Monday, October 25, 2010

Ucheleweshaji wa ku update blog...

Naomba kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi wadau wangu wote kwa kua nachelewesha ku upload blogspot hii yenu, najua nawakera,na nawaudhi etc.

Ila nawaomba mnivumilie katika kipindi hiki nilichonacho, maana siku zingine naamka ndivyo sivyo, mara mgongo, miguu etc. Nawaombeni radhi sana sana, maana pia naangalia na afya yangu kwa ujumla na kiumbe nilichobeba.

Najitahidi kadri niwezavyo nisipilize muda mrefu ku update, maana mambo ni mengi na hua sikurupuki, ni lazima nivifanyie kazi ndio niwaleteeee. Kwa upande wa kazi, kazi inaendelea kama kawaida, maana nina vijana nani wachapakazi wazuri.

Siwezi kumpa mtu password akawa ana update, si unajua anaweza akafanya atakacho na wananchi msinielewe.

Asante sana kwa uvumilivu, though wengi wamekua wakilalamika kwa nini si update, nawaomba mniwie radhi kwa hili


No comments:

Post a Comment