Thursday, May 31, 2012

Usafi wa sofa.....(ya vitambaa...)
Nilitumiwa email na mdau mwenzetu, kua alikua anaomba kujua ni jinsi gani anaweza safisha sofa zake, na ni za vitambaa....
Nashukuru sana sana kwa kuuliza swali lako hapa kwetu, nami napenda kulijibu kama ifuatavyo....
Huku kwetu kwa asilimia kubwa hua hatuna utaratibu wa kusafisha makochi yetu, na hii ni kutokana na wengi wetu kuto kujua ni products gani atumie na zinapatikana wapi, sasa inaishia tuu kwenye kufuta futa tuuu, ama tunasubiria mpaka sofa iwe chafu sanaaa ndio tusafishe.... jua kua hapo unakua unaliharibu sofa lako na unalichakaza wewe mwenyewe, maana siku ya kuja kulisafisha ni lazima utalisugua na matokeo yake pale ulipo sugua rangi haitafanana na sehemu ingine,...
Natumai wengi wetu tunajua ama kusikia haya makampuni ya networking, kwa kweli kwa sasa yanakuja kwa kasi na ni mazuri maana yana products nyingi nzuri na ambazo hazijachakachuliwa....ama kua diluted...
Moja ya hii kampuni ni GNLD INTERNATIONAL, Hii kampuni nimeshafanya nao kazi, kwa miaka 3 na nusu, hii ni kua ninawafahamu, na kufahamu products zao.... si mnajua siwaletei vitu bila kujua ama kufanya research kwanza.....
Sasa basi, hii kampuni wana product yao moja kwa upande wa home care.... inaitwa SUPER 10, ni nzuri mno, na kwa wale wanaotaka kubana matumizi, basi products zao hawa ni nzuri maana una dilute mwenyewe kulingana na matumizi na mahitaji yako...
Super 10 kama mnavyoiona hapo juu,,, inahitajika kutumika na spray bottle yake, hii ina vipimo kabisa inakuonyesha.....
Kwa wale wenye sofa za vitambaa, kwanza kabisa, inabidi uipanguse vumbi, ama kama un hoover basi puliza, hakikisha hakuna vumbi kila mahali,
Unatakiwa kua na kitambaa kisafi kama kitaulo kisicho toa mavumbi, ama manyoa, maana itazidi kuchafua.
Hiyo Super 10 unaichanganya na maji katika ujazo wa 1:20 (vipimo viko kwenye spray bottle), halafu unaitikisa, unafanya hivi ili utakapokuja ku spray kwenye sofa isitoke maji, inatakiwa itoke povu,
Ukisha spray, unachukua kitambaa chako na unaanza kusafisha kwa design ya mduara, na usipulize sehemu kubwa, unakwenda kidogo kidogo.... mpaka unamaliza.
Baada ya hapo acha sofa lako likauke na utakua umeshafisha sofa lako, bila gharama kubwa....
Haihiitaji kua na hela nyingi kusafisha sofa yako kwa kutumia Super 10....
Upatikanaji wa Super 10, ni mpaka uwe member wao, na hapo kunakua na punguzo la bei, ila sio lazima kujiunga, unaweza kununua kwa mtu ambaye tayari ni member wao.

Naomba kwa watakaohitaji, mpigie huyu kaka anaitwa Tija, na kwa walio Dar anaweza kuja hata akakuonyesha jinsi ya kusafisha hapo hapo nyumbani kwako ama hata ofisini...

TIJA
0713 - 336977, - 0754 - 006977

Ni hayo tu kwa leo...... siku njema...

4 comments:

 1. Nimefarijika na ninashukuru sana Dada Sylvia kwa kunijibu (mimi ndio nilikuomba utuelekeze jinsi ya kusafisha sofa). Natumai na wengine watanufaika pia. Mungu azidi kukubariki sana katika kila ufanyalo.

  ReplyDelete
 2. sorry jamani mie sijaelewa kua huo ujazo wa 1:20 ni hiyo super 10 au ni ujazo wa maji ndio yafike mpk 1:20? tafadhali naomba kuelewesha juu ya uchanganyaji naogopa nisije jaza maji mengi au super 10 nyingi plz

  ReplyDelete
 3. Thanks much for the advice. Nimefarijika. Godbless u my gal!

  ReplyDelete
 4. thaks for your advice sweet pay,pia mimi ningependa kujua jinsi ya kusafisha madirisha (viyoo)

  ReplyDelete