Thursday, January 26, 2012

After........Living room transformation @ Tabata.......(Nakushukuru mteja wangu wa Tabata.... )


Sina mengi ya kuongea...sofa ni L-shape na 2 sitter moja ila kila kitu kina wezekana ukijipanga, hapa tumeanza na sofa.... tutakuja mapazia, then decorations...... ambapo rangi hii ya sofa, inakubali kutupia pillows, na throws color yoyote ile........
Mbao tunazo, sponges zipo... etc,

Dunia ni yako, Chaguo ni lako...

(Ukiamua kuvaa, nyumba ikafuata,ama, ukiamua kutengeneza nyumba, then kuvaa kutafuataa.... uamuzi ni wako)

Haujachelewa kupanga ratiba ya nini cha kubadilisha nyumbani kwako......

Tuwasiliane, kwa ushauri, huduma zetu......

Regards
Sylvia a.k.a mama Jaydan....

NB: Kazi hii ilichukua wiki moja na nusu,, na kama kawaida ya Homez Deco,, tuna Time Frame..... Alipata muda tuliokubaliana........
Mtanisamehe kwa picha, ila ninajitahidi kupiga eheeee, so mungu akipenda  nitatafuta professional photographer apige kazi zangu.....NO NO NO ......

katika pita pita yangu, kwenye net, nikakutana na hizi picha, pls chooni hua hakuwekwi pazia ndefu.  shower curtain ndio inatakiwa kua ndefu. lakini sio pazia.........

this is correct... pazia linatakiwa liwe fupi.......... sehemu ingine pazia linatakiwa kua fupi, ni stoo, jikoni. .........


Rgds,
Mama Jaydan.....

Publishing comments

Habari zenu wadau,,,, napenda kuwajulisha kua, comments zenu hua ninazijibu, muwe mnaangali katika artical ambayo umecomment,

pls ndugu mdau uliyenitumia comment kua sijakujibu, hebu angalia katika artical uliyotoa comment, na utakuta jibu... kwa maswali zaidi tuwasiliane, 0713 - 920 565


Regards,
Sylvia aka Mama Jaydan

Before & After.... living room furniture......... at Tabata.
Hapa ni kabla ya sofa set kubadilishwa, nilimpelekea catalogues mteja, na akachagua design ya L shape, baada ya hapo, nimwambia kwa design ya L-shape ni lazima nije kupima sitting room yako ili tujue itachukua space kiasi gani, na ibaki kiasi gani,,, so tulikubaliana na nikaenda kwake, nikapima, akanipa advance, na nikaanza kazi, Ilichukua muda wa wiki moja na nusu kumaliza kazi. 

Rome haikujengwa siku moja,...... tulianza na sofa, tutakuja na mapazia etc. Ninachoweza kusema ni kwamba usisubirie eti mpaka upate hela nyingi ndio uanze kuiremba nyumba yako, kidogo ulichokua nacho jipange na uanze, hata siku moja hela haiwi nyingi na ikakutosha........Hizi ziuatazo ni steps za sofa jinsi tunavyotengeneza, kweli ninawaapia, sofa inayotoka hapa kwetu, hatofautiani na hizo za mamilions za huko kwa wenzetu,,,,,,, jamani mbao zipo, almost malighafi zote ziko hapa kwetu tanzania, sasa kwa nini tuhangaike? Mafundi wangu wamekua trained, na ni wasai kwenye kazi, kwenye sofa zetu, hakuna msumari utakaouona, hakuna nyuzi utakayoiona, etc,  

Hapa mnapopaona ni mahali ambapo kazi hufanyika ya sofa, nahii ni kwasababu bado tunajikongoja na mitaji....so kwa kuanzia ndio tuko hapa, ila mungu akipenda, tutakua na warehouse kuubwa,, itakayokidhi biashara yetu,so tuwee pamoja katika hili........


Fundi akipima kitambaa cha sofa...... ni quality, tujitahidi kuangalia quality na sio quantity....

Hii sofa kwa chini, kama mnavyoona ni kua hakuna makorokoro ama uchafu, maana hua ndio unao attract panya.....

Hukuti uchafu hata ukijafumua,,,,,, kila kitu kiko wazi, actually hii ni sofa ingine, nilikua ninawaonyesha tuuu usafi wake.....kabla hatujafunika kitambaaa....

fundi akifunika sofa kitambaaaaaa anapiga staplers, hizi ni za sofa,, then anashona......

hapa akifunga miguu ya sofa.....


unaona usafi wa sofa... sio kama sehemu fulani hivi, jamani sofa nje inaridhisha ila huko ndani duh.... panya ndio wanakua familia.....

Kitambaa kikifunikwa......

Hii ni sindano special kwa ajili ya kushonea sofas.... kweli hazipatikani hua ninaagiza nje ya nchi...... so hua ninakua nazo makini sana ofisini......fundi akifanya mambo... anashona sofa, hakuna uzi unaooneka hapo...... mteja mwenyewe amenikubali,,,,, hahahhaha...kitambaa kikifunikwa.... chini ya sofa.......


Almost...... tunamaliza.... stay tuned........

Wednesday, January 25, 2012

Kazi imekwisha........

Pazia inatakiwa ikae hivi........ umeona marinda yalivyokaa na kujipanga... ni rahisi, usijali nitawaelekeza.......Dinning... hiyo scarf ya dirishani inaweza kuwekwa design nyingi tuuu ni utundu ma mtu, waweza pitisha katikati, etc.......

Baada ya kazi nikimsubiri mwenye nyumba nimkabidhi kazi yangu........

Toilet ya master... hizo tiles zina papo na pink kwa mbali. Vyooni hua tunaweka hizi shee.......

Master Bedroom,.........

Tuesday, January 24, 2012

Tulianza na curtain poles, sasa ni mapazia..........

Hapa ni sitting room, kama mnavyoona, tumeweka curtains za rangi ya dark brown, ukuta ni rangi ya butter scotch, na makochi kama mnavyoyaona.... moja kwa moja hapa color inayotakiwa ni neutral color....
baadae tutabadilisha vitambaa vya sofa, hizo pillows....twaenda kwa awamu, nyumba ni mpya ndio wana miezi 3 tokea wahamie... so tunafanya vitu kwa awamu....INAWEZEKANA


curtain fixer, ofisini kwangu, mafundi ni wengine, curtain fixer ni wengine. na kila mtu anajua kazi yake wakiwa kazini


tunaangalia ilivyokaa....

tunarekebisha,,,, unajua bwana ukipenda kazi yako, ama biashara unayoifanya, utafanya kwa ustadi mkubwaaa, hapo unavyoniona, nilikua ninaiweka pazia vizuri kwenye curtain holder yake, nikiwa site(kwa mteja) hakuna cha bosi wala mfanyakazi, wote tunaingia mzigoni. nikimuonyesha fixer kitu.....


Hapa nikipanga gathers za pazia(marinda)....

dinning area...

hivi ndivyo pazia linatakiwa kukaa, yaani unaona marinda tokea juu mpaka chini....

upepo......nilichopenda huku ni kuna hewa,,,hakuna mbanano wa nyumba jamani...

Hapa nikitayarisha pazia za chumbani......hua sometimes, nina fitisha pazia, kama dirisha ziko nyingi, ntawaonyesha siku nikiwa ninaning'inia juu ya madirisha.....well I love my job....

nimemaliza kuweka hooks, fixer anafanya kazi yake, huku ni chumbani....master

kuna jinsi ya kushika pazia kuweka kwenye curtain holder ili kupata marinda...... nitawaonyesha...


well fixer, akifuatilia marinda...Zoezi litaendelea...........