Nakutakia kila la kheri sis,
Wednesday, November 23, 2011
Colorfull Roof - Gypsum ceiling board
Unajua kua gypusm unaweza kupigwa rangi? Sasa hii inahitaji utaalam zaidi, maana ikipigwa vibaya ama kwa wasiwasi, basi utaichukiaje kama sio kuitoa yote, designs ziko nyingi sana,,,maana sie tumezoea tuuuu roofing ina plain,
Make a statement into your roof.
Bado ninafanya research ya kutafuta mafundi ambao sio wabaishaji na wanaojua kazi zao, once nikiwapata nitawajulishaaaa.........
Shear butter products & Vaseline products helped my rough skin...
Hapa kitu bila make up......
hii musk ni rahisi sana kuitumia, na sio ya kubandua, ikikauka unaosha na maji ya uvugu vugu.......
Vaseline cocoa butter hua haitoki kwenye pochi yangu,, ukiangalia mikono yangu na miguu yangu na magoti yangu sina sugu hataaaaaaaaaaaaa, na ina flavour ya chocolate. yaani tahadhari weka mbali na watoto........mkorogo sio lazima, ukitumia body products ambazo ni orginal, zinafanya kazi...... maana tuangalie na jua hili na hii mikorogo, si unaiva jamaniiiiii) I love every part of my body,,,
Kama zinavyoonekana hizi products za shear butter, hapo kuna shear butter scrub, shear butter lotion, na shear butter. Plus vaseline cocoa butter deep conditioning. Bila kusahau chocolate musk.
Hizi products kwa kweli zimenisaidia sana sana, nilivyokua mjamzito nilikua ninapaka sana sana hiyo vaseline deep conditioning, tumboni pamoja vaseline(mafuta ya mgando) huwezi amini ila ndio hivyo sijatokewa na strech mark hata moja.
Kwa atakae hitaji zinapatika hapa homez deco, just give me a call;
Kwa wa mikoani tunazisafirisha pia.
NB: Ziko pia za watu wanaosumbuliwa na chunusi, scrub na mafuta yake. (MAFUTA HAYA HAYAJACHAKACHULIWA NI ORIGNAL, NA TOKEA NIMEANZA KUYAUZA SIJAWAHI KUPATA MALALAMIKO YA KUA YAMEMUHARIBU MTU AMA NINI, NA HAYACHUBUI, NI NGOZI YAKO INAKUA SMOOTH NA MOISTURE).
Karibuni katika ulimwengu wa kutumia products orignal.
Emagine hizi ndio city garden zetu za Tanzania (sasa umepiga picha)
Mmmhh, sasa hapa ndio mnazi mmoja, ile city garden.......
Haya maua hapa kwetu yapo, yaani ni kiasi tu cha kuamua na kubadilika, sio kila siku maua ni yale yale,,,,, design ni zile zile......... haahhahaha
Huyu ni Jossyanne (USA)
Inawezekana hapa kwetu kua na city garden nzuri.
Tuesday, November 22, 2011
Program Mpya
Ninayo furahaa kuanzisha program hii mpya, kwa kua nimekua nikitoa ushauri wa nyumba zetu, garden etc. Sasa basi, naomba kwa wale wote ambao ushauri huu umewasaidia na wameweza kuufanyia kazi wao wenyewe, naomba wanitumie picha za sehemu walizozifanyia decorations, yoyote ile iwe kubwa, ndogo zote ni decorations, haijalishi ni chumba gani ama mahala gani.
Hii itatusaidia wote, kwani tusiwe waoga wa ku share mawazo yetu, wote tunajifunza na kama patahitaji ushauri wangu basi nitachangia, free off charge.
From Sylvia a.k.a mama Jaydan
Curtain Poles - Nyumba ya kupangishwa
Wengi wetu tumejaaliwa kua na nyumba hapa mjini na tumeamua kuzifanyia biashara, ya kuzipangisha, ila sasa, wengine tuna kua wavivu kuzifanyia ukarabati, na hata ukifanywa basi ni wa juu juu, utakuta nyumba inachakaa kabla ya wakati,
sasa basi, nina wazo kwa hawa wenye nyumba, unajua kutoboa toboa ukuta kunachangia kuharibika kwa nyumba na hatimae kuleta ufa, hebu fikiria kila mpangaji anaeingia aweke curtain poles zake, hiyo nyumba itadumu kweliiii.
Hivyo basi mwenye nyumba una mamlaka yote ya uchaguzi wa nini kifanyike, amua kuweka curtain poles za design unayoipenda, hii itasaidia kufanya nyumba yako idumu. (ukiweka ac kabisa pia ni vizuri zaidi, yaani vile vitu vya ukutani we viweke kabisaaaa, ingawa picha za ukutani wao wapangaji wataweka, ila utaawaambia kabisa nini wafanye ukuta usiharibike)
asilimia kubwa kwenye issue za delivery hua ninakuwapo ili kuhakikisha kila kitu kiko sawa, na mteja anaridhika.
Pillow Protector
Hivi mnajua kua unaweza kuulinda mto wako usichafuke na mafuta na majasho? Hizi ni pillow protector, yaani huna haja tena ya kununua mito mara kwa mara, unachofanya ni kuuvalisha kwanza mto wako hii protector, then uvalishe pillow case.
Soon zitapatikana Homez Deco.
Subscribe to:
Posts (Atom)




