Thursday, May 31, 2012
Usafi wa sofa.....(ya vitambaa...)
Nilitumiwa email na mdau mwenzetu, kua alikua anaomba kujua ni jinsi gani anaweza safisha sofa zake, na ni za vitambaa....
Nashukuru sana sana kwa kuuliza swali lako hapa kwetu, nami napenda kulijibu kama ifuatavyo....
Huku kwetu kwa asilimia kubwa hua hatuna utaratibu wa kusafisha makochi yetu, na hii ni kutokana na wengi wetu kuto kujua ni products gani atumie na zinapatikana wapi, sasa inaishia tuu kwenye kufuta futa tuuu, ama tunasubiria mpaka sofa iwe chafu sanaaa ndio tusafishe.... jua kua hapo unakua unaliharibu sofa lako na unalichakaza wewe mwenyewe, maana siku ya kuja kulisafisha ni lazima utalisugua na matokeo yake pale ulipo sugua rangi haitafanana na sehemu ingine,...
Natumai wengi wetu tunajua ama kusikia haya makampuni ya networking, kwa kweli kwa sasa yanakuja kwa kasi na ni mazuri maana yana products nyingi nzuri na ambazo hazijachakachuliwa....ama kua diluted...
Moja ya hii kampuni ni GNLD INTERNATIONAL, Hii kampuni nimeshafanya nao kazi, kwa miaka 3 na nusu, hii ni kua ninawafahamu, na kufahamu products zao.... si mnajua siwaletei vitu bila kujua ama kufanya research kwanza.....
Sasa basi, hii kampuni wana product yao moja kwa upande wa home care.... inaitwa SUPER 10, ni nzuri mno, na kwa wale wanaotaka kubana matumizi, basi products zao hawa ni nzuri maana una dilute mwenyewe kulingana na matumizi na mahitaji yako...
Super 10 kama mnavyoiona hapo juu,,, inahitajika kutumika na spray bottle yake, hii ina vipimo kabisa inakuonyesha.....
Kwa wale wenye sofa za vitambaa, kwanza kabisa, inabidi uipanguse vumbi, ama kama un hoover basi puliza, hakikisha hakuna vumbi kila mahali,
Unatakiwa kua na kitambaa kisafi kama kitaulo kisicho toa mavumbi, ama manyoa, maana itazidi kuchafua.
Hiyo Super 10 unaichanganya na maji katika ujazo wa 1:20 (vipimo viko kwenye spray bottle), halafu unaitikisa, unafanya hivi ili utakapokuja ku spray kwenye sofa isitoke maji, inatakiwa itoke povu,
Ukisha spray, unachukua kitambaa chako na unaanza kusafisha kwa design ya mduara, na usipulize sehemu kubwa, unakwenda kidogo kidogo.... mpaka unamaliza.
Baada ya hapo acha sofa lako likauke na utakua umeshafisha sofa lako, bila gharama kubwa....
Haihiitaji kua na hela nyingi kusafisha sofa yako kwa kutumia Super 10....
Upatikanaji wa Super 10, ni mpaka uwe member wao, na hapo kunakua na punguzo la bei, ila sio lazima kujiunga, unaweza kununua kwa mtu ambaye tayari ni member wao.
Naomba kwa watakaohitaji, mpigie huyu kaka anaitwa Tija, na kwa walio Dar anaweza kuja hata akakuonyesha jinsi ya kusafisha hapo hapo nyumbani kwako ama hata ofisini...
TIJA
0713 - 336977, - 0754 - 006977
Ni hayo tu kwa leo...... siku njema...
Wednesday, May 30, 2012
Monday, May 28, 2012
Apenda ipi wewe...........(http://www.homezdeco.co.tz)
Habari za weekend, kwangu ilikua safi, busy kweli kweli, mie hua sina likizo, weekend, holiday etc....... na ninafuraha sana sana.........
Angalia design kati ya hizi uliyoipenda, na kulingana na sink lako la jikoni lilivyo, na waweza kutengeneza kwa fundi aliye karibu nawe......
Rack hizi husaidia sana sana, kua msafi, na dasta za jikoni ama makosheo kuto toa harufu,, na jiko kua safi muda wote. Kumbuka mahali hapa ndipo chakula hutayarishwa na kupikwa, sasa kila kitu kinatakiwa kua kisafi.......kuepuka magonjwa........
nawatakia siku njema.........
Friday, May 25, 2012
Kwa wale wanaoishi kwenye vyumba 1 ama 2 ........tembelea website yetu, http://www.homezdeco.co.tz
Habari wadau, napenda kuwajulisha kua sasa Homez Deco - Kreative Homez inakuja kivingine........
Sasa hivi website/blog site http://www.homezdeco.co.tz yetu hii haitakua iki upload sanaaa picha za kwenye mtanda na badala yake nitakua nikiwaletea makala na kazi zangu ambazo nimezifanya.....
Huu ni mwaka wa tatu sasa tokea nimefungua blog hii, na nilikua nikifundisha na ku download kazi za wengine......kwa ajili ya kufundisha....na nashukuru kua nimefanikiwa hilo...
Imefika wakati sasa ni wa vitendo, naomba tushirikiane kwa hili....
Una swali, nitumie email, picha ya chumba chako na nitakujibu kwa faida yako na ya wengine, bila gharama yoyote ile
Nimekua nikipata sana sana, maombi ya wale wanaokaa nyumba ndogo, nikisema ndogo ni chumba 1 ama 2.
Naomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha kwa maswali, na ikiwezekana piga picha na nita design na kuiweka kwenye website/blog ili iwasaidie wote bila malipo yoyote kuanzia rangi ya ukuta, fanicha zikaeje, mapambo unayotakiwa kuweka, carpet, etc.......na nitakuwekea budget kabisa..... ya baadhi ya vitu ambavyo unatakiwa kuviweka....
Naona hii nitawasaidia wengi kwa jinsi hii....
Karibuni sana sana.....
Ukiipenda kazi yako.....utaifanya kwa moyo wote na upendo bila kujali gharama.....kutoa ni moyo.....
NB:
Naomba upime chumba chako kina upana gani na urefu gani, kila kitu kinatakiwa kwenda kwa vipimo.........dirisha pia lina upana gani na urefu gani kwenye dirisha pima mwanzo wa frem na mwisho wa frem, na kuanzia juu ni pale curtain box yako ama poles imeanzia wapi........
Shoe rack ......
Bei za shoe rack ni kama ifuatazo:
1. Pea 20 Tshs. 90,000/-
2. Pea 30 Tshs. 120,000/-
3. Pea 40 Tshs. 150,000/-
4. Pea 50 Tshs. 180,000/-
5. Pea 100 Tshs. 250,000/-
Ukitoa oda inachukua siku 5 kua tayari.....
Karibuni.............
Wednesday, May 23, 2012
Mbezi Beach Project.....Iron furniture by Homez Deco.....
Dinning table.......ya viti 5.....
Mto ukiwa na cusion cover na tayari kwenda kwa mteja...
Mto ukiwa na linning....
Kiti kikianza kuonyesha muelekeo....
Ninashukuru mungu kua sasa nimeweza kuwapatia vijana ajira hapa mtaani kwetu kwenye ofisi yangu........
Hapa nikikagua kazi, mito kama ujazo uko sawa na inakaaje kwenye kiti....kazi hazitoki mpaka nimezikagua.....
Hii ndio kazi ya yale magodoro madogo madogo ambayo tuliyakata kata vipande vidogo vidogo, tukavichanganya na fiber, na tukashona decron tunazitumbukiza ndani mchanganyiko huo, na tunashonea lining, mwisho tunashonea foronya ama cover, na mto unakua tayari.
Kama kawaida yetu Homez Deco, hatufichi kitu, mito yetu ni imara na haina harufu hata ukimwagia maji, utauanika na utakauka na hakuna harufu itakayotoka ama kutoa alama kwenye mto....maana tunaweka vitu visafi tuuu..... mito ni soft na inadumu kwa muda mrefu bila kusinyaa.....
Hii ndio ile nyumba ambayo nilitengeneza curtain poles za chuma, vitanda vya chuma, vya four posters, nikawaonyesha, na last week tukamaliza na meza ya chakula na makochi..... wishing you all the best my dear customers.......
Asante sana mteja wangu na zawadi yako ya magazine rack iko jikoni......nitawaonyesha......
Tuesday, May 22, 2012
Mrs. Jossyanne & Me.....(Landscaping & Gardening)
Jamani kama nimenenepa vile........ hahahhaha....hahhahha... ngoja nianze mazoezi, maana nikichekea unene nitavua mabua.......
Mrs. Jossyanne yuko, naomba tumtumie, maana hua akikaribia kuondoka ndio utakuta tunatafutana, safari hii yuko kwa muda wa miezi 3 hapa TZ.... Kwa wote wale wenye maswali ya landscaing & Gardening tuwasiliane, na tutapanga kuja kwako na kutoa ushauri....
kwa wale wa mikoani, tuwasiliane kwa simu.........YUKO NCHINI TUMTUMIEKWA USHAURI, NA KUFANYIWA KAZI KABLA HAJAONDOKA.....
Friday, May 18, 2012
Wall Candle holder....
............Mimi binafsi nimezipenda, na zinapendeza sana kwa wale walio na space ndogo kwenye nyumba zao....
mmmmhhhhhhhhh!!!!!!!! Asante....na Mungu akuongezee pale ulipopungukiwa....
[Homez Deco - Kreative Homez] New comment on Maandalizi ya Website yakiendelea.......
Hide Details
FROM:
Anonymous
TO:
sylvianamoyo@yahoo.com
Message flagged
Wednesday, May 16, 2012 4:00 PM
Anonymous has left a new comment on your post "Maandalizi ya Website yakiendelea......":
wewe acha kisema ivyo idea ipi watu tunayo hio idea siku nyingi nikwambie ndugu yangu njoo taratubu au idea gani tucukuwe mbona kuna watu wanafanya kazi kama yako na ni kubwa na ww pia unapata idea kutoka kwao,ebu niambie mbona unatupa idea ya kusafisha nyumaba na kuweka vizuri tunachukuwa,usiwe mchoyo utaboa na watu hatutakuunga mkono,mwamgalie joseline upo wapi na sio mchoyo semuse wewe mtoto wa kichochoroni ndo mana umelea mimba mwenyewe
Moderate comments for this blog.
Posted by Anonymous to Homez Deco - Kreative Homez at May 16, 2012 4:00 PM
Hii ni comment ambayo nimetumiwa.
Any way nadhani ile mada watu wameielewa vibaya na wameichukulia visivyo, ukiisoma vizuri, kwa kutulia utaielewa, na kuliko kupoteza mudawako na kuandika haya uliyoyaandika, matusi, kashfa etc.....
Hii ni moja ya comments zambazo kidogo haijavunja maadili ya kitanzania, kwa upande mwingine ni matusi.....
Blog/Website hii ni ya watu wastaarabu, na wanaopenda kujifunza, etc... sio blog/web ya matusi, malumbano kama baadhi ya hawa watu wanavyochukulia,
Mimi kulea mimba mwenyewe, kulea mtoto mwenyewe haikuhusu, na hayo ndio maisha niliyoyapanga, na ninayafurahia mnoooo......na sijui huyu malaika wa mungu, mtoto wangu amekuingiaje mpaka ukamuhusisha huku,
Kazi yangu hii nimejitolea kuelimisha na tunaelimishana, mimi sio malaika kwamba kila kitu najua, tunasaidiana na kuchangia wote kwa pamoja.......ni wangapi wanaofanya kazi kama yangu, wanachukua muda wao na kuelimisha, kutoa ushauri bila malipo???????
Ninachotaka na ninachopenda ni kwamba hata kama mtu una aidia yako na umeitoa kwa uma..... kuna watu wanataka wasikie kitu ndio wakianzishe, sio waumize vichwa, na akili zao waanzishe etc. basi hata kama kuiga... EDIT basi........
Hawa watu wapo, na nitaendelea na msimamo wangu huo huo.......
Unapenda kitu umekiona humu, chukua, peleka kwa fundi aliye karibu na wewe etc.... Sijamaanisha kua wote wanaochukua vitu humu basi ndio niliowasema.... hapana, hapana, hapana......
Naomba kuwataarifu kua, comments zote, ni lazima zipitie kwenye email yangu, nazisoma, halafu ndio ninaziruhusu, sasa wewe unaetuma matusi, maneno ya kashfa etc. hapa sio mahala pake, na kamwe lengo la blog/website halitobadilishwa na wanaotukana matusi ama kunijaribu kwa njia ingine ile yoyote. Unajipotezea muda, na nguvu bila sababu...... Ila pia nakuombea mungu akunusuru kwa yote maana hujui ulitendalo.......
Kinachoniuma ni mimba yangu ambapo sasa nina mtoto, amekukosea nini.........?????????????????
Challenge za biashara ninazipenda, na ndizo zilizonifikisha hapa, maana ninazifanyia kazi.......
Ninawashukuru wadau wote kokote mliko kwa support yenu, na tunaendelea na kazi kama kawadia, unahitaji ushauri, ufanyiwe kazi, na ninapokea ushauri pia kutoka kwenu, na kubadilishana mawazo....etc... karibuni sana sana sana.........
Mungu awabariki kokote mliko........
Wednesday, May 16, 2012
Comments.......
Naomba kujibu baadhi ya comments zenu ndugu wadau....
1. Kuna mdau aliniuliza wapi anaweza pata magodoro dodoma, ila hakuniambia kama yuko Dar ama mkoani. kwa Dar. anaweza kwenda duka liko karibu na maktaba kuu ya taifa unarudi nyuma jengo la pili. kuna duka la wahindi pale wanauza.....
2. Viti vya garden tunatengeneza naomba tuwasiliane kwa simu ama email. sylvianamoyo@yahoo.com, niweze kukutumia catalogues.
3.Uliye mkoani kitanda ama furniture za chuma ama chochote utakacho kutoka kwetu, unaweza kukipata, tutakutumia kwa njia ya basi, ama lori.... tuwasiliane zaidi kwa simu, 0713-920565
karibuni...
Second hand Furniture.....
Nimeanza kwa kuweka baadhi ya furnitures, na kwa kweli kipengele hiki kimepokelewa vizuri kweli. Ninaendelea kupokea simu za kuulizwa furniture kama kuna zingine.........
Nilichokua nikiwaomba ndugu wadau, kama una furniture ungependa kuiuza, ila iwe kwenye hali nzuri, nakuomba tuwasiliane, ili nije niiangalie na niikague kama itaweza kufaa kuuzwa, nitaipiga picha na kuja kuitangaza hapa,
Hii itakusaidia wewe, kwanza kupunguza vitu ndani, hela utakayoipata itakusaidia kwa mambo mengine ama kuongezea na kununua kingine, na nyumba yako ikaonekana ni nzuri na safi na yenye mpangilio mzuri, na utatusaidia pia sie tunaohitaji kupata vitu vizuri kwa bei nzuri........
Kwa wale wa mikoani msihofu, nanyi sijawaacha nyuma, piga picha furniture yako na nitumie kwenye email hii sylvianamoyo@yahoo.com, nitahitaji unipigie kila upande, niangalie, na pia kama ina matatizo kidogo nijulishe ili niweke bayana kwa wadau wenzetu waweze kujua.
Nipigie simu namba 0713 - 920 565 kwa maelezo zaidi.
NB;
Kutakua na kulipia tangazo na litakaa kwa mwezi mzima, kwenye website yetu, na tutaweka contacts zako muuzaji, sisi homez deco hatutokua watu wa katikati. mta deal nyie wawili, muuzaji na mnunuzi. kazi yetu ni kutangaza tuuu.... naomba muuzaji wa mali ikitoka/ikiuzwa mtuambie, ili tuweze kuliondoa tangazo.
Nawashukuru wote.....
Karibuni sana sanaaaa........
Monday, May 14, 2012
Hizi ndizo Siri 12 unazotakiwa kuzijua kwa ajili ya nyumba yako unayoitarajia ama uliyonayo....
Ukiwa na plan iliyokamilika, ya nini unataka unaweza ukapanga uanzie wapi, na kwa awamu. Hii itakusaidia, kuepuka ama kupunguza makosa ya kuweka vitu kimakosa, kama switch etc.
2. Floor plan yako iliyokamilika ni nzuri kwa kuanzia:
floor plan nzuri na iliyokamilika inakusaidia kujua ukubwa wa sehemu yako na vipi utapangilia furnitures zako kwa size na bila ya kua na mlundikano wa vitu ndani.
3. Uchaguzi wa taa, switch, sockets etc. ni uamuzi mzuri:
Ipi inakwenda wapi, na inakaa wapi, inatakiwa ijulikane kabla ya yote, na mpangilio mzuri wa taa unahitajika angalau kwa njia 2 ama 3 za switches. Na pia, katika kundi hili kuna sockets za simu, computers,pasi etc. zote ziwe kwa mpangilio mzuri.
4. Uchaguzi wa rangi ni rahisi kupatia nani rahisi kukosea:
Kupaka rangi kwanza sio chaguo zuri kwa kuanzia, rangi zina tabia ya kukufanya ujisikie vizuri ama vibaya kulingana na ulivyozichanganya, Ushauri wa Interior decorator ama designer, utakusaidia sana kufanya asubuhi yako kua nzuri, na jioni yako kua ya mapumziko.
5. Style hubadilika:
Style sio tuu iko kwenye muonekano, lakini hata pia kwa ajili ya jengo, na pia ni muhimu kwenye project yako hii na kukufanya uwe makini kwenye hii project yako.
6. Kua na imani na subcontractors:
Subcontractors unaowachakua ndio mwangaza wa project yako, na hakikisha wanafanya kazi ontime, wanafanya vizuri, sio wababaishaji na wawe na uzoefu wa kutosha, usipokua makini, project yako hii inaweza ikawa ni mojawapo ya ndoto mbaya siku zote.......
7. Kila mtu ajue:
Ni vizuri mwenzio ajue (Husband or Wife) nini unataka kufanya na mkubaliane, ili kuepuka kurudia vitu mara mbili mbili,
8. Picha za ukutani:
Pata ushauri wa jinsi gani ya kutundika picha zako za ukutani, kutoka kwa professionals, na itakusaidia kua kila kitu kinakwenda kwa mpangilio, na kupendeza.
9. Mapambo:
Mapambo sio rahisi kama tufikiriavyo, maana hii ni kitu muhimu sana kwenye project yako, Kua na uchaguzi mzuri wa mapambo ni kama vile vile unavyopanga hii project, bila kuidharau. Hii ni hatua ya mwisho na inatakiwa ipendezeshe na sio kuchukiza, ama kukaraisha. Jaribu kwenda taratibu na kila pambo, ina hii itakusaidia kutokua na vitu viwili viwili, na kuharibu budget.
10. Landscaping/garden:
Hii ni kama nguo, yaani ni muonekano wa kwanza kwenye nyumba yako. Muonekano wa nyumba yako kwa nje siku zote unatakiwa kua mzuri, msafi , wakuridhisha na ulioko kwenye mpangilio mzuri. Ni viziru kua na plan ya garden yako kabla haujaianza ama kuanza kununua maua etc. Utakapokua na plan yako na umeridhika nayo sasa, anza kuangilia systems za maji, kabla ya kuweka udongo, mbolea etc. Baada ya hapo sasa unaweza kuendelea na kuanza kuifanyia kazi kwa kupanda etc.
11. Fengshui:
FengShui is a Chinese Science that has to do with the energy in your house and office. Their basic principles are that the good energy is running very smoothly all around your place. A good combination of fengshue and a good design can be a great asset.
Today in the western hemisphere you will find many interior designers and architects that naturally incorporate these basics in their projects. (nitaielezea zaidi kipengele hiki)
12. Vitu vya kuzingatia kwanza.
Nafasi, ceiling, kabati ya nguo, milango, taa, sauti, jikoni, sakafu, rangi, pazia, garden, picha za ukutani, ukuta.
Friday, May 11, 2012
Maandalizi ya Website yakiendelea......
Huyu ndie aliyewezesha website yangu mpaka iko hewani, na yeye ndie atakua akihusika na maswala yote ya website, isiende kombo.........ni web designer......sio kwamba ninamsifu, ila katika kutafuta web designer wa kunifanyia kazi yangu hii, nikakutana nae, tena nilimpata kwa mteja wangu mmoja ndio akaniunganisha nae. Anaitwa Kaduma huyu web designer wangu.
Yaani this guy, anajua anachokifanya, na anajua kazi yake, hana haraka haraka ya kufanya kazi bora liende tuu... ana anafanya kazi kulingana na wewe unachokitaka na anakupa ushauri, na hakatai mawazo. Na imetuchukua kama miezi 2-3 hivi, maana tulikua tukiiandaa na kupumzika na kutafuta hela... hhahha si unajua tena tunajikongoja... hahaa.... lakini hakuchoka wala kukasirika. etc..... kwa ufupi he is a great guy of all.......atakaemhitaji contacts zake ziko hapo juu kwenye tangazo.......then utakuja kuniambia.....
hahahaha, imetokea wote leo tumevaa blue..... hhahahaha.... ila tumependeza ehehehhe hahahaah
Bado tunaendelea na kuijazia sehemu ambazo zinahitajikaa, maana ninataka iwe ni directory ya Interior decorations, etc...... sasa jamani si kazi ndogo hii naomba tuwe tunavumiliana pale ambapo ninachelewa ku post, ingawa sitakua ninakaa muda sana..... na hii ni kwa ajili yenu ndugu watanzania wenzangu, ninataka ifike mahala sasa, unahitaji kitu basi wewe unaingia kwenye website na blog yangu na kutafuta kampuni unazozitaka, na kwenda kwenye website zao.... na hii naona itasaidia sana sana, wawe wana update website zao mara kwa mara kwa kuweka vitu vipya walivyoagiza.
Natumai kwa kufanya hivi jamani tutakua tunaokoa muda, maana kwa sasa unahitaji kitu nahujui wapi pa kukipata, mwishowe hela unakula.......
Kwa kusema ukweli hii kazi ni ngumu, maana ni mpaka makampuni yaelewe na wanikubalie, sasa sio kazi ya leo ama kesho kukubaliwa, ila ninaamini nikiianza mapema itakua rahisi kwetu wote sote...
Ninajaribu kuwapa mawazo yangu ya nini nafikiria kukifanya na wapi tunakwenda, ninahitaji ushirikiano wenu wa hali na mali, kwa kunivumilia ili tufikie malengo.....ifike pahala na sie tunaweza kununua vitu online kwenye makampuni yetu ya nchi yetu hii.......najua inawezekana na ndio maana ninataka kuifanyia kazi......
Jamani kuna watu wamekaa tuu na kutafuta mawazo ya watu na wao waige ili watoke....... naomba kusema kua sitoogopa, wala kumuonea mtu huruma, nikiona mtu kaiga haya mawazo yangu na kuyafanyia kazi........yaani nitamuaibisha mpaka atashangaaaa, na nadhani kwa hili ndugu wadau tutasadiana na watu wa namna hiiiii.
Kwa haya mafupi napenda kuwashukuru wote kwa kuendelea kua nami na mnaendelea kua nami maana bila ninyi nisingefika hapa nilipo na kujivunia kazi yangu......naendelea kuomba mawazo yenu juu ya hi website yetu, kama kuna kitu tuongeze, tupunguze, etc.... nitayapokea na kuyafanyia kazi....
Nawatakia weekend njema.......