Friday, May 11, 2012

Maandalizi ya Website yakiendelea......

Mambo ya mtandao, sasa hatutembei na files za catalogue, ni kitu cha ipad hapa......Thanks Lord naendelea kupiga hatua taratibu kwa juhudi zangu mwenyewe......I love my self




Huyu ndie aliyewezesha website yangu mpaka iko hewani, na yeye ndie atakua akihusika na maswala yote ya website, isiende kombo.........ni web designer......sio kwamba ninamsifu, ila katika kutafuta web designer wa kunifanyia kazi yangu hii, nikakutana nae, tena nilimpata kwa mteja wangu mmoja ndio akaniunganisha nae. Anaitwa Kaduma huyu web designer wangu.

Yaani this guy, anajua anachokifanya, na anajua kazi yake, hana haraka haraka ya kufanya kazi bora liende tuu... ana anafanya kazi kulingana na wewe unachokitaka na anakupa ushauri, na hakatai mawazo. Na imetuchukua kama miezi 2-3 hivi, maana tulikua tukiiandaa na kupumzika na kutafuta hela... hhahha si unajua tena tunajikongoja... hahaa.... lakini hakuchoka wala kukasirika. etc..... kwa ufupi he is a great guy of all.......atakaemhitaji contacts zake ziko hapo juu kwenye tangazo.......then utakuja kuniambia.....


hahahaha, imetokea wote leo tumevaa blue..... hhahahaha.... ila tumependeza ehehehhe hahahaah

Bado tunaendelea na kuijazia sehemu ambazo zinahitajikaa, maana ninataka iwe ni directory ya Interior decorations, etc...... sasa jamani si kazi ndogo hii naomba tuwe tunavumiliana pale ambapo ninachelewa ku post, ingawa sitakua ninakaa muda sana..... na hii ni kwa ajili yenu ndugu watanzania wenzangu, ninataka ifike mahala sasa, unahitaji kitu basi wewe unaingia kwenye website na blog yangu na kutafuta kampuni unazozitaka, na kwenda kwenye website zao.... na hii naona itasaidia sana sana, wawe wana update website zao mara kwa mara kwa kuweka vitu vipya walivyoagiza.

Natumai kwa kufanya hivi jamani tutakua tunaokoa muda, maana kwa sasa unahitaji kitu nahujui wapi pa kukipata, mwishowe hela unakula.......

Kwa kusema ukweli hii kazi ni ngumu, maana ni mpaka makampuni yaelewe na wanikubalie, sasa sio kazi ya leo ama kesho kukubaliwa, ila ninaamini nikiianza mapema itakua rahisi kwetu wote sote...

Ninajaribu kuwapa mawazo yangu ya nini nafikiria kukifanya na wapi tunakwenda, ninahitaji ushirikiano wenu wa hali na mali, kwa kunivumilia ili tufikie malengo.....ifike pahala na sie tunaweza kununua vitu online kwenye makampuni yetu ya nchi yetu hii.......najua inawezekana na ndio maana ninataka kuifanyia kazi......

Jamani kuna watu wamekaa tuu na kutafuta mawazo ya watu na wao waige ili watoke....... naomba kusema kua sitoogopa, wala kumuonea mtu huruma, nikiona mtu kaiga haya mawazo yangu na kuyafanyia kazi........yaani nitamuaibisha mpaka atashangaaaa, na nadhani kwa hili ndugu wadau tutasadiana na watu wa namna hiiiii.

Kwa haya mafupi napenda kuwashukuru wote kwa kuendelea kua nami na mnaendelea kua nami maana bila ninyi nisingefika hapa nilipo na kujivunia kazi yangu......naendelea kuomba mawazo yenu juu ya hi website yetu, kama kuna kitu tuongeze, tupunguze, etc.... nitayapokea na kuyafanyia kazi....

Nawatakia weekend njema.......



Thursday, May 10, 2012

Homez Deco Website........(Suprise......)


Napenda kuchukua nafasi hii, kwa kuwashukuru wadau wangu wote kwa support yenu,
Leo ni siku yangu rasmi nakuja kwenu kuwaeleza kua tumefungua website yetu... Tunawaomba comments zenu, za ushauri wowote ule kwa jinsi mtakavyo iona kama tubadilishe nini, iweje ili iweze kua nzuri na ya kuvutia, ama hivyo ilivyo inatosha
Sasa basi,
Website hii iko pamoja na blogsite, blog itaendelea kuwepo, ila ukiingia kwenye blogsite kama tulivyozoea hutoweza kuona changes, ila ukiingia kwa address hii hapa chini utaona changes, na kuna vingi vipo, na vinaendelea kuwepo kutokana na mahitaji yenu.........,
kingine ni kwamba website yetu hii iko tofauti kidogo, kwani utaweza ku Scroll up & Down, topics, na matangazo yakawa pale pale.........ama kama tulivyo zoea ukatumia ya pembeni......
Nina furaha sana sanaaa, maana ukimya wangu ni ilikua kwa ajili ya website hii yangu iweze kuwa tayari mwanzoni mwa mwezi huu kama nilivyo ahidi....Mungu ni mwema na namshukuru kwa kila jambo...
Kuazia sasa Mtakua mkiingia kwa kupitia address hii: http://www.homezdeco.co.tz
Karibuni......

Color Schemes.........Wapenda ipi wewe?





Umegundua nini kwenye utandikaji wa vitanda hivi?







Thursday, May 3, 2012

Kazi ya Homez Deco-Kreative Homez, Site- Mbezi Beach.....











Ni vitanda vya four poster, design 2 tofauti, na wengi wenu mmekua na maswali kua vitanda hivi vinakuaje na je kama ni imara, jibu ni kua vitanda ni imara tena kuliko mbao, maana mbao asilimia kubwa zinaliwa na wadudu;
Ukubwa wa vitanda hivi ni 4 by 6, na tumeweka godoro la 4 by 6 inch 8....(hatutoa karatasi za godoro maana bado kuna kazi zinaendelea......yasichafuke) na godoro waweza kuweka lolote lile kulingana na uwezo wako na kukapendeza.
Karibuni sana mtoe orders......

Tuesday, May 1, 2012

Nimewagusaaa eheheee!!!!






Inafika pahala sasa tuambizane ukweli....., watanzania asilimia kubwa hatuna hela si ndio ehee, ila hao hao utawakuta wanavaa vizuri, tena vitu vya designers, kama ndio nguo, cheni, viatu (CL) ndio vimeingia maana navisikia tuuu, lace wig kuchangia sherehe kwa kiasi kikubwaa cha fedha etc.

Wanakokaa hapafai na ni aibu jamani, yaani unamkuta mtu nje mrembo kavalia huyoooo, gari zuri ila nenda home kwake, jamani, unaweza ukakataa lol...

Hivi kweli uki save hela yako hiyo ukasema sasa mwezi huu ama miezi miwili sinunui nguo wala viatu etc, natengeneza nyumba yangu, kama ni yakupanga ama ya kwako, utashindwaaaa kweli, ama ndio kupanga kuchagua....

Hebu tujirekebishe sasa, na tuanze kupenda nyumba zetu, maana maisha yetu yanategemea sana nyumba zetu, na ukiipendezesha nyumba yako, basi na hata safari usizozipangilia na mafoleni haya kumaliza mafuta ya gari, na uchovu hata kama unapanda basi, zitapungua na utakua unarudi home kwako moja kwa moja kwa amani, na utapumzika kwa amani.....


Ni hayo tuuu kwa leo.........TUBADILIKE, NA HILI LINAANZA NA WEWE, SIE WENGINE NI WATAZAMAJI TUUUUU UKIJIBANA KWA MUDA UNAWEZA KUPAMBA NYUMBA YAKO NA IKAWA NZURI TENA ZAIDI YA HIZI............



1 Room, 2 looks






Picha zinajieleza jamani ama sio...........