Thursday, November 22, 2012

Site ya Kitunda (Dar) - Homez Deco, tuliweka curtain poles, pazia na vitanda vya chuma na neti .....


 Hapa ndio sitting room baada ya kazi kumalizika jinsi kunavyoonekana...rangi ya ukuta ni blue....hivyo nikaweka pazia hizi, zenye doti doti ziweze kuleta mvuto zaidi.....


Kitanda .....kikiwa na neti yake....(ijulikane kua hatuuzi kitanda na godoro)
 Dinning room pazia zikiwekwa vizuri...
 Dinning room
 Pazia za dinning room
 Pazia za chumbani.....
 Sitting room,
 Pazia zikiwekwa vizuri za sitting room
Hizo ni pazia za jikoni, na hizo nyaya ni za hita......

Nina tatizo kidogo la network, ila linafanyiwa kazi.....Nitawaletea picha zaidi, tukisha solve tatizo hili.....

Nyumba hii  ni mpya, na mwenye nyumba anataka kuhamia mwezi wa kumi na mbili, hivyo anafanya kwa awamu, tumemaliza pazia, vitanda, sasa anajiandaa kuweka furniture zingine zilizobaki, kama sofas, etc.......

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza......

Sorry kua kimya...

Napenda kuwaomba radhi kwa ukimya wangu....Nilikua ninauguliwa na mtoto. na pia naomba kwa baadhi ya wadau, msiwe mnanilaumu, mkiona kimya mjue kuna kitu siwezi kaa kimya bila ku update blog, nami ni binadamu na matatizo humtokea kila mmoja wetu......

Samahani kwa usumbufu mlioupata....

Wednesday, November 14, 2012

I love my self......



Ukijipenda kwanza wewe mwenyewe, basi hata wengine watakupenda. haijalishi una hali gani, tariji, maskini,    mnene ama mwambamba, mfupi ama mrefu, jikubali kwanza wewe mwenyewe na ridhika ulicho nacho......

Kwa kweli ninajipenda mimi kama mimi, na ninafurahi kua mimi kama mimi, na ninafurahia mafanikio yangu mpaka hapa nilipo tena kwa juhudi zangu binafsi.......napenda kazi yangu na ninajivunia kwa kazi yangu...kwani ndio iniwekayo mjini......

Kwa upande wa ngozi yangu hakuna mkorogo hapo hata kidogo.....ni products za shear butter ambazo ziko njiani zaja toka marekani......nitawajulisha humu humu zikifika.

Napenda kushukuru wateja wangu wotee kwa kuni support, na kuniamini, etc.......yaani sijui hata nisemeje.....ninawashukuru mno...

Kazi inaendelea kama kawaida......na tukumbuke ndio tunaingia mwezi wa kumi na mbili...sikukuu ndio hizo karibu....tumejiandaaje?

Kwa upande wa pazia, rangi za ukuta, kubadilisha vitambaa sofa, mapambo, mpangilio wa nyumba, vitanda vya chuma......etc.

Haujachelewa kabisa......Karibu tuwasiliane kwa mahitaji yako ya nyumba yako.


Tuesday, November 13, 2012

Dulux Products (Sadolin Paints (T) Ltd)....Metal paint...



What is Hammerite Paint?
This metal paint combines both the undercoat and topcoat into one. It offers a brilliant glossy finish that feels smooth to the touch, and forms a barrier that provides long-lasting protection by sealing out moisture both out and inside.

The paint is easy to use and you can use it on both non-ferrous and ferrous metals. The most common color of this paint is Hammerite metal paint in red. The paint is also designed in such a way that protects the metal from rain, humidity and even rust.

AVAILABLE COLOURS:
BLACK
BLUE
SILVER
GOLD
WHITE







Sasa tumepata mkombozi, kwa upande wa vitu vya chuma, iwe ni furniruters, iwe ni mageti, iwe ma grill ama chochote kile cha chuma....mkombozi amepatikana....

Tumekua tuki zoea kua kabla ya kupaka rangi kwenye vitu vyetu vya chuma hua tunapaka kwanza red oxide halafu ikishakauka ndio tunapaka rangi tuliyokusudia....Lakini hii hua inachelewesha sana...

Sasa basi Sadolin Paints (T) Ltd sasa wanakuletea mkombozi.....
Product hii mpya inatwa Hammerite.....ambayo iko 3 in 1,  yaani tayari imeshachanganywa Primer, Gloss, na  Undercoat, na unaipaka moja kwa moja kwenye fanicha zako......

Inapatikana katika Rangi 5, ambazo ni:

BLACK
BLUE
SILVER
GOLD
WHITE
Zinapatikana katika ujazo wa, (tshs)

1/4 lit. = 10,000/-
 1/2 lit.  =16,000/-
1 lit. =23,500/-
5 lit. = 113,000/-

Tunakukaribisha kwa mahitaji yako ya Hammerite:

Wasiliana na: 0713 - 920565,  0715-487388





Friday, November 9, 2012

Bidhaa za usafi...Zinapatikana Homez Deco....

 Tumekua tukijenga nyumba zetu nzuri ama kuaa kwenye nyumba nzuri, lakini vipi kwa upande wa usafi? Umeshajiuliza kua, je hizo tiles, ulizoziweka, carpet, Hizi ndizo Products za usafi majumbani mwetu na maofisini ama mahali panapotuzunguka......Matumizi ya bidhaa hizi ni wewe mwenyewe ndio unaaamua utumieje, tofauti na bidhaa zingine ambapo tayari wanakua wame ku limit matumizi......

Product hii hung'arisha sakafu, iwe ni ya tiles, mbao, marumaru......baada ya kusafisha na super 10.....Bei ya Fantastik ni 27,000/-
 Product hii ya care, hutumika majumbani, hospitalini, mashuleni, na sehemu yoyote yenye mikusanyiko....Kazi ya product hii ni huua vijidudu, visivyoonekana, kama maeneo ya vyooni, kwenye masinki, etc...product hii haiharibu mikono na haina kemikali, na pia haijakua diluted....yaani ni wewe mwenyewe ndio utaichanganya kulingana na matumizi yako mwenyewe, tofauti na zingine ulizozoea kuzitumia, tayari zinakua zimeshachanganywa...... Bei yake ni Tshs...20,000/=
Hii ni sabuni hutumika, kuoshea vyombo vya aina yoyote ile, iwe ni glass, masufuria, vyombo vyenye mafuta na huviacha vikiwa ni visafi na bila michirizi etc. hutumika kulowekea nguo laini za ndani, na pia kuogea, na kuoshea mikono.....hutumika pia kuondoa wallpapers.....husafishia mabafu (bath tub), na sehemu zingine za bafuni, tiles, sinks, kusafishia taa...  Bei yake ni Tshs. 26,000/-
 Kwa upande wa nguo, hauko nyuma, sabuni hii ya G! Laundry, ni nzuri kwa kufulia, kwa matumizi ya washing machines(mashine za kufulia) ama hata kwa kufulia kwa mkono...na hubana matumizi kwani unatakiwa kutumia kidogo, kijiko 1-3 tuu kwa ufuajia mkubwa. na ina harufu nzuri.....Pia haichujishi nguo....Ina ujazo wa kg 2.  Bei Tshs. 50,000/-
 Hii hutumika kusuuzia mashuka, mataulo baada ya kufua....nakumbuka nilitoa somo la kuandaa chumba chako kama cha hotel, sasa basi watu wa hotel hutumia product hii kwa ajili ya kufanya mataulo ama mashuka kua soft wakati yanakauka... unachotakiwa kufanya ni baada ya kufua na G1 Laundry, unasuuza na soft, na kuanika...Yakikauka hayatokua magumu ama kukakaaa maa.....Bei  tshs. 18,000/-
Product hii hutumika kila sehemu ya nyumba yako ama ofisi, kwa kufanyia usafi. kuondoa madoa sugu kwenye nguo, jikoni, kwenye masink, kusafisha sakafu ya aina yoyote ile, ikiwamo tiles, mbao, marumaru na matumizi yake ni kidogo tuu na hiyo hapo juu ni kipimo chake....Bei Tshs. 22,000/-

Hii ni furniture polish, ina kazi kuu 3, hairuhusu maji kupenya,  hung'arisha, na huilinda furniture yako. Inahitajika utumie kidogo, hutumika kwenye furniture za mbao, plastics, metal areas, na unaitumia na kitambaa kisafi ama kitaulo, na ni kidogo tuu. Futa vumbi furture yako, paka Lemon Glo, na acha kwa dk. kadhaa na uanze kupolish na kitambaa safi...

Ni rahisi kua na gari iliyooshwa vizuri na kung'aa, na bila rangi ya gari kufifia, Product hii ni nzuri kwa hili, ni 2 in 1 yaani inaosha gari nani pia ni wax ya gari.  Unachotakiwa kufanya ni kuimimina kwenye kifuniko chake ni ambacho kimeshapimwa ni 5mls unachanganya kwenye maji ya 6 lits, ambapo utaweza kuosha mara 100 kwenye kila chupa utakayo nunua......( hutotakiwa kuongeza, nikiwa na maana ya kua uzidishe kipimo, maana gari vumbi litakua linakamata kwenye gari kumbuka ina polish pia)

Wednesday, November 7, 2012

Mali mpya......Mito ya kwenye sofa, sakafuni, na kitandani...(mito na foronya zinatengenezwa na Homez Deco...karibu ujionee tofauti ya mito yetu, na haitoi harufu ni misafi nani soft)

 Mito hii iko tayari kwa kuuzwaaa



 Mito hapo juu iko tayari kwa kuuzwa....imejaa vizuri, muonekano wake mzuri, na pia ni soft sio migumu...na haisinyai mapema......
 Mito ikiwa bado haijavalishwa foronya zake.... mito ya kwanza kushoto ni size 55 by 38
 Mito size 45 by 45
 Mito size 45 by 30


Bei ya mito kwa size hii ni bila foronya zake:

1. 55 by 38 = tshs. 18,000/-mito ya kwenye sofa/makochi, kitandani


2. 45 by 45 = tshs. 15,000/-mito ya kwenye sofa/makochi, kitandani


3. 40 by 40 = tshs. 15,000/-mito ya kwenye sofa/makochi, kitandani


4. 45 by 30 = tshs. 12,000/- mito ya kwenye sofa/makochi, kitandani

5. 88 by 88 = tshs. 45,000/- mito ya chini sakafuni



Bei ya foronya za mito kwa size

 55 by 38 = tshs. 13,000/-

2. 45 by 45 = tshs. 12,000/-

3. 40 by 40 = tshs. 12,000/-

4. 45 by 30 = tshs. 10,000/-

5. 88 by 88 = tshs. 15,000/-

Nakushukuru Mungu kwa kuendelea kutuwezesha...... pole pole ndio mwendo....Haraka haraka.....

 Heavy duty machine
 Fundi akishona neti
Ofisi  yangu kwa sasa.....panavyoonekana... na hizo hapo juu ni sample za rangi yaani hizo za juu, njano, nyekundu na bluu ni primary colors. na mstari wa chini ambazo ni orange, zambarau na kijani  secondary colors.....


Kwa sasa Homez Deco, inapenda kuwafahamisha kwamba, kwa kua tumekua tukiendeleza vitendea kazi, sasa kwa upande wa vitu vya kushona kama neti, pazia, foronya, vitambaa vya meza na mashuka ambayo tutaanza muda si mrefu.....ect.... nguvu imeongezeka mara dufu...

Kwani machine hii ina uweza wa kushona pazia dirisha 10 kwa siku......

Karibuni sana sana......