Sunday, April 29, 2012

Surprise..........

Habari za weekend, yangu ilikua poa, ila na hii mvua......iliniishia nikiwa site za wateja... si mnajua kazi tena hua sina weekend mara nyingi ninakua site...


Nina surprise kwa ajili yenu, unapenda kuijua ni nini?


Endelea kupitia blog hii yetu ndani ya wiki hii ya mwanzo wa mwezi huu wa tano......


Love u all..... Nawatakia wiki njema na mei mosi njema....


Sy

Friday, April 27, 2012

SOLD


Mnaikumbuka hii set, ina 3 sitter 1, 2 sitter 1 na single sitter 1....
Shelf pekee ndio inauzwa...waweza weka vitabu, urembo etc...
Meza ya viti 6


Sofa wanakaa watu 6. 3 sitter, 2 sitter, na 1 sitter.

viko katika hali nzuri... na vina umri mdogo sana... tuwasiliane kwa atakae hitaji.... 0713 - 920565...Karibuni

NB:
Nimeanzisha kipengele hiki, kwa atakae hitaji kuuza furniture zake, tuwasiliane na nitaviweka kwenye blog kwa mauzo.....ila viwe na hali nzuri, na nitakuja kuvikagua kwanza kabla sijaviweka humu...kwa watu wa mikoani naomba mvipige picha kila kona ili niweze kukagua......

Tiles.........(Nilitembelea CTM Mwenge wana tiles nzuri, na nilipata maelezo ya kutosha na kuwaletea makala hii).....




Nikiandika maelezo kutoka kwao...
Ni baadhi ya mabafu ya kisasa waliyonayo...
Mabomba ya kisasa waliyonayo.....kwa kweli ni mazuri sana...



Display ya mabafu waliyonayo..... hivyo unachagua upendayo....(jamani jamani, bafuni, na jikoni, sio sehemu yakuweka tiles zinazoteleza... maana wengine wanadondoka wanasema ni nguvu za giza, ama visingizio kibao, kumbe ni tiles ulizoweka zinateleza....sasa ukienda kwa mawakala watakushauri, na utanunua vitu quality)




Display za tiles zimepangwa kwa square metre kabisaa... na wana designs nyingi. nimewapenda sana kwa kutoa ushauri, na bidhaa zao ni quality.....
Katikati ya wiki hii, nilipita CTM pale mwenge kituo cha ITV, hii ni kampuni ya tiles, sanitary ware, (masink, mabafu ya vyooni etc)& brass ware (mabomba).

Niliongea na mwakilishi wa kampuni hiyo, kwa kutaka kujua matumizi ya tiles, na wapi tunaweka, kwa sababu nimeona kuna matatizo ya uchaguzi wa tiles.....

Types of Tiles;
Tiles za ukutani (Wall Tile)
Tiles za sakafuni (Floor Tile)

Designs of tiles:
Ceramic - hizi zina urembo
Porcelain - hizi ni za kung'aa, sasa hapa kuna zinazoteleza na hazitelezi.
Corto ama outdoor - hizi ni za nje, hata ndani waweza weka ila jikoni.
Kilimanjaro tile- zinatengenezwa south africa, kuna za ndani na za nje na hazitelezi.

Sasa kabla ya kwenda kununua tiles haya yafuatayo ni lazima uyajue.

Ujue unataka kuweka wapi,
matumizi ya hicho chumba,
na vipimo hua vinahitajika kwa square metre.

kampuni hii malighafi zao zinatoka:
South Africa
Brazil
Spain
China.

Umuhimu wa kununua tiles kwa mawakala ni kwamba, huwezi kupata vitu feki, wa ujanja ujanja.... na vinakua na guarantee....

Kwa mawasiliano zaidi, wanapatikana hapo mwenge kituo cha ITV, wako barabarani kabisa.....Karibuni

NB:
nitakua nikiwaletea makampuni yayouza vitu orignal, na ni mawakala na vyenye guarantee.... sasa na pia kama unataka kujua kitu chochote kile, niambie na nitawafuatilia na kuwaletea humu...
UMEFIKA MUDA SASA TUACHANE NA VITU FEKI... FEKI NI GHARAMA....(nyumba yako na unakaa mwenyewe, ila bado unachakachua... lol......haipendezi......tuachane na hiyo dhana sasa....)

Nawatakia weekend njema.......


Wednesday, April 25, 2012

Curtain Designs.....Homez Deco Tutakushonea na kukufungia utakapo...Karibuni....





Hizi ni baadhi ya pazia ambazo tunashona hapa kwetu homez deco, karibu uchague designs, utakazo, ziko nyingi na nzuri sana.........Karibuni....

Vitanda vinapatikana Homez Deco, kwa kutoa order...na kitakua tayari ndani ya siku 7.... Vitanda vyote ni 5 by 6....

Hiki ni 450,000/-
hiki ni 400,000/-
hiki ni 400,000/-
hiki ni 400,000/-
Hiki ni 430,000/-
Hiki ni 390,000/-
Hiki kitanda bei ni shs, 360,000/=

Bei hizi ni bila usafiri.......utalipia usafiri tukikuletea kukufungia. chaga za vitanda hivi ni za mbao...rangi ya vitanda hivi ni nyeusi.....karibuni sana.

Tuesday, April 24, 2012

Before & After House make over...(Tabata site)

Kazi imekwisha........Karibuni sana kwa mahitaji ya pazia, kubadilisha covers makochi, viti vya dinning, interior decorations, furniture arrangment, ushauri, kupaka rangi kuta, fanicha za chuma, Landscaping & gardening, interior design etc.......
Ukifanya kazi yako kwa umakini, na upendo, kila kitu kitakwenda sawa.......Naipenda kazi yangu.......


Wallpaper, huu ukuta uliokaa tv, tunaita ni focal point, ya sitting room yetu, nitaja elezea nini maana ya focal point siku ingine...tuliweka wallpaper rangi ya offwhite, na ni wash able, ikichafuka unaifuta na maji kidogo...



Hapa tukivalisha cusion covers tulizozishona Homez Deco....





Hizi ni pazia za vyumbani, kama tunavyoonekana mzigoni, hakuna cha boss wala mfanyakazi, we work as a team work......
Maua haya niliyapenda sana.... ninamtafuta huyu anaefanya shughuli hii then nitawapa contacts zake kwa watakao muhitaji..... ni maua ya artficial...(yanafanana na ya kariakoo haya...)
Kiti cha kulia ndio kilichobadilishwa na fixer wetu....


Fixer akibadilisha cover za viti vya dinning.....



Tukianza kazi ya ku fix pazia za sitting room......


Sitting room & dinning before make over.....

NB:
Naomba radhi, kwani kuna baadhi ya picha zimetoka giza... ninafanya utaratibu wa kupata profession camera muda si mrefu.... tuombe mungu....