Somo letu linaendea........na leo tunaangalia upande wa matayarisho ya ukuta kabla ya kupaka rangi......
Kuna msemo usemao: DAIMA SAFISHA NA PAKA RANGI...... NA SIO PAKA RANGI NA USAFISHE.
Sasa sisi tunageuza na tunatumia: PAKA RANGI NA USAFISHE.....
Msemo huu Daima safisha na paka rangi maana yake ni kua, katika matayarisho ya ukuta kwa ajili ya kupaka rangi, tunahitajika kutumia 80% katika kutayarisha ukuta, na 20% ndio kupaka rangi......
Ila sisi ama wengi wetu tumekua tukitumia 20% Kutayarisha ukuta na 80% ndio kupaka rangi....kitu ambacho ni makosa makubwa mno....na hii ni kutokana na ama fundi hajui, ama mwenye nyumba ana haraka ya nyumba kuisha, ama mwenye nyumba anakwepa gharama, ama fundi amedanganya na kupotea na hela....na sababu nyingi nyingi......
Hawa ni baadhi ya maadui wa rangi katika ile 80% ya kuandaa ukuta:
- Kabla ya kupaka rangi yoyote ile kwenye ukuta, hakikisha sehemu hiyo iko katika hali ya kuridhisha, nikiwa na maana kua kuna maadui wa rangi ambao ni vumbi (kuta zenye vumbi mfano wa chokaa...kama gypsum powder ni mfano wa chokaa), oil, grisi, kutu, mchanganyiko wa kemikali, unyevu, na fangasi ama vimelea vya wadudu.
- 80% ya malalamiko ya kuhusu rangi yanatokana na maandalizi duni ama yasiyo sahihi ya ukuta, kwenye usafi, kuziba matundu, kuondoa rangi iliyobanduka na isiyokamata vizuri, kutoondolewa kwa ukungu na fangasi, kutokusafisha vizuri kuta zenye chokaa, ama kutondoa rangi ya zamani na varnish etc.....
Hapo chini tunaoneshwa kua hayo ndio maandalizi ya ukuta ambayo tumeyazoea na tumekua tukiendelea nayo.
- Njia ya kwanza tuliyoizoea baada ya kujenga nyumba hua tunapiga ripu.(ripu ni mchanganyiko cement na mchanga).
- Pili, tunafanya skimming kwa kutumia white cement na rangi ya maji unachanganya, na wengine wanatumia niru, na wengine ndio hiyo gypsum powder wanachanganya na maji.
- Tatu, ikishakauka tunapiga msasa.
- Nne, kufuta vumbi ukuta wako uliopiga msasa.
- Tano, Kupaka primer.
- Sita, tunapaka under coat.
- Mwisho ni kupaka rangi yako iliyokusudiwa....
NB:
Sado binder (primer) ni gundi ambayo huhitajika kupakwa baada ya kuvufuta vumbi ukuta wako....husaidia rangi kushikana na ukuta,.....rangi hua haishiki kwenye ukuta wenye vumbi ama sehemu yenye vumbi ndio maana hubanduka.....sasa kwa wale waliotumia gypsum powder ama white cement hii sado binder itawahusu mnoooo.......
Picha hii hapo chini ndio ukuta livyozoea kuuandaa...
(kwenye picha hii hapa juu maneno yasiyoonekana ndio hayo hapo chini.
UKUTA
LAZIMA UWE MSAFINA MKAVU USLEWENAVUMBI, UCHAFU, OILI AU GRI.
TUMIA KITU SAHIHI CHA KUSAFISHIA KAMA
KUNA ULAZIMA
BRASHI SKRAPA AU MSASA KUTEGEWEANA NA
KITU, MFANO MBAP CHUMA CHENYE KUTU. MDIA KWENYE PLASTA
ZIBA MATUNDU AU NYUFA. ANGALIA
KIWANGO CHA JOTO NA UNYEVU (KAMA INTUFAYIKA)
Kwa kawaida ukuta unatakiwa kua na unene wa microns (thickness) 125 kama hapo juu inavyoonekana katika mchoro wetu.....Mchoro wetu huu unaeelezea kua tumechukua karatasi ndio kama ukuta wetu......na tukapaka primer ambapo ina 20 microns, tukaongezea undercoat ambapo ni 45 microns na mwisho tukapaka coat mbili za rangi tuliyokusudia kupaka ambapo kila coat ina microns 30 . hivyo basi tunapata microns 125 ambazo ndio zinahitajika katika ukuta wako ziweko......
Katika hapa sasa, ili kulinda ukuta wako, hautakiwi na sio vizuri kupunguza ama kuzidisha......maana italeta madhara hapo siku za baadae....Nikisema kuzidisha ama kupunguza ni kwamba, baadhi ya mafundi hua wanaongeza maji mengi kupiliza kwenye rangi na rangi kua ni nyepesi zaidi nikiwa na maana inawezekana hawajui makadirio, ama wanabana matumizi ...ama mteja unaibiwa bila kujijua......
IFUATAYO NDIO MAANDALIZI SAHIHI YA UKUTA WAKO WA NYUMBA AMA OFISI:
- Kama inavyoonekana hii ni Smoothover skimming plaster, kazi yake ni kufanya skimming ya ndani na nje ya nyumba yako.....na product hii hutumika mara baada tuu ya kupiga ripu nyumba yako.....
- Baada ya kupaka utahitajika kusubiria ikauke na ndio upige msasa ukuta wako.
- Utahitajika kufuta vumbi.
- Na mwisho ndio upake rangi yako uliyokusudia.......
Smooth over inapatikana katika ujazo wa
1.5 kg
35 kg
matumizi yake ni 1 square meter = 1 kg(smooth over skimming plaster lakini pia inategemea na unene, unaoupaka ukutani)
kwa hiyo hakuna haja ya kutumia white cement, ama gypsum powder kwa ajili ya skimming na wala huhitaji prima ama under coat.....SMOOTH OVER SKIMMING PLASTER INA COVER EACH AND EVERYTHING.......
Kwa mahitaji yako ya Smoothover wasiliana nasi Homez Deco kwa simu 0713 - 920565 ama email: sylvianamoyo@yahoo.com
Karibuni sana....