Tuesday, June 26, 2012

Site Makongo......

 Homez deco tuliweka curtain poles.... vyumbani, nilipenda na vingine.....
 Nilipenda design ya makabati ya jikoni, na jiko lake ni dogo, lakini ameli design na limependeza sana... simple and neat.........top ya makabati ni marble.... hapa wengi tunachanganya sana kati ya marble na formaica,
 Ninashauri kwa jikoni, tutumie mbao, makabati na top ziwe ni marble.... maana sikuhizi kuna hizi mdf, zinazotengenezea makabati, jamani zile hazitaki maji kabisaaaaaa... sasa ukiweka jikoni na jikoni kuna maji,,,, utakuja kuniambia.....na mbao nchini kwetu tunazo, na mafundi wako, na nitajitahidi kuwaletea contact za mafundi pindi ninapopata, na kuona kazi zao nikaridhika nazo,
 Niipenda pia nyumba kwa nje... nyumba haijahamiwa bado, na ni juu na chini, yaani ni familia mbili watakaa hapa..... Nzuri sana na imependeza.....hii design ya madirisha kwa nje, naona ndio iko kwenye fashion sasa, nyumba nyingi inazo, na inavutia....
 Hii ni corridor, nilipenda hizo nguzo, natafuta contacts zao nitawapa, soon,
 Bafu....
 Toilet..... Tiles ziko nyingi na za aina tofauti, na ubora tofauti, sasa ni wewe tuu chaguo lako , na jinsi ya kuzipangilia ziweze kuendana, nzuri sana.....

Kwa haraka tuu nilivyoingia ndani ya hii nyumba nilijua tuu mwenye hii nyumba anapenda sana neutral colors......

Nashukuru sana kwa mwenye nyumba kwa kunipa ruhusa na contacts za mafundi ili sisi sote tuweze kupendezesha nyumba zetu,

Na ninaamini kwa kufanya hivi, mafundi feki watajichuja tu wenyewe.....

Namba ya fundi ni 0753-218817

NB:
Mafundi hawa, sijaonana nao, ingawa ninatafuta muda nionane nao, niendapo site, nikipendezewa na kazi zao basi ndio ninaomba contacts, kwa wenye nyumba..... Ninawashukuru wote wenye nyumba kwa ushirikiano wao.....na tuendelee na moyo huu wa upendo..........

1 comment:

  1. Hongera kwa kazi nzuri, nyumba nzuri sana "Big Up" kwa wenye nyumba. nashukuru kwa kutupatia contact za mafundi. KEEP IT UP DADA

    ReplyDelete