Friday, October 19, 2012

Msaada wa ujasiriamali....Ndugu wadau nakaribisha ushauri, mawazo tuweze kumsaidia mdau mwenzetu....Maana mimi sina uzoefu kwa upande wa biashara ya nguo.......

Mambo Sylvia, Hongera kwa kazi nzuri na elimu unayotupatia. Mimi nimekuwa napita kwa blog yako kila siku,
nahitaji ushauri wako wa kijasiriamali...
Nataka nifanye biashara ya nguo za watoto na kina dada tu toka nje ya nchi..
Natafuta mtu mkweli na mwaminifu wa kunipa maelekezo na misaada ya jinsi ya kufanya nikifika huko kwa watu hasa China / Hongkong,
na je natakiwa kuwa na mtaji wa sh. ngapi? Maana bado mgeni kwenye biashara. Please help me my dia dada.

1 comment:

  1. Jamani mnaofahamu haya mambo tujuzeni wenzenu, ahsante kwa mdau aliyefunguka bila uoga. KARIBUNI BASI JAMANI Eeeh!

    ReplyDelete