Friday, May 18, 2012

mmmmhhhhhhhhh!!!!!!!! Asante....na Mungu akuongezee pale ulipopungukiwa....[Homez Deco - Kreative Homez] New comment on Maandalizi ya Website yakiendelea.......
Hide Details
FROM:
Anonymous

TO:
sylvianamoyo@yahoo.com
Message flagged
Wednesday, May 16, 2012 4:00 PM
Anonymous has left a new comment on your post "Maandalizi ya Website yakiendelea......":

wewe acha kisema ivyo idea ipi watu tunayo hio idea siku nyingi nikwambie ndugu yangu njoo taratubu au idea gani tucukuwe mbona kuna watu wanafanya kazi kama yako na ni kubwa na ww pia unapata idea kutoka kwao,ebu niambie mbona unatupa idea ya kusafisha nyumaba na kuweka vizuri tunachukuwa,usiwe mchoyo utaboa na watu hatutakuunga mkono,mwamgalie joseline upo wapi na sio mchoyo semuse wewe mtoto wa kichochoroni ndo mana umelea mimba mwenyewe

Moderate comments for this blog.

Posted by Anonymous to Homez Deco - Kreative Homez at May 16, 2012 4:00 PMHii ni comment ambayo nimetumiwa.

Any way nadhani ile mada watu wameielewa vibaya na wameichukulia visivyo, ukiisoma vizuri, kwa kutulia utaielewa, na kuliko kupoteza mudawako na kuandika haya uliyoyaandika, matusi, kashfa etc.....

Hii ni moja ya comments zambazo kidogo haijavunja maadili ya kitanzania, kwa upande mwingine ni matusi.....

Blog/Website hii ni ya watu wastaarabu, na wanaopenda kujifunza, etc... sio blog/web ya matusi, malumbano kama baadhi ya hawa watu wanavyochukulia,

Mimi kulea mimba mwenyewe, kulea mtoto mwenyewe haikuhusu, na hayo ndio maisha niliyoyapanga, na ninayafurahia mnoooo......na sijui huyu malaika wa mungu, mtoto wangu amekuingiaje mpaka ukamuhusisha huku,

Kazi yangu hii nimejitolea kuelimisha na tunaelimishana, mimi sio malaika kwamba kila kitu najua, tunasaidiana na kuchangia wote kwa pamoja.......ni wangapi wanaofanya kazi kama yangu, wanachukua muda wao na kuelimisha, kutoa ushauri bila malipo???????

Ninachotaka na ninachopenda ni kwamba hata kama mtu una aidia yako na umeitoa kwa uma..... kuna watu wanataka wasikie kitu ndio wakianzishe, sio waumize vichwa, na akili zao waanzishe etc. basi hata kama kuiga... EDIT basi........

Hawa watu wapo, na nitaendelea na msimamo wangu huo huo.......

Unapenda kitu umekiona humu, chukua, peleka kwa fundi aliye karibu na wewe etc.... Sijamaanisha kua wote wanaochukua vitu humu basi ndio niliowasema.... hapana, hapana, hapana......

Naomba kuwataarifu kua, comments zote, ni lazima zipitie kwenye email yangu, nazisoma, halafu ndio ninaziruhusu, sasa wewe unaetuma matusi, maneno ya kashfa etc. hapa sio mahala pake, na kamwe lengo la blog/website halitobadilishwa na wanaotukana matusi ama kunijaribu kwa njia ingine ile yoyote. Unajipotezea muda, na nguvu bila sababu...... Ila pia nakuombea mungu akunusuru kwa yote maana hujui ulitendalo.......

Kinachoniuma ni mimba yangu ambapo sasa nina mtoto, amekukosea nini.........?????????????????

Challenge za biashara ninazipenda, na ndizo zilizonifikisha hapa, maana ninazifanyia kazi.......

Ninawashukuru wadau wote kokote mliko kwa support yenu, na tunaendelea na kazi kama kawadia, unahitaji ushauri, ufanyiwe kazi, na ninapokea ushauri pia kutoka kwenu, na kubadilishana mawazo....etc... karibuni sana sana sana.........

Mungu awabariki kokote mliko........5 comments:

 1. Wasamehe mpendwa wangu kwani wengine ni malimbukeni na wala hawajui walitendalo wao wanawaza kuwavunja moyo wenzao na kuwakashfu bila sababu yoyote ya maana na ukiwaangalia vizuri wao wenyewe si lolote si chochote wapo wapo tu mtaani kazi kudiscus maisha ya wenzao wakati yao yanawashinda,usijali mpendwa wangu tuko pamoja kaza buti mwanao apate maisha bora kwani hizo ni kelele za chura ambazo wala hazimzuii tembo kunywa maji

  ReplyDelete
 2. Nakushauri tu mdogo wangu when people comments take what will be usefull to you and ignore the rest. hukutakiwa kurespond to any foolish comments bse the world is watching over just ignore those abusive words. I like your blog

  ReplyDelete
 3. Pole sana my dear sis, achana na hao magubegube wanataka wakupe strain mambo yako yaende hovyo fanya vile Mungu anakuongoza kufanya kama mtoto ni wako hakuna aliyekusaidia kubeba mimba wala kuingia labour.

  ReplyDelete
 4. pole sylvia......haya yote ni sehemu ya maisha, yatapita tu

  ReplyDelete
 5. Yaani Sylivia usihangaike siku nyingine kujibu upuuzi kama huo. kila mtu na maisha yake na anavyochagua kuishi. cha msingi uwe happy tuu. huyo anakuonea donge. Kwanza ni mshamba maana hicho kiswahili chenyewe alichoandika waala hakieleweki. Kaza buti mama utafika mbali.All the best!

  ReplyDelete