Wednesday, May 23, 2012

Mbezi Beach Project.....Iron furniture by Homez Deco.....

Asikuambie mtu fanicha za chuma zinapendeza sana... na hautogombana na dada wa kazi kua hafanyi usafi chini ya makochi......kote kunaonekana.....

Dinning table.......ya viti 5.....
Mto ukiwa na cusion cover na tayari kwenda kwa mteja...
Mto ukiwa na linning....
Kiti kikianza kuonyesha muelekeo....


Ninashukuru mungu kua sasa nimeweza kuwapatia vijana ajira hapa mtaani kwetu kwenye ofisi yangu........

Hapa nikikagua kazi, mito kama ujazo uko sawa na inakaaje kwenye kiti....kazi hazitoki mpaka nimezikagua.....


Hii ndio kazi ya yale magodoro madogo madogo ambayo tuliyakata kata vipande vidogo vidogo, tukavichanganya na fiber, na tukashona decron tunazitumbukiza ndani mchanganyiko huo, na tunashonea lining, mwisho tunashonea foronya ama cover, na mto unakua tayari.

Kama kawaida yetu Homez Deco, hatufichi kitu, mito yetu ni imara na haina harufu hata ukimwagia maji, utauanika na utakauka na hakuna harufu itakayotoka ama kutoa alama kwenye mto....maana tunaweka vitu visafi tuuu..... mito ni soft na inadumu kwa muda mrefu bila kusinyaa.....

Hii ndio ile nyumba ambayo nilitengeneza curtain poles za chuma, vitanda vya chuma, vya four posters, nikawaonyesha, na last week tukamaliza na meza ya chakula na makochi..... wishing you all the best my dear customers.......

Asante sana mteja wangu na zawadi yako ya magazine rack iko jikoni......nitawaonyesha......


5 comments:

  1. kazi nzuri sana.sasa na sie wa uswazi wenye kipato kidogo tusaidie basi tupambeje kwenye nyumba au vyumba vyetu.

    ReplyDelete
  2. waw makochi ya chuma ndo bei gani mama?

    ReplyDelete
  3. I LIKE IT MAMII MUNGU AKUBARIKI SANA JAMNI VPI NIKITAKA VITI VIDOGO KAMA HIVYO VIWILI NA KUBWA LA KUKAA WATU WAWILI SHILINGI NGAPI UNAFANYA.SAMAHANI KWAUSUMBUFU NAOMBA UNIJIBU NITASHUKURU SANA KAMA HUTONIPOTEZEA MIMI PENDA KAZI YAKO.

    ReplyDelete
  4. HEllow dear..

    Am so proud of you mama Jaydan, unafanya kazi nzuri, safi na ya uhakika. Mungu azidi kukubariki uendelee kutuletea mambo mazuri.

    Nilitaka kujua hizo rell za chuma za mapazia unauza kiasi gani? I mean ile ndogo na hiyo kubwa (Huwa zinakaa mbili kwa kila dirisha moja ya lining ya pazia na nyingine ya pazia lenyewe).

    Siku njema kisses to bby boy.

    ReplyDelete
  5. Ma dia hongera saaaanaa kazi zako nzuri na sinasisimua. Mwenyezi Mungu azidi kukupigania nakukuongoza. BIG UP MAMIE

    ReplyDelete