Monday, March 19, 2012

Jikoni, Bafuni Chumba cha kusomea na Chumba cha kuchezea watoto...

Jikoni...
Chumba hiki kinahitaji kua na mwanga wa kutosha kulingana na ukubwa wa jiko. Unaweza kuweka taa zaidi ya moja kwani husaidia jiko kua safi, usalama etc. Naomba ijulikane kua chumba hiki kina vitu vya hatari kama jiko, fridge etc.. sasa basi ukiweka taa za kwenye dari, za ukutani zitakusaidia sana kutoa mwanga unaohitajika na uta akisi rangi ya ukutani na vyombo vyako ambapo utapata muonekano mzuri.

Chumba cha kusomea/home office:
Chumba hiki mwanga ni muhimu, kumbuka ni sehemu ya kusomea na kuandika etc. Sasa mwanga hafifu utaweza kuharibu macho yako. Kama chumba chako hiki ni kikubwa na deski imewekwa katikati ya chumba, basi socket ya umeme inahitajika kuwekwa level ya sakaru, kwa juu kidogo ili kusaidia kutokua na nyaya nyingi na zinakua na mpangilio.

Mwangaza katikati ya desk husaidia kufanya chumba kidogo kuonekana kikubwa.

Bafuni..
Hapa kunahitaji mwanga zaidi ambao utakuwezesha kuona vizuri, lakini pia mwangaza huo unahitaji kua sawa yaani ukitaka unaweza  kupunguza ama kuongeza, maana siku hizi tunajenga mabafu mazuri ya kisasa, ambayo unaweza kupumzika pia. Hii ni kwa  mara chache inatokana na kuhusishwa na mwanga ama sakafu ambazo zimewekwa kwa usadi na kwa mpangilio mzuri na huonyesha umaridadi wake.

Chumba cha kuchezea watoto:
Chumba hiki kinahitaji usalama zaidi, taa ziwe ni za juu ama ukutani, kusiwe na mrundikano wa vitu, weka taa ambazo mwanga wake unaweza kuupunguza, kuto kuweka vitu sakafuni ambavyo ni hatarishi. bila kusahau mapazia, pia yanatakiwa kua yanafungwa vizuri, kuzuia watoto kuchezea maana yanaweza kudondokea watoto.

Mwisho wa Topic ya taa....

No comments:

Post a Comment