Tuesday, April 17, 2012

Interview na Radio Capital, 101.4 fm Mada ilikua Kuepuka Makorokoro, ama vitu vingi visivyohitajika majumbani mwetu.....

Ninapenda kuchukua fursa hii ya kuwashukuru sana Capital Radio, kwa kuweza kunipa nafasi mara kwa mara, kufanya nao majihojiano ya kuelimisha jamii kwa kupitia radio yao, na kuweza kuwafikia wale wote wasio pata muda, ama kutoweza kuangalia blog yetu hii.....

Kipindi kilikua kama ifuatavyo:

Nilifanyiwa interview na Ms. Sara Kipingu, na kipindi hua kinaanzaa saa 9:00am weekdays mpaka saa 1:00pm na mimi hua ninafanya nao kipindi kuanzia mida yaa saa 11:15am ama 11:30am, na ni muda waa nusu saa...


Mada kama nilivyoitambulisha hapo juu, Kuepuka kua na vitu vingi visivyofaa majumbani (makorokoro kwa lugha ya haraka haraka)

Makorokoro ni nini?

Hivi ni vitu vyote ambavyo vimeisha, vimevunjika, havitumiki, etc.....

Sababu zinazofanya uwe na makorokoro:

  • Hobi ya kununua vitu kila mara bila kujali check list
  • Stress, baadhi ya watu wanapokua na stress hufanya shopping wakihisi watapata faraja, na kupunguza stress, kumbe anajaza vitu ndani, napia anatumia hela nyingi bila budget.
  • Kuna watu hawapitwi, hawa ni wale ambao wakiona kitu wanashindwa kujizuia kila anachokiona anakitaka. n.k

Matokeo yake:

  • Nyumba inakua ndogo, maana space ndio imechukuliwa na hayo mavitu.
  • Inakaribisha kutokwenda na wakati, unakua ni mtu wa mood mbaya muda mwingi, na vile vile inakaribisha wadudu, na uvundo kwenye nyumba. wadudu hao ni kama mende, panya etc

Hizi ni baadhi ya hatua unazotakiwa kuchukua kuepuka tatizo hili:


  • Fanya filling magazeti, makaratasi, bill zote na aina yote ya makaratasi ambayo unayahitaji. usivyohitaji tafadhali tupa, tena kwa usafi.
  • Kabla ya kufanya shopping kua na checklist, tafuta muda na andika vitu vyote unavyovihitaji, na kagua nyumba yako ndio utakavyojua nini unakuhitaji, hii ni kwa sehemu zote,
  • Hili ni tatizo kwetu sie, asilimia kubwa ya wanawake, yaani utakuta mtu ana nguo nyingi, kuna zinazombana, zilizochakaa, alizozichoka, na hazigawi, zote anazo, na bado anaendelea kununua nguo...... tafadhali kama kuna ambazo huihitaji, gawa, unaweza kupeleka makanisani, misikitini, na nyumba za wasiojiweza.. (mi hua ninawaita ni selfish hawa watu).
  • Vilivyovunjika vitu jamani tupa...... unachupa zilizoisha vitu tupa...... mfano mdogo angalia hiyo dressing table yako jamani........haina chupa empty, na mabox.....jibu unalo
  • Hifadhi cd na dvd, zako vizuri, kama kwenye kabati, ama cases zake specially. etc, na kama kuna ambazo huihitaji ama umezichoka gawa... nasisitiza gawa.....
  • Design kabati chest droo yako na hii ndio iwe ni muongozo wako wakua ukiweka vitu unavyohitaji, na ikijaa, basi kabla ya kununua vitu, fanya check list, na utoe ambavyo hutumii....inamaana kua hii droo haitajaa kamwe.....
  • Wageni wako wanapokuja kwako, wanalala ama wamekaa masaa, sasa wameondoka wamesahau vitu vyao, unavifanya nini? Ni rahisi, wajulishe kua wamesahau na wape muda wa kuja kuchukua, ama wapelekee, ikishindikana gawa..........
  • Namalizia kwa upande wa stoo... hii sio sehemu ya kuhifadhi hayo makorokoro, utakuta mtu kahamia kwenye nyumba ya kupanga, halafu anahifadhi mabox eti kwamba akihama atatumia tena, jamani jamani, hebu acheni.......ukihama miaka 3 je, haujaleta panya ndani.......unaweza ukawa na vitu vya thamani , na bado ukiwa umevijaza tuuuuu hayo ni makorokoro...

Kwa kufuata hayo niliyoyasema, nyumba yako itakua ni safi, muda woteeeeeee, na itatupa urahisi kwa ku decorate nyumba yako, kama uta decorate mwenyewe, ama utatafuta mtaalamu, maana akikuta nyumba iko safi, hata gharama itakua ni nafuu.......


Nashukuru, tuwasiliane kwa maelezo zaidi

Sylvia

Director.....

No comments:

Post a Comment