Monday, September 13, 2010

Homez Deco work (this time was at kigamboni area, and we were decorating baby's room theme was unisex) Enjoy)

Kazi hii ilifanyika wiki moja iliyopita, na nashukuru sana sana kwa ushirikiano na mteja wangu huyu, kwani kazi ilifanyika vizuri na tulimaliza salama. Ilikuwa ni ku decorate chumba cha mtoto wake anayekuja, (hajazaliwa) haya ni baadhi ya maandalizi. Nili discuss nae rangi ya kupaka ukutani, kwani yeye hakutaka kujua jinsia ya mtoto, so theme ya decoration ya chumba hicho ilikua ni neutral colors. Borders za wall paper zilikua ni za kwake. Tulipaka rangi chumba, tuka bandika borders za wall papers kama inavyoonekana, na tuka repair kochi ambalo atakua anatumia eidha kwa wageni watakoingia ama kunyonyeshea mtoto. Mwisho tuka tundika picha ukutani za winnie the pooh. Kazi hii ilifanyika kwa awamu, tatu:

1. tulipaka rangi

2. tulibandika borders za wall papers

3. tuka hang picha ukutani.

Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru mteja wangu huyu kwa kunielewa na kuniruhusu kupiga picha kwa ajili ya kumbukumbu na kushare na watanzania wenzetu, kazi za homez deco. Homez Deco inapenda kuwafahamisha kua hua tunahifadhi privace za watu, kwa kuto toa details zozote za mteja, zaidi tuu ya eneo la kazi ilipofanyika. 

Nakutakia kila la kheri na maandalizi mema ya mtoto wetu, mungu awe nawe all the way.

NB: nawaombeni mniwie radhi wadau tarehe inayoonekana hapo kwenye hizi picha si ya kweli, kidogo nilipitiwa ku edit tarehe.

It was so fun enjoy the pictures.







Hapa ni baada ya kubandika picha ukutani yaani hatua za mwisho, na hilo ndilo kochi lenyewe.
Wall paper border inavyoonekana kwa karibu.

Kabla ya kubandika picha ukutani ambayo ndio ilikuwa ni hatua ya mwisho.

3 comments:

  1. vipi mama zehome, mimi nilikuwa naomba tuwekee bei zako kwa mfano ukitaka kunipangia my living room ni kiasi gani, je chumba changu ni kiasi gani, garden ni shi ngapi tupe bei tusiogope ili tukuite utusaidie. asant

    ReplyDelete
  2. hi, asante sana kwa wazo lako, unajua ninashindwa kuweka bei, maana nyumba, ama vyumba vinatofautiana, kwa hiyo ni mpaka nije nione ndio nitoe bei. Usiogope kua labda nitakua na bei ghali.

    ReplyDelete
  3. Good work mama homedecoz! hongera sana!

    ReplyDelete