Thursday, June 14, 2012

Rangi za ndani za nyumba zetu........
Hili somo nimekua nikiliongelea kila mara..... na naomba mniwie radhi kama nitakua ninawaboa, ninasema hivyo kwa sababu, hili limekua ni tatizo kubwa kwetu, na nimekua nikilishuhudia katika kazi zangu huko niendako......
Nimeweka hapa baadhi ya charts ili mjionee ni jinsi gani ya kutumia rangi hizi ndani ya nyumba..... kama unataka kutumia rangi kali basi changanya na zilizopooza na zinazoendana, na zisiwe ni za giza....
Katika interior design, epuka kupaka ama kutumia rangi za giza, maana zinafanya nyumba inakua ni giza, ndogo, etc....
Mfano:
Waweza tumia rangi 3 kwa wale ambao wanapenda kuremba nyumba bila kutumia wataalam,, hii itakusaidia usijichanganye.
kwanza, unatakiwa kujua unapendelea nini? na unataka nyumba yako iwe na mandhali gani, kama ni ya misitu, bahari, etc......basi nenda na rangi hizo.... kama ni misitu basi tunajua kabisa rangi yake ni kijani, kama ni bahari rangi inakua ni ya sky, blue......
Hizi rangi ndio zinakua ni main color zako, yaani waweza zipaka ukutani, kinachofuatia, tafuta rangi inayoendana ya pili ambayo haita kua kali.. na hii ukaiweza kuitumia kwenye sakafu, carpet, tiles, etc...
Na mwisho, hiyo rangi ya tatu, itumie kwenye mapambo, pazia, viti etc...
na hapo utakua umemaliza ku pamba nyumba yako kama mtaalamu.....

Wengi wetu tumekua tukifanya makosa ya kutumia rangi nyingi bila mpangilio mzuri.... angalia baadhi ya picha hapo juu najua itakua imekupa mwangaza wa nini ufanye ili kuepuka makosa hayo....
Somo hili nitakua nikiliongelea mara kwa mara naomba tusichokane......
kwa maswali karibuni......

sylvia
Director....


3 comments:

  1. ASANTE MAMII TUNAAPRECIATE SANA KWAKUTUJALI MY DEAR.

    ReplyDelete
  2. Kweli hapo unatufungua macho, Mungu akuzidishie kipawa.....

    ReplyDelete
  3. nimeipenda hiyo!! si wote wanajua kutumia rangi, endelea kutuelimisha!

    ReplyDelete