Friday, April 27, 2012

Tiles.........(Nilitembelea CTM Mwenge wana tiles nzuri, na nilipata maelezo ya kutosha na kuwaletea makala hii).....
Nikiandika maelezo kutoka kwao...
Ni baadhi ya mabafu ya kisasa waliyonayo...
Mabomba ya kisasa waliyonayo.....kwa kweli ni mazuri sana...Display ya mabafu waliyonayo..... hivyo unachagua upendayo....(jamani jamani, bafuni, na jikoni, sio sehemu yakuweka tiles zinazoteleza... maana wengine wanadondoka wanasema ni nguvu za giza, ama visingizio kibao, kumbe ni tiles ulizoweka zinateleza....sasa ukienda kwa mawakala watakushauri, na utanunua vitu quality)
Display za tiles zimepangwa kwa square metre kabisaa... na wana designs nyingi. nimewapenda sana kwa kutoa ushauri, na bidhaa zao ni quality.....
Katikati ya wiki hii, nilipita CTM pale mwenge kituo cha ITV, hii ni kampuni ya tiles, sanitary ware, (masink, mabafu ya vyooni etc)& brass ware (mabomba).

Niliongea na mwakilishi wa kampuni hiyo, kwa kutaka kujua matumizi ya tiles, na wapi tunaweka, kwa sababu nimeona kuna matatizo ya uchaguzi wa tiles.....

Types of Tiles;
Tiles za ukutani (Wall Tile)
Tiles za sakafuni (Floor Tile)

Designs of tiles:
Ceramic - hizi zina urembo
Porcelain - hizi ni za kung'aa, sasa hapa kuna zinazoteleza na hazitelezi.
Corto ama outdoor - hizi ni za nje, hata ndani waweza weka ila jikoni.
Kilimanjaro tile- zinatengenezwa south africa, kuna za ndani na za nje na hazitelezi.

Sasa kabla ya kwenda kununua tiles haya yafuatayo ni lazima uyajue.

Ujue unataka kuweka wapi,
matumizi ya hicho chumba,
na vipimo hua vinahitajika kwa square metre.

kampuni hii malighafi zao zinatoka:
South Africa
Brazil
Spain
China.

Umuhimu wa kununua tiles kwa mawakala ni kwamba, huwezi kupata vitu feki, wa ujanja ujanja.... na vinakua na guarantee....

Kwa mawasiliano zaidi, wanapatikana hapo mwenge kituo cha ITV, wako barabarani kabisa.....Karibuni

NB:
nitakua nikiwaletea makampuni yayouza vitu orignal, na ni mawakala na vyenye guarantee.... sasa na pia kama unataka kujua kitu chochote kile, niambie na nitawafuatilia na kuwaletea humu...
UMEFIKA MUDA SASA TUACHANE NA VITU FEKI... FEKI NI GHARAMA....(nyumba yako na unakaa mwenyewe, ila bado unachakachua... lol......haipendezi......tuachane na hiyo dhana sasa....)

Nawatakia weekend njema.......


4 comments:

 1. waow!! nimependa blog yako, nilikuwa natafuta tiles original ila kila nikienda madukani, nashindwa. naomba uwe unaweka prices za bidhaa pia ili mtu awe anajipanga.

  ReplyDelete
 2. mi nipo mbeya,nikitaka hzo bidhaa napatajje?

  ReplyDelete
 3. mi nipo moro natafuta sana mabafu ya kisasa na vitu vingine, ninachohitaji na ni muhimu pia kwenu ni kutoa pia mawasiliano kwa maana ya namba za simu itakuwa vizuri

  ReplyDelete
 4. nawashauri muweke namba za simu

  ReplyDelete