Monday, March 4, 2013

Ofisi za Homez Deco .........& tumekua ni wakala halali wa rangi za Dulux. (Sadolin Paints Ltd)

Ninayofuraha kuwajulisha kua sasa Homez Deco ni wakala halali wa Dulux Paints.....na Sadolin Paints......Tutakua tunatengeneza rangi hapa hapa ofisini, na unaondoka nayo ndani ya dakika ama saa kulingana na ukubwa wa order yako......Rangi aina zote zinapatikana hapa, za nje, za ndani etc......Tuna catalogue ya rangi zaidi ya rangi 3200...........

Ninamshukuru Mungu kwa mema yote anayonitendea na anayoendelea kunitendea.......Mungu ni mwema kwetu sote.....

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wadau wangu wote, maana bila ninyi nisingekua na mafanikio haya niliyo nayo.........
Shukrani zingine ziwaendee wateja wangu wa rangi ambao ndio walioniwezesha mpaka hapa nilipo, Mrs. Pamela, Mrs. Consolata, Dr. Sara, Mr. Anthony, na wengineo wengi.........hawa ni baadhi tuu ambao watawawakilisha wenzao kwenye shukrani hizi......


 Huu ndio muonekano mpya wa ofisi za Homez Deco.......kwa nje......wafanyakazi wa Sadolin paints, wakileta machine za kutengeneza rangi.......
 Gari likiwa limeteta machine za kutengeneza rangi na kuchanganya.....
 Muonekano wa nje ya ofisi.....

 Ndani ya ofisi zetu......hiyo ni display ya decorations kama inavyoonekana.......

Ofisi kwa ndani........na waiting area............Kama ofisi yetu inavyoonekana, ni ndogo, sasa basi vitu vingi kama furniture, etc ni vya kutoa order ndio utengenezewe.......na mungu akipenda tukija kukua, basi tutakua na ofisi kubwa na asilimia ya vitu vingi mtavikuta viko tayari......Kuna msemo usemao, hata mbuyu ulianza kama mchicha........
Hizi ndizo machine za kutengeneza rangi za dulux.........

Hii ndio color chart ya dulux tuliyonayo ambayo ina rangi  zaidi ya 3200. Kila rangi ina namba yake.....hivyo hakutakua na usumbufu wa kutoka rngi ambayo haukuichagua........Tunakukaribisha pia ukiwa na rangi zako binafsi tutakutengenezea pia.....

Ofisi zetu zinafunguliwa kuanzia saa 9:00 am - 7:00 pm......

Ofisi zetu ziko Kinondoni makaburini, kituo cha basi mwembeni,unaingia barabara ya kulia ya vumbi kama unatokea mjini unakuja nayo mbele kidogo kuna maduka kulia kwako..duka letu ni la kwanza kutoka barabarani..... Karibuni.

Tuwasiliane 0713 - 920565

NB:
Hii ndio sababu ya ukimya wangu, ni katika kuandaa ofisi....


4 comments:

 1. Hongera sana uzidi kubarikiwa. mi nilikuwa nauliza je hata kama nahitaji kuchanganyiwa rangi ya lita 5 means lile kopo dogo inawezekana na ni bei gani.

  ReplyDelete
 2. Asante sana.....kwa upande wetu wa Dulux, tunachanganya rangi kuanzia lita 5, rangi yoyote ile unayoitaka....kwetu inawezekana...na kuhusu bei, itanibidi nijue ni rangi gani unahitaji.....
  karibu

  ReplyDelete
 3. kwa mfano hiyo lita 5 nyeupe ?itakuwa sh ngapi?

  ReplyDelete
 4. WELL DONE U MAMA.U MAKE US WOMEN PROUD.MUNGU AKUZIDISHIE

  ReplyDelete