Wednesday, January 30, 2013

Taa za urembo ....


 Hizi ni taa za urembo, ambazo hutumika sebuleni,ama vyumbani. ila pia hutokana na ukubwa wake.....Taa hizi huvutia sana na zinaleta ladha uzitumiapo......Hufanya chumba kua na mwangaza na hupendezesha chumba....


 Taa hizi ziko za aina tofauti, na kulingana na matumizi yako......
 Kama tunavyoona kwenye picha hizi, taa zinatofautiana kulingana na wewe upendavyo....unaweza kuweka taa moja ama mbili kulingana na upendavyo....taa hizi ziko za aina tofauti, na unaweza ukanunua kulingana na sehemu yako ilivyo, nikiwa nina maana ya rangi ya ukuta, fanicha etc.....

 Si lazima ukaweka taa nyingi, unaweza ukaweka taa moja kubwa, ama mbili ndogo, ama mbili kubwa. na pia unaangalia na ukubwa wa sehemu yako, na vitu ulivyoviweka.....taa hizi zina shades, na urembo tofauti kulingana na upendavyo( shades ni hizo kofia za juu ya taa, hua zinatoka na unaweza kuzibadilisha kwa urahisi)

Taa hizi unaweza ukaziweka pembeni ya makochi yako, ama pembeni ya tv stand, ama kama kuna kimeza nyumba ya makochi yako unawez kuweka pia......

Kwa hapa Tanzania, taa hizi ziko na zinapatika kwenye maduka ya taa, ama shopping malls, etc.......

No comments:

Post a Comment