Tuesday, June 19, 2012

Kabati za ndani.... Mbao aina ya mninga....mbao zetu....


Jumapili ya juzi, nilikwenda site eneo la Goba....., lengo ni kwenda kupima pazia, na hii ni baada ya sisi kuweka curtain poles, kama kawaida yangu, jamani kizuri kisifie.....na chema chajiuza....
Nyumba hii ni nzuri, na nilipenda na nikamsifia sana mwenye nyumba, na ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kuniruhusu kupiga picha ili tuweze kushirikiana katika hili...
kuna msemo usemao, kizuri kula na nduguyo, na kibaya ........
Nilipenda kila kitu, yaani tiles, makabati etc.....
Nimeonelea tuangalie makabati haya na uniambie kua umeyaonaje,
kwa mtazamo wangu, fundi aliyeyatengeneza haya makabati anastahili sifa, maana haku chakachua, na finnishing yake ni nzuri. maana hata milango pia ni mninga......na fundi huyu hana usumbufu wa kazi.......
kwa mahitaji ya milango makabati wasiliana na fundi huyu
anaitwa fundi Dennis - 0715 - 888680
Ninamshukuru tena mteja wangu huyu kwa kutupa mawasiliano ya huyu fundi ili wote tusingie hasara, maana mafundi asilimia kubwa ni kula hela za watu na kiswahili kingi....


9 comments:

 1. Mazuri sana kwakweli binafsi nimeyapenda, mungu awabariki kwa kazi nzuri!!!

  ReplyDelete
 2. hyo hair do imekupendeza kweli mdada

  ReplyDelete
 3. ASANTE SANA MAMII MUNGU AKUBARIKI SANA.

  ReplyDelete
 4. Habari mdada!
  Hayo makabati ih!ni mazuri sanaaaa jamani!tunashukuru kwa kutuwekea contacts tukijaaliwa tumtafute fundi amejitahidi!na mwenye nyumba barikiwa sana na wewe Sylvia pia barikiwa na songa mbeleee!

  ReplyDelete
 5. ningependa kujua kama fundi Dennis ndiye aliyefanya kazi ya kuezeka paa kwani nami natafuta fundi wa kufanya hiyo kazi.

  ReplyDelete
 6. Nyumba nzuri sana. Mungu akubariki kwa kazi nzuri. unatufumbua macho na sisi tupendezeshe nyumba zetu

  ReplyDelete
 7. Mambo silvia nyumba nzuri sana nimependa milango na paa jiko safi sana .
  Nilikuwa natakakujua hivi unafanya kiasi gani kuweka hizo chuma nyumba nzima na mapazia ?
  Nina vyumba viwili sittingroom nataka kujua bei tafadhali asante

  ReplyDelete
 8. habari dada,tutamtafuta fundi denis makabati sio mchezo.please pia na mimi naomba bei ya kuweka pazia.namalizia nyumba yangu kibamba.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nyumba nzuri sana dada yangu
   Mimi naishi nje ya nji nafikiria kujemga nyumba yenye garage kama yako kunauwezekano nikapata ramani dada yangu nimeipenda sana = Email yangu ni jonde80@yahoo.com

   Delete