Thursday, May 30, 2013

Kazi imemalizika katika nyumba ya kinondoni katika zoezi la rangi...na pazia......


 Hapa ni sitting room ambapo nyumba hii ina madirisha mawili......homez deco tulilipaka rangi na baada ya hapo tukaweka pazia.....na huu ndio muonekano wa baada ya nyumba kuisha kupaka rangi.....mteja wangu alihitaji rangi zilizo poa....ambazo kwa upande wa rangi za Dulux utazipata katika group ya neutral colors.....
nilimpa mawazo yangu akayakubali...na nilichokifanya baada ya hapo ni kutafuta pazia zilizo la light colors.....


 Hizi ndio colors nilizozitumia.....sitting room na dinning ukutani......
 Nyumba hii kidogo roof yake iko chini, sasa basi kama tungepaka rangi ambazo ziko dark ukutani...nyumba ingeonekana kua ni ndogo......kwa upande wa pazia niliweka pazia zenye mistari kama hivyo inavyoonekana....mistari ya kutoka juu mpaka chini.....pazia za aina hii husaidia kufanya dirisha na na roof kuonekana kua ni ndefu.....

 Unaweza kuweka pazia aina tofauti lakini zikawa na theme moja....hasa kwa zile sitting room na dinning room ambazo zinaangaliana.....dinning kulikua na madirisha 2 pia.........

 Kwa upande wa furnitures......ametoa zote anataka kununua mpya....na amekubali nimshauri katika ununuzi wa fanicha.......
 Na pia meza ya samaki itatoka hii yote itajumuishwa katika ununuzi wa furnitures.....
Nilikuta hizi dolls....nikaona sio vibaya kupiga nazo picha........ tutawaletea mpaka mwisho wa hii nyumba .......

NB:
Katika ukarabati wa nyumba yako....unao uwezo wa kufanya kwa hatua......kwakujipanga na kazi ikimalizika inapendeza ..........

1 comment:

  1. samahan dada kwa usumfu,naomba kma unaweza kupata pic za madirisha ya kisasa yenye gril na vioo vya aluminiam utuwekee,mna natafuta madirisha ya kisasa nione.naomba usipuhuzie jmn hta pic mbili au 3 nitashkuru,ongera kwa kz nzri.

    ReplyDelete