Friday, January 18, 2013

Color combo......Nyumba hii iko kunduchi, na nilipenda mpangilio wake.....

 Sitting room ni nzuri, simple, etc.....Fanicha zote hizi za mbao zimetengenezwa hapa hapa Tanzania-Dar...
 Hapo juu ni sitting room, umeona hiki kiti kilivyo na design kama ya kusuka vile......Angalia pia rangi zake alizo tumia, hua nasema, ukijiamini kwenye rangi kila kitu kitakua sawa...na ukiwa umekwama mahali, basi tuwasiliana.....Mdau huyu rangi alizozitumia ni white, orange, green, blue, na brown ambayo ndio viti vyake...
Rangi hizi ukiangalia picha hizi kwa makini, utaona kua kuwenye hii cusion ya green ina colors zote, kasoro brown.....Siku zote kwenye upande wa ku design, angalia vitambaa vyako vya sofa, ama pazia je vina rangi nyingi? kama ndio, basi tumia rangi hizo kwa kuendeleza kupamba nyumba yako na hii itakusaidia, kuto kuchanganya rangi, ama kua na rangi zaidi zisizoendana...
 Open Kitchen.....Ukiangalia hii dinning table, huoni hata muungo mmoja wa kati ya mbao na mbao....utadhani furniture hizi zimeagizwa nje ya nchi vile....kumbe ni kazi ya mtanzania mwenzetu...


 Meza hii ya tv, ni ya mbao, na ni mkongo
 Wapendwa wadau, hii ni open kitchen.....ninachoweza kusema kwa kweli tokea nimeanza kazi hii ya Interior Design& Decorations....nyumba zenye open kitchen zinahesabika.....Open kitchen ni nzuri, ila kwa kusema ukweli zinahitaji usafi wa hali ya juu....maana ukiwa siting room unaona mpaka jikoni, na dinning iko hapo hapo.....nyumba hii ni safi mno....
 Stool za pembeni, kama unavyoona picha ya chini hapo, ameweka taa zile ndogo,
 Hapa kama panavyoonekana ni sitting room, mdau huyu yeye ametumia mbao aina ya mkongo....ni mpenzi wa mbao ameniambia, na mimi mwenyewe nilizipenda maana zina finnishing nzuri mno....
 Kitenga kikiwa hakina kitu.....
 Hapa ni toilet, na toilet yake ni ndogo, akaamua kuweka kitenga cha mbao kwa ajili ya kuhifadhi mataulo, products za usafi....etc....ni padogo, pasafi, na mpangilio mzima ni mzuri. maana mara kwa mara nasema kujaza vitu vingi sio upambaji......
Nilipoziona furniture hizi, nilifurahi mno, kwani ni kazi ya watanzania hapa hapa nyumbani....unajua imeshafika wakati sasa mafundi mbao hawaamini, kwa kuharibu kazi, na kuchelewesha kazi...na maneno mengiiii...

Vitu vyote hivi hapo juu vimetengenezwa hapa hapa, na mafundi wanaojua nini wanafanya, maana kazi ni safi, nzuri kama mnavyoionaa....furniture hizi zote ni mbao aina ya mkongo....

Kilichonifurahisha ni kua hii ni kazi ya mdau mwenzetu, ambaye yeye anatengeneza hizi furniture za mbao, design ziko nyingi mno......na hawana ujanja ujanja ............

Stress za furniture za mbao zote zitakua zimekwisha......kuanzia makabati ya jikoni, viti, meza za dinning etc...

Endelea kua nasi, na nitakuja kukueleza kua utampata wapi.....

9 comments:

  1. Kwa kweli kazi ni njema mno. Tafadhali tupatie mawasiliano ya jinsi ya kumpata mtu huyo.
    Kibe

    ReplyDelete
  2. Kazi nzuri sana,hiyo sofa set ni bei gani? Nimezipenda zaidi.

    ReplyDelete
  3. Nzuri sana "I like it"

    ReplyDelete
  4. tafadhali naomba number ya fundi aliyetengeneza hizo fanicha

    ReplyDelete
  5. tafadhali naomba number ya fundi aliyetengeneza hizo fanicha

    ReplyDelete
  6. aisee nyumba imependeza sana hongera kwa fundi na wenye nyumba kwa ubunifu

    ReplyDelete
  7. kwa kweli furniture ni nzuri sana hongera sana kwa mwenye nyumba

    ReplyDelete
  8. tuwekee namba ya huyo fundi tafadhali

    ReplyDelete
  9. tafadhali sana jamani tuwekee namba ya huyo fundi au tupe maelekezo ilipo workshop yake

    ReplyDelete