Wednesday, September 4, 2013

BEFORE MEETS AFTER.....(SITE YA MBAGALA.....TULIPAKA RANGI ZA DULUX........)Kwanza kabisa napenda kuomba radhi kwa kua kimya kwa kipindi kirefu kidogo......na hii ni kutokana na mambo yaliyo nje ya uwezo wangu ya kifamilia..........sasa nimerudi tena....kwa speed kama kawaida......

Homez Deco tuliitwa mbagala na mteja wetu, kwa ajili ya ushauri wa rangi, pazia, furnitures na accessories.....za ndani.

Nasi bila kuchelewa, tulikwenda na kutoaushauri kwao, na baada ya makubaliano ya rangi. tulianza kazi mara moja.......

Picha ya juu ni kabla hatujaanza kazi jinsi nyumba ilivyokua na muonekano wako......na kama uonavyo, rangi zimefifia za ukutani, na haieleweki......hii huchangiwa na ubora wa rangi utumiazo..... picha hizi zikionyesha kabla hatujapaka rangi katika nyumba hii....na kufanya mabadiliko yoyote yale


 ukiangalia picha za juu hapa ni kua katika korido hii ilikua imepakwa rangi ya dark brown, na rangi hii iliifanya hii korido kuoneka kua ni fupi na ndogo, na haina mwanga wa kutosha.......sasa emagine na umeme wetu wa Tanzania ukikatika......inakuaje katika korido hii.......


 Hapo juu ni jikoni ambapo nilipaka rangi ya light green, na kuweka pazia la roman blind, ambapo linafunguliwa na kamba kwa pembeni.....unavuta kwa kwenda juu utakavyo, na kushuka chini na hivyo kufunika dirisha zima....kama inavyoonekana. Rangi zilizoniongoza katika jiko hili ni kutoka katika hicho kitambaa cha pazia.....
 korido inanavyoonekana baada ya kupigwa rangi.... na sasa unaweza kukubaliana nami kua korido hii sasa imekua ni ndefu, na yenye mwanga......
 muonekano wa korido kwa mbali......pia tunazingatia na taa ambazo unaweka katika nyumba yako.tumetumia rangi mbili tofauti...korido na sitting room.
 hii hapa ni living room baada ya kumalizika, nilichokifanya hapa ni kupaka rangi ambayo ni ang'aavu, maana imesaidia kuonekana sitting room kua kubwa, nimeweka poles na pazia ambazo zina prints kwa mvuto zaidi......sasa basi....ukiangalia pazia zangu ambazo zilizoniongoza katika kupata rangi za nyumba hii. ni kua tuliweka sofas za brown...na tukatupia floor pillows. Nyumba hii ina watoto wadogo sasa hatukuweka coffee table ili watoto waweze kucheza, na kupita kwa nafasi.....bila kupata matatizo yoyote yale.....kuumia kwenye meza etc...

Nimetumia mito ya rangi  hizi ili kuweza kufanya sitting room yetu iweze kua ang'aavu na yenye mvuto na iweze kuchangamsha na bila kuchosha..........(kwa mbali kwenye kona tumetumia kwa muda water despensa kama stand ya maua.....wakati tukipanga kwa ajili ya ungwe ya pili ya kununua picha za ukutani, na maua ya kwenye kona ......badala ya kuitupa tumeitumia kama flower stand, ubunifu wa muda........)


Nawashukuru wateja wangu wa hii site ya mbagala.

5 comments:

 1. NIMEVUTIWA NA HIZO SOFA, NAOMBA KUJUA GHARAMA YAKE PLZ

  ReplyDelete
 2. Karibu sana, sofa zilinunuliwa furniture center. bei sifahamu walinunua wenyewe

  ReplyDelete
 3. Nimependa idea ya floor pillows! hivi unazo folonya za hizo floor pillow?

  ReplyDelete
 4. rangi zako za ndani na nje unauza bei ngapi?

  ReplyDelete