Tuesday, March 20, 2012

mazingira yakitunzwa na kuhifadhiwa yanapendeza popote pale,

Tuyapende mazingira tunayoishi na kuwayeka ktk hali ya usafi hili ni jukumu la kila mwanajamii, siyo
 jukumu la serikali wala serikali za mitaa pekee, kwani milipuko ya magonjwa ambayo inatokana na uchafu malundo ya taka mitaani, huwaga milipuko ya magonjwa ikilipuki ktk majengo au ofisi za serikali ni kwa nyinyi wanajamii,wenzengu mnaopata maafa, kila mmoja wetu anajukumu la kulinda mazingira yanayomzunguka
iwe majumbani sehemu za biashara , kwenye migahawa, na maofsini usafi upewe kipaumbele ktk jamii yetu
wanajamii yetu,

Nawa mikono mara kwa mara, ukikohoa ziba mdomo wako na handchief au lesso cover up yr cough, maana wengine akihoa inakuwa nikero kuna magonjwa ambayo ukikohoa huna yanaambukiza na wengine TB kifuu kikuu,enfluenza,na tujifunze ustaarabu na maadili ambayo siku zote yatasadia jamii yetu.

Kuna hii tabia ya baadhi ya wanaume kukojoa hovyo kando ya barabarani kwenye ukuta ni tabia mbaya sana ambayo inatakiwa ikemewe iweje wanyama kama paka ajisitiri ambayo hanakili kama za mwanadamu nyinyi baadhi ya  wanaume wenye akili timamu mshindwe kujisitiri,(IJULIKANE NI BAADHI YA WANAUME WENYE TABIA YA KUKOJOA HOVYO BARABARANI SIO WOTE)  najuwa kuna ambao watasema nimetoka nje ya topic no haya yote ni mazingira hatakupiga makelele bila sababu za msingi haitakiwi, miziki ya sauti za juu kwenye mabar , kwenye vyombo vya usafiri ni maudhi siyo sifa,

Kuna baadhi ya maeno ya jiji hasa magomeni ni kero jamani siku za week end ni kero kumbi zinapiga miziki mpaka asubuhi ni maudhi maudhi ili suala lishuhulikiwe, kikamilifu, mitaani kukiwa na shuhuli ndio kabisaa, kelele unaweza ukawa na shughuli mtaani mkafurahia mpka mkajirusha mpka saa fulani mkafunga miziki au makendelea ila kwa sauti ya chini, ila walio wengi wenu ukiishakuwa na shughuli basi, mpka mtaa wa kumi wajua, mjifunze kujali, na kuthamini majirani, zenu hayo yote ni mazingira punguzeni miziki, mabaar restaurants kwenye public transports ni kero kero siyo sifa, starehe zenu isiwe shida kwa wengine, nadhani mumenielewa mpka hapo tusitaarabike maana ustaraabu haununuliwi dukani,
muungwana ni vitendo siko zote. na si maneno tuu hayo yote ni mazingira,asanteni

From Jossyanne - USA

3 comments:

  1. Edit your work before posting, ni handkerchief na sio handchief!!! Tushukuru technology cause computer zetu zina spell check, USE IT!

    ReplyDelete
  2. asante kwa kunielimisha, ila ninachokuomba ni kwamba, ninaandika articals nyingi, so kukosea ni lazima, ingawa ninajitahidi sana kurekebisha, sasa usidhani ni rahisi kama ufikiriavyo, nia na madhumuni ni ujumbe ufike kwa hadhira/jamii, na sio kuchunguza spellings. jitahidi kuuliza maswali msingi ili uelimike....

    ReplyDelete
  3. jamani umesahau kutema mate ovyo!!!!!!

    ReplyDelete