Friday, December 30, 2011

Natanguliza Shukrani Zangu kwenu wadau wangu

Tangu nimeanzisha blog hii ya Home Decoration (Interior Design & Landscaping), mwaka 2009/August, Nashukuru imepokelewa vizuri na wadau wangu, na imenipatia, wateja, marafiki, na pia tumeweza ku maintane kua ni blog ya decor na si vinginevyo....

Nina mengi ya kuongea ila ngoja niyafanye mafupi.....

Kuanzisha kwangu blog hii ni kwamba nilitaka huduma hii iwafikie watu wengi zaidi, na iweze kuwasaidia, na kweli nimefanikisha hilo, wengi wanafanya decor kwa ushauri ninaowapa, wengine kwa kunitumia email, simu, sms. tena wao wenyewe bila mie kuwepo

Mmeweza pia kunivumilia pale ambapo ninachelewa ku update, hasa kipindi ambacho nilikua mjamzito, na sasa ninalea, kwa hiyo ninatakiwa ni balance muda, kwa haya yote, na nimeweza kufanya hivyo.

Ninachoweza ni kuwashukuru sana sana sana, na ninaomba mtarajie mengi, mengi mapya, kwani nimekua nikifanya projects, ya jinsi gani ya kuweza kuwasaidia katika kuelimishana.

Kama kuna mahali nimewakosea, ama niliteleza, tusameheane, nami pia nimewasamehe wote wale walionikosea.

Mwaka 2012 ninataka kuukaribisha vizuri na ninafuraha sana sana, kwani nitakua na mtoto wangu Jaydan, I'm proud to be a mum (single mum) hakuna kinachoshindikana ukimuomba mungu na kuamiani.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote waliokua nami katika kipindi chote cha ujauzito mpaka sasa na tunaendelea kushirikiana, kwani hao ndio marafiki wa kweli, sio kweye raha tuuuuu.......

Nawatakia Muukaribishe mwaka mpya salama. Nawapenda woteeee

Sylvia a.k.a mama Jaydan

No comments:

Post a Comment