Tuesday, May 14, 2013

Suluhisho la kwenye ukuta unaosumbuliwa na fangasi, unyevu unyevu, etc.....




 Kuna kuta ambazo zinasumbuliwa sana na fangasi ama unyevu unyevu, sehemu hizi ni kwenye njia za mabomba, sehemu uliyoweka air condition, nje sehemu ya garden inayozunguka nyumba etc.....

Huu ndio muonekano wa tatizo la fangasi ama maji yavyoharibu ukuta......



Kwa mtazamo wa hizi picha utakubaliana nami kua hili tatizo lipo katika baadhi ya nyumba zetu.....matatizo haya ni kua yanaletwa na  maji ya ardhini kupanda juuu etc.....jamani wakati wa kuanza ujenzi, nikiwa namaana msingi ukisha chimbwa ni muhimu kuweka pvc plastics...... Hizi ni plastics zinazoweka layer ya maji ama unyevu unyevu kugusana na tofali...na hivyo kufanya nyumba kua imara.

Sasa kuna baadhi ya nyumba hua hawaweki....ama kwa kutokujua, ama kwa kukwepa gharama.
Kuna msemo usemao KUNA MAKOSA YANAYOSABABISHWA NA FUNDI MJENZI....HIVYO FUNDI RANGI HAWEZI KUYAMALIZA BALI HUYAGHAIRISHA KWA MUDA NA SI KUYAMALIZA......

Kwa mfano hili swala la kuta kuwa na maji maji, ama unyevu unyevu.....asilimia kubwa ni kwamba hazikuwekwa pvc wakati zinajengwa na hili ni kosa la fundi mjenzi....sasa akija fundi rangi hato tatua tatizo bali atalighairisha kwa kutumia products za kuzuia Unyevu unyevu ama fangasi ......na baada ya miaka kadhaa litarudi tena.....

Tatizo lingine ni kutokana na rangi zenyewe. kuna baadhi ya rangi hua zinaleta fangasi kwenye kuta za nyumba zetu....hili nitakuja kuliezea pia......


 Hizi ni kuta kwa nje
 Hapo juu ni ukuta kwa ndani.....
Ukuta kwa nje.....



Product hii ya DAMP SHIELD. ni product mahususi kwa matatizo kama haya.......

Kwanza kabla ya kutumia hakikisha unatayarisha ukuta wako vizuri na kwa kutibu tatizo...mfano, kama mabomba yanavuja basi hakikisha umelitengeneza kwanza ndio utumie hii damp shield..... halafu suribia ikauke vizuri, piga msasa,  futa vumbi na ndio upake rangi yako uliyokusudia......

Product hii inasaidia maji kuto haribu ukuta wako kwa 50%.......na hali hizo ambazo nimeziongelea hapo juu.


Karibuni sana Homez Deco maana mkombozi amepatikana.......

Maelezo....
  • Inakauka baada ya masaa 2 baada ya kuipaka mahali husika.
  • kuirudia kuipaka ni baada ya masaa 4.
  • 12 square meter katika lita moja.....upakaji wake ukutani.
  • Rangi yake ni nyeupe...
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa email: sylvianamoyo@yahoo.com  Tel: 0713 - 920-565

Monday, May 13, 2013

Matayarisho/Maandalizi sahihi ya ukuta kabla ya kupaka rangi.....( iwe ni kuta za ofisini ama nyumba zetu).......


Somo letu linaendea........na leo tunaangalia upande wa matayarisho ya ukuta kabla ya kupaka rangi......

Kuna msemo usemao: DAIMA SAFISHA NA PAKA RANGI...... NA SIO PAKA RANGI NA USAFISHE.

Sasa sisi tunageuza na tunatumia: PAKA RANGI NA USAFISHE.....

Msemo huu Daima safisha na paka rangi maana yake ni kua, katika matayarisho ya ukuta kwa ajili ya kupaka rangi, tunahitajika kutumia 80% katika kutayarisha ukuta, na 20% ndio kupaka rangi......

Ila sisi ama wengi wetu tumekua tukitumia 20% Kutayarisha ukuta na 80% ndio kupaka rangi....kitu ambacho ni makosa makubwa mno....na hii ni kutokana  na ama fundi hajui, ama mwenye nyumba ana haraka ya nyumba kuisha, ama mwenye nyumba anakwepa gharama, ama fundi amedanganya na kupotea na hela....na sababu nyingi nyingi......

Hawa ni baadhi ya maadui wa rangi katika ile 80% ya kuandaa ukuta:


  • Kabla ya kupaka rangi yoyote ile kwenye ukuta, hakikisha sehemu hiyo iko katika hali ya kuridhisha, nikiwa na maana kua kuna maadui wa rangi ambao ni vumbi (kuta zenye vumbi mfano wa chokaa...kama gypsum powder ni mfano wa chokaa), oil, grisi, kutu, mchanganyiko wa kemikali, unyevu, na fangasi ama vimelea vya wadudu.
  • 80% ya malalamiko ya kuhusu rangi yanatokana na maandalizi duni ama yasiyo sahihi ya ukuta, kwenye usafi, kuziba matundu, kuondoa rangi iliyobanduka na isiyokamata vizuri, kutoondolewa kwa ukungu na fangasi, kutokusafisha vizuri kuta zenye chokaa, ama kutondoa rangi ya zamani na varnish etc.....



Hapo chini tunaoneshwa kua hayo ndio maandalizi ya ukuta ambayo tumeyazoea na tumekua tukiendelea nayo. 

  • Njia ya kwanza tuliyoizoea baada ya kujenga nyumba hua tunapiga ripu.(ripu ni mchanganyiko cement na mchanga).
  • Pili, tunafanya skimming kwa kutumia white cement na rangi ya maji unachanganya, na wengine wanatumia niru, na wengine ndio hiyo gypsum powder wanachanganya na maji.
  • Tatu, ikishakauka tunapiga msasa.
  • Nne, kufuta vumbi ukuta wako uliopiga msasa.
  • Tano, Kupaka primer.
  • Sita, tunapaka under coat.
  • Mwisho ni kupaka rangi yako iliyokusudiwa....
NB:
Sado binder (primer) ni gundi ambayo huhitajika kupakwa baada ya kuvufuta vumbi ukuta wako....husaidia rangi kushikana na ukuta,.....rangi hua haishiki kwenye ukuta wenye vumbi ama sehemu yenye vumbi ndio maana hubanduka.....sasa kwa wale waliotumia gypsum powder ama white cement hii sado binder itawahusu mnoooo.......

Picha hii hapo chini ndio ukuta livyozoea kuuandaa...


(kwenye picha hii hapa juu maneno yasiyoonekana ndio hayo hapo chini.

UKUTA LAZIMA UWE MSAFINA MKAVU USLEWENAVUMBI, UCHAFU, OILI AU GRI.

TUMIA KITU SAHIHI CHA KUSAFISHIA KAMA KUNA ULAZIMA

BRASHI SKRAPA AU MSASA KUTEGEWEANA NA KITU, MFANO MBAP CHUMA CHENYE KUTU. MDIA KWENYE PLASTA

ZIBA MATUNDU AU NYUFA. ANGALIA KIWANGO CHA JOTO NA UNYEVU (KAMA INTUFAYIKA)







Kwa kawaida ukuta unatakiwa kua na unene wa microns (thickness) 125 kama hapo juu inavyoonekana katika mchoro wetu.....Mchoro wetu huu unaeelezea kua tumechukua karatasi ndio kama ukuta wetu......na tukapaka primer ambapo ina 20 microns, tukaongezea undercoat ambapo ni 45 microns na mwisho tukapaka coat mbili za rangi tuliyokusudia kupaka ambapo kila coat ina microns 30 . hivyo basi tunapata microns 125 ambazo ndio zinahitajika katika ukuta wako ziweko......

Katika hapa sasa, ili kulinda ukuta wako, hautakiwi na sio vizuri kupunguza ama kuzidisha......maana italeta madhara hapo siku za baadae....Nikisema kuzidisha ama kupunguza ni kwamba, baadhi ya mafundi hua wanaongeza maji mengi kupiliza kwenye rangi na rangi kua ni nyepesi zaidi nikiwa na maana inawezekana hawajui makadirio, ama wanabana matumizi ...ama mteja unaibiwa bila kujijua......


IFUATAYO NDIO MAANDALIZI SAHIHI YA UKUTA WAKO WA NYUMBA AMA OFISI:
  • Kama inavyoonekana hii ni Smoothover skimming plaster, kazi yake ni kufanya skimming ya ndani na nje ya nyumba yako.....na product hii hutumika mara baada tuu ya kupiga ripu nyumba yako..... 
  • Baada ya kupaka utahitajika kusubiria ikauke na ndio upige msasa ukuta wako.
  • Utahitajika kufuta vumbi.
  • Na mwisho ndio upake rangi yako uliyokusudia.......
Smooth over inapatikana katika ujazo wa
 1.5 kg
35 kg

matumizi yake ni 1 square meter = 1 kg(smooth over skimming plaster lakini pia inategemea na unene,  unaoupaka ukutani)

kwa hiyo hakuna haja ya kutumia white cement, ama gypsum powder kwa ajili ya skimming na wala huhitaji prima ama under coat.....SMOOTH OVER SKIMMING PLASTER INA COVER EACH AND EVERYTHING.......

Kwa mahitaji yako ya Smoothover wasiliana nasi Homez Deco kwa simu 0713 - 920565 ama email: sylvianamoyo@yahoo.com

Karibuni sana....






Wednesday, May 8, 2013

Curtain Designs.....(Karibu utoe oda na ushonewe)


 Hizi ni baadhi ya designs ya mapazia, ambayo yanahitaji curtain box ndio ziweze kukaaa vizuri.....

Interior Blogs and Websites.....


Napenda kuchukua fursa hii kushukuru kwa wale wote wenye blogs za interior decorations, za hapa kwetu, kwani naona sasa tumeanza kujitokeza na lengo ni katika kusaidiana katika kazi hii ya designing.....

Naendelea kukaribisha wale wote walio na blogs zao ama website wanitumie links zao niweze kuziweka kwenye blog hii yetu....na tuweze kuona kazi zenu.

Hivyo basi  kuanzia sasa, Homez Deco inaweka link za blogs na websites mbali mbali, za hapa kwetu Tanzania na za nje ya nchi, ili kuweza kujua wenzetu ni nini wanafanya na wanaendeleaje.......

 Tunaomba ututumie nasi tutaiweka ili iweze kutunufaisha wote.......

Tunakaribisha maoni, ushauri etc...nasi tutaufanyia kazi....

Asanteni,

Sylvia Namoyo
Director.


NB:
Somo la maandalizi ya ukuta litaendelea siku ya jumatatu tarehe 13/5/2013, Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.....

Thursday, May 2, 2013

SALE SALE SALE.........WALLPAPER FOR SALE......PER ROLLER IT'S TSHS. 50,000/-

 Kila rola ina urefu wa mita 10 na upana wa sentimeter 53 ..... Kwa mahitaji ya wallpaper wasiliana nasi kwa namba 0713 - 920565...ama emali: sylvianamoyo@yahoo.com  Wahi sasa......

Matumizi ya Gypsum powder kwenye ukuta wa nyumba zetu ama ofisi zetu.....



Nadhani wengi wetu tunaifahamu gypsum powder. Leo nimeonelea kuiongelea kutokana na kwamba hua inatumika vibaya, mahala pasipohitajika kutumika......Katika pita pita yangu kwenye nyumba, wakati nafanya kazi, kupima mapazia, kutoa ushauri etc.......nyumba .nyingi  mafundi wanatumia gypsum powder katika kuandaa ukuta kwa matayarisho ya kupaka rangi......

Jamani hili ni kosa kubwa mno.....na wengi wetu tunatumia mpaka kwenye ukuta wa nje ambapo huko sasa ndio hakufai kabisaaaa, maana haihimili hali ya hewa......na matokeo yake nikua rangi inabanduka, ama kuweka cracks kua huu unga unaachiana na ukuta.......Nimejaribu kufanya research ya kwanini watu wanatumia huu unga wa gypsum ukutani......kutoka kwa mafundi wenyewe, na wateja......na jibu nililolipata ni kwamba.....wengi wanakimbia gharama za kununua products sahihi za ukutani, wengine hawajui...etc.....Yaani bora asiyefahamu.....lakini huyu anaekimbia gharama...ndio siwaelewagi kabisaaa....maana kama unaweza kujenga nyumba mpaka ikasimama nani nyumba nzuri....iwe ndogo ama kubwa zote ni nyumba.....kwanini unaharibu upande wa finnishing.... kwa kutaka kuepuka gharama?....yaani ni bora ujenge kwa awamu kuliko kufanya upesi na kuharibu.....jamani hiyo nyumba si ni yako unataka kuhamia? ama hataka kama unataka kupangisha? Kwanini usiitengeneze vizuri......Naomba tubadilike katika hili...na utaona nyumba yako ukipaka rangi inakaa muda mrefu na kudumu.......

Metal Beds......Karibu utoe order na ukipate ndani ya siku 7.....wasiliana nasi kwa email: sylvianamoyo@yahoo.com Tel: 0713 - 920565 (vitanda vyote ni bila magodoro)


 Price tshs. 350,000/-
 Price tshs. 350,000/-
 Price tshs. 350,000/-