha hizi hapo chini zinatuonyesha ni jinsi gani ya kuweka tv zetu ukutani kwa usafi.......

Maana tunajiuliza maswali mbona ukiangalia picha za wenzetu, wao tv zao zinakaa kiusafi...bila nyaya kuonekana? Jibu ni hili



 Kwa wenzetu, nyumba nyingi wanafanya partition, za mbao na  boards etc.....na zinakua na finnishing nzuri na huwezi jua kama ni partition.....hivyo inakua ni rahisi hata kutoboa na kurekebisha etc......

Sasa basi hata kwetu inawezekana, kama ndio unataka kuanza ujenzi, basi fuatilia katika hapa na mwambie archtech wako ama interior desiger wako kua hutaki nyaya zionekane na muanze maandalizi ya kuficha nyaya......Ukitumia wataalam inakua ni rahisi kwako kua na nyumba nzuri na ya kisasa......
 Wengi wetu hua hatutumii interior designers, ama tumekua tukiona gharama, ama hatutilii maanani katika swala hili...na mwisho wa siku unakuta nyumba imesha na haina mvuto....na kumbuka umetumia hela nyingi katika hili......

BADILISHA MUONEKANO WA SEBULE YAKO KWA KUWEKA MITO NA FORONYA .........ZINAPATIKANA HAPA HAPA HOMEZ DECO.....

Mito na foronya, tunaendelea na kuwaletea design mbali mbalimbali na kuweza kupendezesha nyumba yako....Tuna mito mikubwa ya kuweka chini, ijulikanayo kama floor pillows, ni size 75 by 75.

Mito husaidia sana katika kubadilisha muonekano wa sitting room yako, na usio na gharama kubwa........tuna rangi nyingi za foronya kulingana na mahitaji yako,

 Mito ya chini ama floor pillows.......size 75 by 75
 Mito ya makochi size 45 by 45

Tuesday, July 2, 2013

Michoro ya ukutani kwenye vyumba vya watoto....kuanzia mwaka 1-5

 Katika vyumba vya watoto wetu, hua tunaviacha tuu kuta zake zikiwa ziko plain,  na baadhi ndio siku hizi wanaweka wallpaper katika kuta hizo, Kuta ninazozizungumzia ni zile ambazo hazina madirisha, ama makabati, ni ule ukuta ambao unawekea kitanda, kama ndio headboard etc.......

SALE SALE SALE!!!!!! LEATHER SOFA........ SOLD

 Sofa set imebaki seti moja ya watu saba......ni leather ya ukweli.....sio za kubahatisha...ziko katika hali nzuri......zimetengenezwa nje ya nchi........sio zile za kwetu tunazozijua.......

Monday, July 1, 2013

MAFUTA YA SHEA BODY BUTTER & VASELINE........YAMEFIKA YANAPATIKANA HOMEZ DECO....WAHI SASA......

 Mafuta haya ya shea body butter, ni mazuri kwa ngozi ya aina yoyote ile, na hayachubui, yanakupa ung'aavu asilia wa ngozi yako.....nani orignal, .......tokea tumeaanza kuyauza sijawahi pata malalamiko ya kua kuna mtu yamemkataa, ama tatizo lolote lile,,,na ukikaa nayo vizuri, kopo hili linaweza kukufikisha hata miezi miwili......yanafanya ngozi yako iwe na moisture muda mwingi.....na hivyo unakua haupauki ngozi.

Mr. & Mrs. Joe.....wamefika Tanzania......

 Leo nimepata suprise, mrs. Jossyanne amekuja tayari, kumbe tokea ijumaa, sasa wakawa wanataka kunifanyia suprise, mdogo wake akanipigia simu akaniambia, ananiletea mteja mchana.. Haya nikajiandaaa, na kuja ofisini kuja kusubiria mteja.......Hee mara anaingia na Jossyanne....yaani nilifurahi mnooooooo. mpaka nikashindwa kuongea kwa muda tumebaki tumekumbatiana........na mumewe nae tukasalimiana, yaani hua ananicheka, kua nina mwili mdogo, basi hua ananibeba, ananiambia jamani uko hivi hivi kila siku......hahhaahahhahaha.....

HOMEZ DECO INAWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN.....

 Siku ya tarehe 30/06/2013 ambayo ni jana, kulikua na mkutano wa wanawake wa kiislam, na pia kulikua na maonesho ya biashara, tunashukuru Mungu nasi Homez Deco tuliweza kuwepo katika hili, na tukauza pia baadhi ya vitu, na mimi binafsi nilipata mawili matatu, katika mawaidha......

Wallpaper kwenye ukuta unaokaa TV, sitting room...........

 Matumizi ya wallpaper kwenye nyumba zetu. Wallpaper ni karatasi za urembo, ambazo ni maalum kwa kuwekwa ukutani, na zinabandikwa na gundi, ziko za aina nyingi, kuna za aina nyingi, za bafuni, jikoni, hizi ni tofauti, na kuna za sitting room na chumbani hizi zinatumika kote kote.