Tuesday, September 14, 2010

Her garden ( the same house we decorate baby's room)

Ukijiamini unaweza, garden hii ameitengeneza yeye mwenyewe, na imependeza sana, nilimuomba nipige picha ili nije kushare nanyi wadau wetu. Hongera sana sana kwa garden nzuri.

Ninachoweza kusema ni kua ukiamua unaweza, ila kwanza upende, ndio uamue, kwenye upande wa garden, ni gharama kiasi, kuanzia kuanza mpaka ku  maintane, na upate kijana mzuri ambaye atakuwa anafanya jinsi utakavyo. 

Sio kila maua ni ya kupanda chini, na sio kila ua linaweza kustahimili joto ama badiri, na udongo pia una mata, bila kusahau mbolea, unaweza ukanunua maua, na kupanda lakini yakafa na ukamlaumu muuzaji, hapana, tafuta ushauri kwa wenye uzoefu na gardening, na watakushauri, na hata hao hao wauzaji weengi wao hutoa ushauri,

Wengi tunasema kua mimi nyumba ya kupanga siwezi kuipendezesha. Sawa , haya mungu kakubariki una nyumba yako, huipendezeshi, wakulaumiwa ni nani? Kila kitu kinakwenda na budget, wengi wetu tunafanya vitu bila budget, na kwa ushauri wakati unajenga ndio wakati mzuri sana wa kutengeneza garden pia ili vyote viende sambamba. 

Hii ni nyumba ya mtanzania mwenzetu na ameweza kufanya hivi, na namshukuru sana sana kwa kuniruhusu kupiga picha. Na naomba kuwataarifu ndugu wadau kua kwa ajili ya usalama, sikupiga picha nyumba, na sisi homez deco, tuna mipaka yetu kwenye kutoa details za decorations, hivyo basi msiogope kututumia picha za nyumba zenu ili tu share mawazo na wenzetu. KIZURI KULA NA MWENZIO KIBAYA MTUPIE ...............
Garden kwa mbele inavyoonekana, nimependa hizo sanamu za bata, it's all about ubunifu.

Nyuma ya nyumba, jamani jamani, nyumba nyingi huwa wanajali kupendezesha mbele ya nyumba, nyuma ya nyumba hua panaachwa ovyo na kuchafu, yaani ndio pa kuficha uchafu. Jamani dhana hizo ni za kizamani nani uchafu. Mbele ya nyumba na nyuma ya nyumba kote panatakiwa kuwe kusafi.
Banda la mbwa, lilinivutia, jamani wanyama pia wana haki zao,na wanahitaji usafi kama sisi binadamu, wanakulinda, kwa nini usiwaweke sehemu ya usafi? Utakuta banda la mbwa bovu, mbwa wana nuka, vinyesi vyao ndio usiseme etc. lol,, banda hili lilinifurahisha sana. TENGENEZA BANDA LA MBWA WAKO, SI NI MLINZI WAKO? KWANINI USIMJALI, MSHAHARA WA MBWA NI MALAZI, CHAKULA, NA MATIBABU.
Entertainment hazikuwa nyuma kwa kweli, it was so lovely,,,, taa za garden ziko garden nzima. UKIAMUA UNAWEZA. KUNA USEMI USEMAO UTAVUNA ULICHOPANDA, KAMA UMEPANDA KUVAAA NA MAZINGIRA YA UNAPOKAA UMEYAPA MGONGO, UTAVUNA MAGONJWA, NA KAMA UMEPANDA KUWEKA MAZINGIRA YA UNAKOKAA NA YANAYOKUZUNGUKA MASAFI, UTAVUNA ................

1 comment:

  1. wow!...Lovely garden jamani!...thanks for sharing with us maana unatujuza haswaaa

    ReplyDelete