Hapa ni kabla ya sofa set kubadilishwa, nilimpelekea catalogues mteja, na akachagua design ya L shape, baada ya hapo, nimwambia kwa design ya L-shape ni lazima nije kupima sitting room yako ili tujue itachukua space kiasi gani, na ibaki kiasi gani,,, so tulikubaliana na nikaenda kwake, nikapima, akanipa advance, na nikaanza kazi, Ilichukua muda wa wiki moja na nusu kumaliza kazi.
Rome haikujengwa siku moja,...... tulianza na sofa, tutakuja na mapazia etc. Ninachoweza kusema ni kwamba usisubirie eti mpaka upate hela nyingi ndio uanze kuiremba nyumba yako, kidogo ulichokua nacho jipange na uanze, hata siku moja hela haiwi nyingi na ikakutosha........
Hizi ziuatazo ni steps za sofa jinsi tunavyotengeneza, kweli ninawaapia, sofa inayotoka hapa kwetu, hatofautiani na hizo za mamilions za huko kwa wenzetu,,,,,,, jamani mbao zipo, almost malighafi zote ziko hapa kwetu tanzania, sasa kwa nini tuhangaike? Mafundi wangu wamekua trained, na ni wasai kwenye kazi, kwenye sofa zetu, hakuna msumari utakaouona, hakuna nyuzi utakayoiona, etc,
Hapa mnapopaona ni mahali ambapo kazi hufanyika ya sofa, nahii ni kwasababu bado tunajikongoja na mitaji....so kwa kuanzia ndio tuko hapa, ila mungu akipenda, tutakua na warehouse kuubwa,, itakayokidhi biashara yetu,so tuwee pamoja katika hili........
Fundi akipima kitambaa cha sofa...... ni quality, tujitahidi kuangalia quality na sio quantity....
Hii sofa kwa chini, kama mnavyoona ni kua hakuna makorokoro ama uchafu, maana hua ndio unao attract panya.....
Hukuti uchafu hata ukijafumua,,,,,, kila kitu kiko wazi, actually hii ni sofa ingine, nilikua ninawaonyesha tuuu usafi wake.....kabla hatujafunika kitambaaa....
fundi akifunika sofa kitambaaaaaa anapiga staplers, hizi ni za sofa,, then anashona......
hapa akifunga miguu ya sofa.....
unaona usafi wa sofa... sio kama sehemu fulani hivi, jamani sofa nje inaridhisha ila huko ndani duh.... panya ndio wanakua familia.....
Kitambaa kikifunikwa......
Hii ni sindano special kwa ajili ya kushonea sofas.... kweli hazipatikani hua ninaagiza nje ya nchi...... so hua ninakua nazo makini sana ofisini......
fundi akifanya mambo... anashona sofa, hakuna uzi unaooneka hapo...... mteja mwenyewe amenikubali,,,,, hahahhaha...
kitambaa kikifunikwa.... chini ya sofa.......
Almost...... tunamaliza.... stay tuned........