Wednesday, January 23, 2013

Dustbin za jikoni..... Dustbin za jikoni mara nyingi hua zinasahaulika sana kusafishwa, na kama zikisafishwa basi hua hazitakati, na sabuni zinazotumika kusafishia, zinatakiwa ziwe zinaua vijidudu.....
 Haijalishi ni dustbin ya design gani unayo ama ni kubwa ma ndogo inategemea na matumizi yako.....Dustbin zinatakiwa zisafishwe kila siku, kama sio mara mbili kwa siku basi hata maramoja kwa siku......
Dustbin ziko za aina nyingi, niwewe tu unahitajika kununua kulingana na matumizi yako......


Umeona kwenye dustbin hizi kuna mifuko ya plastic...mifuko hii husaiidia sana kutokuchafua dustbin na kuto kuichakaza....na kwa usafi pia wa kabati chini ya sink.....

Jamani kuna kabati zingine za chini ya sink ambako dustbin zinakaa, hazifai, zimeoza, ama zina ukungu.....ama ndio mtu akitupa uchafu ndio basi unadondoka chini ......ilimradi tuuu ni shida....

Jitahidi kwenye dustbin yako hapo jikoni, kwanza iwe na mfuniko, hakikisha sink lako halivuji, na dustbin yako utangulize mfuko wa plastik, haijalishi ni mfuko wa rangi gani,

Mifuko hii hupatikana super markets, ama hata madukani pia hupatikana.... hakikisha unatanguliza kwa nza kwenye dustbin ndio uanze kuweka uchafu, na pia wakati wa kutupa takataka, usirushie jamani, maana uchafu unaweza kudondoka chini...usiwe mvivu kuinama na ndio utupe uchafu, maana utahakikisha uchafu umeingia mahala pake, na unafunga mfuniko......

Nawatakia siku njema....


No comments:

Post a Comment