Tuesday, May 1, 2012

Nimewagusaaa eheheee!!!!






Inafika pahala sasa tuambizane ukweli....., watanzania asilimia kubwa hatuna hela si ndio ehee, ila hao hao utawakuta wanavaa vizuri, tena vitu vya designers, kama ndio nguo, cheni, viatu (CL) ndio vimeingia maana navisikia tuuu, lace wig kuchangia sherehe kwa kiasi kikubwaa cha fedha etc.

Wanakokaa hapafai na ni aibu jamani, yaani unamkuta mtu nje mrembo kavalia huyoooo, gari zuri ila nenda home kwake, jamani, unaweza ukakataa lol...

Hivi kweli uki save hela yako hiyo ukasema sasa mwezi huu ama miezi miwili sinunui nguo wala viatu etc, natengeneza nyumba yangu, kama ni yakupanga ama ya kwako, utashindwaaaa kweli, ama ndio kupanga kuchagua....

Hebu tujirekebishe sasa, na tuanze kupenda nyumba zetu, maana maisha yetu yanategemea sana nyumba zetu, na ukiipendezesha nyumba yako, basi na hata safari usizozipangilia na mafoleni haya kumaliza mafuta ya gari, na uchovu hata kama unapanda basi, zitapungua na utakua unarudi home kwako moja kwa moja kwa amani, na utapumzika kwa amani.....


Ni hayo tuuu kwa leo.........TUBADILIKE, NA HILI LINAANZA NA WEWE, SIE WENGINE NI WATAZAMAJI TUUUUU UKIJIBANA KWA MUDA UNAWEZA KUPAMBA NYUMBA YAKO NA IKAWA NZURI TENA ZAIDI YA HIZI............



4 comments:

  1. Syl you are forgetting one thing, KILA MTU ANA PRIORITIES zake, so kuna wengine their priority is looking good then the rest will follow. Na suala la kutokuwa na pesa ongelea personal experience yako cause TZ kama huna pesa does not mean wote hawana pesa. And mind you, bado waTZ hatuna utamaduni wa kudecorate our houses. So introduce hili suala pole pole sio kwa kama kuzodoa watu! Just thinking.....

    ReplyDelete
  2. naungana na wewe Nanah...not about what you say but how you say it...unatuzodoa wewe kama nani?? Una habari kama sisi ni wateja watarajiwa. Tembelea blog nyingine za kibiashara utambue lugha inayotumika....

    ReplyDelete
  3. ulicho ongea ni cha kweli na kuna baadhi ya watu huwa hawapendi kuambiwa ukweli hilo ndio tatizo,nyumba ndio kila kitu sio kushindana kubadilisha magari ya kifahari ila likija suala la kupeleka mgeni nyumbani kwako unakwepa,tuamke sasa wapo walio na pesa na wapo walio na pesa za kudunduliza kama zangu ila penye nia pana njia,mwanamke nyumba bwana,thnx kwa somo zuri,keep it up.

    ReplyDelete
  4. Hao watakuwa ni wale wale ndio maana kinawauma..kawazodoa kasema kweli?!au ndio ukweli unauma.na ukiangalia wanawake wengi hp mjini kuvaa sana,gari la fahari,cm 3..nenda kwake utachoka!2badilike jamaniwanawake..sio lzm uweke v2 vya ghali lkn vp v2 cheap na nyumba inapendeza pia.ht MR haoni tabu kurudi home mapema.c panavutia..hamuoni tabu kuwakaribisha rafiki zenu w.ends ,ckukuu..ht wao wakiona wanapata wivu,wivu wa maendeleo..TUBADILIKENI WANAWAKE

    ReplyDelete