Tuesday, October 30, 2012

Je ungependa chumba chako kiwe na mandhali hoteli za kimataifa?Kuna msemo usemao kupanga ni kuchagua........Sasa je, ungependa chumba chako kiwe na mandhali ya hoteli ya kimataifa?

Unachotakiwa kufanya ni.
 kwanza, chumba chako kipigwe rangi vizuri, na kiwe kisafi juu mpaka chini. Rangi waweza piga kama ni nyeupe ama rangi zilizopoa...

Pili, kama chumba chako hakina tiles. basi weka carpet chumba kizima, na kama kina tiles basi weka carpet ndogo, 

Tatu, weka pazia nzuri pamoja na curtain poles, ama curtain box... na hakikisha pazia zako zimeacha inch 2 ama 3 toka ardhini......nikiwa na maana zisiburuze.

Nne, kitanda ulichonacho ama kama ungependa kubadilisa, hamna neno,  hakikisha tuu gororo lako ni zuri nani kubwa nikiwa na maana lina inch 8 upana...maana hii husaidia kua na muonekano mzuri ukitandika....na haijalishi ni kitanda cha mbao ama cha chuma, vyote hupendezaaa...bila kusahau kuweka picha juu ya kitanda upande unaolaza kichwa

Tano, Tukija kwenye mashuka, sasa hapa shuka zinazohitajika ni zile zenye duvet, nikisema duvet ninamaanisha ni ile mfano wa godoro lakini lenyewe ni laini sana, maana wanaweka fibre ndani.....hapa kwetu yako madukani, kama Home shopping center, Mr. price etc...

Sita, ukija kwenye utandikaji sasa, unatakiwa uwe na shuka la kutandika, shuka la kujifunikia, halafu duvet ambalo ndio limevalishwa cover ya shuka la mwisho.....

Saba, tunakuja kupande wa mito, mito waweza kuanzia mito 4,5,6 ni wewe tuu unapenda kua na mito mingapi kitandani kwako, na kumbuku hii inakua ni set nzima......

Nane, kuna kitambaa kinaitwa scarting, hiki ni kitambaa ndio kinaanza kabla ya godoro ili kuficha uvunguni.....na kinakaa katika vitanda design yoyote ile..

Tisa, throw ama bed runner, hua ni kitambaa cha urembo ambacho hutandikwa kwa upande wa miguuni kwa upana....

Kumi, unahitajika kua na stools za pembeni mwa kitanda, sasa hizi zinaweza kua ni 2 ama moja maana inategemea na ukubwa wa chumba chako....juu ya hizo stools unahitajika kuweka taa, taa hizi ni ndogo na ni za urembo pia na husaidia pia kwa wale wanapenda kusoma, ama ambao hawapendi mwanga mwingi.....

Mwisho, ndio unakuja kwa upande wa dressing table, na kabati la nguo........

Hakikisha usijaze vitu sana chumbani, na ndio maana wengi wetu tukienda kwenye hotels tuna relax, hii ni kwa sababu wenzetu wana kua na mpangilio mzuri sana, na wanazingatia usafi kila siku iendayo kwa mungu.....


4 comments:

 1. Nimependa maoni yako mi nina tiles lakini nataka kubadili style na kuweka carpet chumba kizima naomba ushauri kama itapendezea na hayo ma carpet akam ninayo yaona Hotels kubwa naweza yapata wapi hapa Dar, Asante sana Mungu akubariki

  ReplyDelete
 2. wewe ni kichwa,nakukubali sanaaa

  ReplyDelete
 3. Sikujua kama maswali hayajibiwi humu ndani, napita tu

  ReplyDelete
 4. thnx kwa ushauri na kazi yako vip hamna tawi mbeya?

  ReplyDelete