Kumekua na tatizo la uchaguzi wa rangi za nje ya nyumba zetu.......kwa mfano...wengine wanapaka rangi ambazo ni bright sana nje...kama pink, njano etc......hilo ni kosa......nje kunahitajika rangi zilizo poa......
Kwa hapa tanzania hatuna utaratibu wa kuangalia majirani zako wamepaka rangi gani ili uendeleze utaratibu huoo.....sasa unaweza ukakuta wewe nyumba yako ndio ina bright color...peke yako.....hiiii sio nzuri.....
Watu tunajenga.....lakini hatujui rangi ipi inaendana na ipi.....na katika uchaguzi wa rangi za nje....anza na rangi ya bati uliloweka ama kugae.....halafu madirisha, milango, na umalizie ukuta......na kwa uzuri zaidi......mlango uwe ndio focal point yako....maana mlango ndio unakukaribisha ndani.......sasa unahitajika uwe ni mzuri......
Muongozo wa rangi za nje.....na kumbuka rangi za nje ni weather guard, ama wall guard, ama weather shield.....hizi ndio rangi za nje...zinazostahimili hali ya hewa yoyote ile.........(SILK AMA WASH N WARE NI ZA NDANI TUUUUUUUU.....tunachanganya sana hapa)
Picha hizi mbili hapa juu zinatuonesha ni jinsi gani ya kuchanganya rangi nje ya nyumba zetu.......katika rangi hizi tatu.....waweza chagua rangi moja ikawa ni ya bati. rangi ingine ikawa niya milango na madirisha....na rangi ingine ikawa ni ya ukuta wa nje wa nyumba na fensi.....ni wewe tuuu uchague ni rangi ipi uipendayo........
Rangi hizi ni za bafuni ama jikoni......hupendeza zaidi.......
Ona rangi zilivyotulia...............
NB:
kwa wale wanaokaa zile sehemu zenye vumbi....msipake rangi ambayo ni angaavu nikiwa nina maana cream. white etc.....paka rangi ambayo iko dark na hii itakusaidia, nyumba kutokuonesha uchafu kwa kipindi kirefu......
Sehemu yako unayoishi kuna vumbi bara bara ya vumbi...tena lile kama la brown....halafu wewe umepaka rangi white ama cream.........jibu unalo........
Rangi hizi zote zinapatikana Homez Deco.......
Monday, May 27, 2013
Muendelezo wa matayarisho ya ukuta na kupaka rangi......nyumba ya kinondoni.......
Picha hizo mbili juu nikionesha jinsi gani vumbi linabaki ukutani baada ya kupiga msasa mlaini kuondoa rangi iliyochakaa.....na hapo ni baada ya kulifuta kwa ufagio zile za ndani.....lakini bado vumbi liko......sasa hebu fikiria, na vumbi hili lililobaki halafu unapaka rangi juu yake....hii rangi kamwe haitaweza kukaa kwa muda unaotakikana, maana vumbi ni sumu ya rangi...
Picha hizi mbili za juu ni baada ya kupaka sado binder ni gundi ambayo husaidia vumbi lisikutane na rangi na hufanya rangi kudumu kwa muda mrefu bila madhara ya kubanduka ama kuchakaaa....gundi ziko za aina mbili kuna sado binder ama bonding liquid ambapo zote zinafanya kazi sawa ila hii bonding liquid ina uwez zaidi...sasa ni mfuko wako tuuu.......hapo nikiwa nimeridhika na kazi ya mafundi na ndio nimewaruhusu kupaka hii gundi tayari sasa kwa kupaka rangi.....ya dulux katika sehemu zilizokusudiwa.....
Labels:
Colour
Thursday, May 23, 2013
Kifuatacho......(80% ni maandalizi 20% kupaka rangi)
Homez Deco tulipata kazi ya kupiga rangi nyumba iliyoko maeneo ya kinondoni......Rangi ya nyumba nzima ilikua ni cream......
Hapa ni nyumba ikipigwa msasa mlaini, nikiwa nina maana ya tunafanya maandalizi ya ukuta. Ukipiga msasa mlaini ni unaondoa rangi iliyochoka na uchakavu wowote uliojificha......Hatua hii mara nyingi mafundi hua wanaikwepa na kulipua kazi na matokeo yake kazi inakua chafu.......(20% maandalizi ya ukuta 80% kupaka rangi)
Mafundi wakiendelea na kazi ya msasa kwa ajili ya matayarisho......rangi tulipiga sitting room, dinning, na korido.....ilituchukua siku mbili kumaliza kazi...mafundi walikua ni 3. Kutayarisha ukuta ilituchukua siku moja nanusu.......na tulifanya kazi kuanzia asubuhi mpaka saa tatu usiku siku ya kwanza. na siku ya pili tulimaliza saa moja jioni.....
Hili ni vumbi la rangi iliyochoka baada ya kupiga msasa mlaini nyumba hii.......
Tutaende kuleta picha zaidi......
Labels:
Colour
Wednesday, May 22, 2013
Tuesday, May 21, 2013
Rangi bora na imara kwenye nyumba/ofisi yako......
Rangi ni nini?
Rangi ni koti ya kukinga ama kulinda..(it's a protective coating)
Rangi imetengenezwa kutokana na mchanganyiko wa malighafi., na inaweza kupakwa kwa kutumia brashi, rola au kwa kupuliza, na itakapo kauka inakamata ama kushikana vizuri na sehemu uliyoipakana hivyo kupendezesha na kukinga sehemu hiyo.......
Sasa basi rangi sio tuu hupendezesha kuta zetu bali hata kukinga.......
Ukiangalia mchoro wetu hapo chini utaona ni jinsi gani rangi inakua na mchanganyiko mpaka kuitwa rangi.....
Sasa kazi iko hapa kwenye picha ya chini....Tofauti ya utengenezwaji wa rangi......
Katika picha ya kwanza huu ndio utengenezwaji unaostahili wa rangi, na ndipo unapopata rangi imara na yenye mvuto na kuvutia yaani inavigezo vyote vinavyostahili......
Rangi ni koti ya kukinga ama kulinda..(it's a protective coating)
Rangi imetengenezwa kutokana na mchanganyiko wa malighafi., na inaweza kupakwa kwa kutumia brashi, rola au kwa kupuliza, na itakapo kauka inakamata ama kushikana vizuri na sehemu uliyoipakana hivyo kupendezesha na kukinga sehemu hiyo.......
Sasa basi rangi sio tuu hupendezesha kuta zetu bali hata kukinga.......
Ukiangalia mchoro wetu hapo chini utaona ni jinsi gani rangi inakua na mchanganyiko mpaka kuitwa rangi.....
- Malighafi
- viendelezi
- Gundi
- Viyeyushi
- Viongezo
Sasa kazi iko hapa kwenye picha ya chini....Tofauti ya utengenezwaji wa rangi......
Katika picha ya kwanza huu ndio utengenezwaji unaostahili wa rangi, na ndipo unapopata rangi imara na yenye mvuto na kuvutia yaani inavigezo vyote vinavyostahili......
Labels:
Colour
Thursday, May 16, 2013
Unafanyaje vibaraza vya nyumba yako maji yanapotuama na kuweka ukungu?
Tumekua tukisumbuka sana na tatizo la vibaraza vya mbele ya nyumba zetu, kuharibiwa na mvua, ama hali ya unyevu unyevu kipindi cha baridi.....kutokana na maji kutuama kutoka kwenye paa na kuja kwenye vibaraza vya nyumba zetu...
Na mara nyingi tumekua tukipata suluhisho la muda ambalo ni mvua zinapomalizika tunapaka rangi.
Sasa ningependa kuwajulisha kua suluhisho tunalo katika tatizo hili....Katika kampuni ya
Dulux wametuletea suluhisho ambalo ni product inaitwa RAINSHIELD.
Dulux wametuletea suluhisho ambalo ni product inaitwa RAINSHIELD.
Rainshield ni aina ya rangi ambayo, hairuhusu maji kupenya, nikiwa nina maana kua yenyewe inaruhusu maji kuteleza na sio kutuama (water resistant, crack resistant and it's long lasting acrylic formulation). Product hii husaidia sana katika sehemu za nje kama vibaraza......
Inapatikana katika rangi nyeupe na kijivu isiyokoza....
Lita 1 inatumika 2-3 square meters kutegemea na ukuta ulivyotayarishwa.
Zinapatikana katika ujazo wa lita 5.
Wasiliana nasi......0713 - 920565. karibu.
Labels:
Exterior
Subscribe to:
Posts (Atom)


