Sunday, January 27, 2013

Rangi zanye giza......

 Kumekua na tatizo la wengi wetu kupenda rangi zenye giza...ama Dark colors, kwenye nyumba zetu, ama maofisini kwetu....Rangi hizi zinahitaji sana mwanga, nikisema mwanga ni kuanzia mwanga wa asili, na pia mwanga wa taa wakati wa usiku.......Rangi hizi hufanya chumba kua kidogo na chenye giza.....haijalishi umezitumia wapi...maana kokote unaweza kutumia ila zitumike kwa mpangilio kama unapenda rangi zaidi ya moja.

 Kama tunavyoziona picha zetu, rangi zilizotumika ni dark lakini ukiangalia, kwa uangalifu utakuta kua kuna mwanga katika vyumba hivi, na pia fanicha zake ni ang'aavu....Huwezi ukatumia kuanzia rangi, fanicha na urembo, sakafu etc...vyote vikawa ni rangi za giza.....Kwa kufanya hivyo, nyumba itakua ni giza, na haileti mvuto wowote ule.......


Na pia haimaanishi ni lazima uweke vitu vyeupe ndio viweze kufanya nyumba yako kua ang'aavu, kama utatumia rangi za ukuta zikiwa ni Dark, basi fanicha na mapambo yafanye yawe ni light colors....ambazo zitaenda na rangi ya ukuta, ama hata kama utafanya mix and match pia itapendeza.....

Kua na nyumba nzuri na yenye kupendeza, haimaanishi ni mpaka ujaze fanicha, etc, ndio nyumba ipendeze....
Ni kua na mpangilio mzuri, na nyumba itapendeza.......

No comments:

Post a Comment