Friday, February 28, 2014

NEUTRAL UKUTANI NA COLORFUL KWENYE FANICHA NA MAPAMBO.......


Kuna njia moja rahisi sana kwa wale wapendao colorfull kwenye nyumba zao....iko hivi...unapopaka rangi ukutani ambayo ni colorfull halafu ukaja ku mix and match na fanicha na mapambo.....hua inakuja kukuchosha baada ya muda.....na mara nyingi ni kua tunapaka rangi zisizoendana.....

nimeshaona kwenye baadhi ya nyumba zetu utakuta mtu anaweka rangi zaidi ya tano.....na hii huja kumahinda...na kufanya nyumba kuonekana kituko.....jamani kutumia rangi zairi ya tatu.......pls pls......pata ushauri kutoka kwa interior designer.....atakushauri kwa gharamma nafuu ni kukubaliana tuu na nyumba kuonekana nzuri na kuvutia.....hiyo ndio kazi yetu kuumiza vichwa kila siku ili kupendezesha nyumba yako.

nimeweka baadhi ya picha hapa ili muone rangi zinavyokwenda kwa mpangilio....hata kama ni nyingi lakini zinashabihiana...sio moja inamzidi mwingine na kuwaka sana ......


Napenda kutoa picha ili tuweze kuelewana zaidi.....na ukitumia rangi za kuwaka ni lazima utumie na rangi zilizopoa ili kuipunguza makali ile kali.....na kwa ushauri wangu endapo gutaki kutumia designer kwa kudhani kua unakwepa gharama...ama utamfaidisha interior designer. .....basi naomba na ninakupigia magoti.... kua heza na rangi 3 tuuuuuu...na tena ziwe zinaendana sio kupishana....hii itakusaidia nyumba yako kuto onekana kituko na kuchekesha walionuna....sasa basi....paka ukuta wako rangi neutral. ..kama cream, beige, butterscotch,  etc....halafu hizo rangi 2 zilizobaki ndio cheza nazo kwenye fanicha na pazia na marembo.....na pia waweza irudia ile ya ukuta kwenye mapambo pia sio mbaya....
picha hizi 2....kuta ni neutral...then colors kaweka kwenye fanicha na mapambo....kiasi kwamba unaweza badilisha muda wowote wakati wowote mapambo na pazia...bila kuugusa ukuta ama kukuumiza kichwa kuubadilisha rangi.....


mfano picha hii ametumia rangi 3....kijani, pink, na nyeupe....na nyumba imependeza.......sasa ule ujuaji wa ma color combo tuuache kwenye nyumba zetu.....na kwa taarifa tuu color combo hua zinapendeza zaidi kwenye nyumba kubwa na zenye mwanga wa kutosha....ambapo kuna madirisha makubwa.....

No comments:

Post a Comment