Friday, May 25, 2012

Kwa wale wanaoishi kwenye vyumba 1 ama 2 ........tembelea website yetu, http://www.homezdeco.co.tz



Habari wadau, napenda kuwajulisha kua sasa Homez Deco - Kreative Homez inakuja kivingine........
Sasa hivi website/blog site http://www.homezdeco.co.tz yetu hii haitakua iki upload sanaaa picha za kwenye mtanda na badala yake nitakua nikiwaletea makala na kazi zangu ambazo nimezifanya.....
Huu ni mwaka wa tatu sasa tokea nimefungua blog hii, na nilikua nikifundisha na ku download kazi za wengine......kwa ajili ya kufundisha....na nashukuru kua nimefanikiwa hilo...
Imefika wakati sasa ni wa vitendo, naomba tushirikiane kwa hili....
Una swali, nitumie email, picha ya chumba chako na nitakujibu kwa faida yako na ya wengine, bila gharama yoyote ile
Nimekua nikipata sana sana, maombi ya wale wanaokaa nyumba ndogo, nikisema ndogo ni chumba 1 ama 2.
Naomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha kwa maswali, na ikiwezekana piga picha na nita design na kuiweka kwenye website/blog ili iwasaidie wote bila malipo yoyote kuanzia rangi ya ukuta, fanicha zikaeje, mapambo unayotakiwa kuweka, carpet, etc.......na nitakuwekea budget kabisa..... ya baadhi ya vitu ambavyo unatakiwa kuviweka....
Naona hii nitawasaidia wengi kwa jinsi hii....

Karibuni sana sana.....
Ukiipenda kazi yako.....utaifanya kwa moyo wote na upendo bila kujali gharama.....kutoa ni moyo.....
NB:
Naomba upime chumba chako kina upana gani na urefu gani, kila kitu kinatakiwa kwenda kwa vipimo.........dirisha pia lina upana gani na urefu gani kwenye dirisha pima mwanzo wa frem na mwisho wa frem, na kuanzia juu ni pale curtain box yako ama poles imeanzia wapi........





3 comments:

  1. wow, nice initiative Sylvia, thanks

    xoxo

    ReplyDelete
  2. Thanks my dear maana kina sie wenye room 2 na sebule jiko no ilikuwa twaishia tamani tu.Nitajitahid nikutumie yangu ila sebule ndogo hata vyumba na uwezo wa kujenga bado tunajibana kwenye nyumba za watu.

    ReplyDelete
  3. Hi Sylvia, hongera sana kwa kazi nzuri unayofanya. Inatusaidia wengi kuboresha nyumba zetu.

    Naomba dear kama utaweza utuelekeze jinsi ya kusafisha sofa za vitambaa(rough fabric). Natanguliza shukurani

    ReplyDelete